Utaratibu wa kuishi na ndugu baada ya ndoa unafaa uwe vipi?

Utaratibu wa kuishi na ndugu baada ya ndoa unafaa uwe vipi?

Sidhani! Labda ungesema Wajaluo,Wagogo,Wasambaa ningekuelewa! Lakini changamoto ni kuoa ukoo maskini.
Wala sio ukoo masikini bali ukoo wa wa wapumbafu sijui niite wasio jielewa ambao akili zao hazina akili, umasikini sio sababu nikujitambua tu.
 
mkuu tafuta gheto lako self safi kabisa uwe unaishi huko unapunguza stress na uache kununua chakula home na hivi huna mtoto
 
Mimi kiukweli sipo kwa dini yeyote hapa nasema uhalisia tu experience.
Sikia nilikuwa kwenye mahusiano na jamaa ni muislamu anaitwa salim huyu jamaa ni alinipenda sana tu.
Ila chanzo nu ndugu asubuhi wanakuja na watoto zao wanakaa hadi usiku .

Wanapika wanamuomba huyo ndugu yao hela wanaondoka hivyo.
Hadi siku moja nikawa na msimamo nikaamua niwachambee.
Wakanikoma kikaisha.

So wachambee
 
Familia zetu tumezoea kuishi kiujamaa Kama wahindi na waarabu
kuna raha gani ya kuishi mtu na mke tu?
Kama nyumba kubwa acha watu waishi.
Kila kitu kiwe na kiasi hakuna asie penda ndugu, sasa mnajazana utazani hostel ndoa inatakiwa kuwa na staha unaishi kwa kujibana bana sasa mzee mzima kwa mdogo wako na wajukuu si ujinga huo, mwishowe shemeji yake adondoshe taulo bure ujinga tu .
 
sema wananiona mpole kuna kaka zao kabisa wako vizuri kipesa lakini kwao hawakanyagi, ila kwangu kila wikend nilishaanza wabania pesa wanakuja kwa machale, shida hawa wamama hapa nyumbani mtu ana 47 ana watoto watatu, mtoto wake wa kwanza kaolewa ila hajawhi enda ishi na mkwe wake ila hapa kwa mdogowake ndio amefanya kwake.
Wewe hata usimwambie unataka kupanga, wewe siku hiyo jioni panga vizuri vitu vyako na usimwambie umepanga wapi, asubuhi weka kwenye gari lako vitu muhimu kama unasafari vile jioni tuma SMS tu, mwambie wakiondoka utanijulisha, halafu anza kuacha pesa ya kila siku kama ni buku 10 gas ikiisha usinunue nunua mkaa, usijaze vyakula ndani!
 
Ambao hawakumuelewa Dinazarde kwenye uzi wake,,,,Basi hiki ndicho Hasa alichokuwa anakizungumza...

Na nawaomba mtumie kisa cha Mleta uzi kama mfano wa kufundishia

Na alishambuliwa sana
 
Habari za siku nyingi watu wa Mungu.

Hivi ni utaratibu gani unafaa kufuatwa katika kuchagua ndugu wa kuishi nao baada ya ndoa. Nakumbuka mwanzo kabisa kipindi namuoa mke wangu nilimjulisha kuwa napenda sana ndugu ila kuishi na ndugu ni mtihani kama mtu ana uhitaji na tuna uwezo wa kumsaidia bora tumsaidie huko huko aliko kukiwa na ulazima sana ndipo ataishi kwetu.

Bahati mbaya huyu mwenzangu na ndugu zake wamefanya nyumba yangu kijiwe ndugu zake wote wapo hapa hapa mjini sasa imekuwa anakuja huyu anakaa wiki anaondoka wanapokezana , likizo watoto zao wanawaleta kwangu na wana vurugu kweli ile likizo ya mwaka mpya walinivunjia side mirror ya gari ikabidi niwafukuze manake walikuwa wakiaanza kukimbizana wanapita mpaka juu ya makochi ilibaki kidogo wakanyage kompyuta niliwafukuza siku hiyo hiyo.

Tatizo la pili kuna ndugu zake hawa watu wazima wakike ambao ni dadazake ni wakubwa kiasi mmoja binti yake ndiyo mwenye watoto niliowafukuza, hawa wanakaa tu nyumbani hawafanyi chochote ni kuangalia tu tamthiliya mpaka kurudi nyumbani sasa naona kero mimi na wife hatujajaliwa watoto sasa hapo nyumbani kuna familia ya watu 4 na wote wanatokea hapo mabibo yaani mimi ndio nimekuwa kama mgeni kwenye familia.

Nikimuambia hawa watu kwanini wasirudi kwenu kwenye nyumba ya familia wakae sisi tutakaa nao mpaka lini anasema soon wataondoka toka mwezi wa pili anasema hivyo soon wataondoka, karibuni mama anataka kuja kwenye matibabu MOI ila kagoma kufikia kwangu hawezi lala kitanda kimoja na mtu mwingine anashida na mifupa.

hapo bado kuna ndugu zake wanakuja tu wikend wakijisikia na wakiondoka hawana nauli wanakuomba tena shemeji nauli hasa namuuliza hawa nao wanakuja kila wikend kufanya nini, anasema kama sitaki ndugu zake waje atawaambia ila tatizo sio kuja tatizo hata nauli hawana ukiwapa ndogo wanakuimbia kuna sehemu ya kupanda bodaboda.

Ajabu wao wenyewe kwa wenyewe hawatembeleani ni kama vile wanaamua kunimalizia pesa hivi. Nipeni busara kudeal na hawa watu nahisi kuanza kukata mahitaji.
Mkuu kama hutajali chukua ushauri wa jamaa fulani aliwahi kicomment humu jf ,
Ndugu walipomtembelea,alimpigia rafiki yake simu ambaye anafanya kazi hospital..
Akauliza nafasi zipo?rafiki yake akamwambia zipo .
Basi aliwabeba wale wageni Hadi hospital wodini ..akawalaza huko..
Kesho yake asbh akawahi kuwachukua.

Walivyofika tu walifunga safari na kuaga.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Kama huwataki kwako waambie ukweli, acha kutia huruma mwanaume. Na kama huna hiyo bajeti ya nauli waambie hauna acha kulialia jf…otherwise kaa chini na mkeo umwambie ulimuoa yeye hukuoa familia.

Alafu acha uchoyo mkuu[emoji1787] japo hiyo hali inakera[emoji2314]
Uchoyo tena...wanawake ndio wachoyo balaa wanamnyima hadi mume mbususu ambayo ameilipia kwa ng'ombe kadhaa
 
Mbona familia yetu masikin na hatuna tabia yakwenda majumbani Kwa watu tokea wadogo tulilizika na maisha ya home kipatikane chakula kisipatikane hatukuwai kuwaza kwenda kuishi Kwa ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
Si umasikini ni akili kushindwa kufikiri vizuri ujinga tu, tumetoka familia duni lakini tuliridhika na hali zetu
 
Tatizo naliona hapo ni ndugu wa upande mmoja tu kufanyiwa ukarimu wa (yaani ndugu wa mke tu).

Sasa utashangaa ndugu wa mume wakijaribu kutia Maguu hapo tayari mashtaka yataanza
Kwa mume ooh Huyu fulani ndugu wa mume anatabia mbaya hii na ile …….

Yani ubaya na udhaifu mke anauona kwa ndugu wa mume tu lakini Kwa nduguze haonagi ubaya wowote zaidi ya mema tu ?!

Imagine [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Habari za siku nyingi watu wa Mungu.

Hivi ni utaratibu gani unafaa kufuatwa katika kuchagua ndugu wa kuishi nao baada ya ndoa. Nakumbuka mwanzo kabisa kipindi namuoa mke wangu nilimjulisha kuwa napenda sana ndugu ila kuishi na ndugu ni mtihani kama mtu ana uhitaji na tuna uwezo wa kumsaidia bora tumsaidie huko huko aliko kukiwa na ulazima sana ndipo ataishi kwetu.

Bahati mbaya huyu mwenzangu na ndugu zake wamefanya nyumba yangu kijiwe ndugu zake wote wapo hapa hapa mjini sasa imekuwa anakuja huyu anakaa wiki anaondoka wanapokezana , likizo watoto zao wanawaleta kwangu na wana vurugu kweli ile likizo ya mwaka mpya walinivunjia side mirror ya gari ikabidi niwafukuze manake walikuwa wakiaanza kukimbizana wanapita mpaka juu ya makochi ilibaki kidogo wakanyage kompyuta niliwafukuza siku hiyo hiyo.

Tatizo la pili kuna ndugu zake hawa watu wazima wakike ambao ni dadazake ni wakubwa kiasi mmoja binti yake ndiyo mwenye watoto niliowafukuza, hawa wanakaa tu nyumbani hawafanyi chochote ni kuangalia tu tamthiliya mpaka kurudi nyumbani sasa naona kero mimi na wife hatujajaliwa watoto sasa hapo nyumbani kuna familia ya watu 4 na wote wanatokea hapo mabibo yaani mimi ndio nimekuwa kama mgeni kwenye familia.

Nikimuambia hawa watu kwanini wasirudi kwenu kwenye nyumba ya familia wakae sisi tutakaa nao mpaka lini anasema soon wataondoka toka mwezi wa pili anasema hivyo soon wataondoka, karibuni mama anataka kuja kwenye matibabu MOI ila kagoma kufikia kwangu hawezi lala kitanda kimoja na mtu mwingine anashida na mifupa.

hapo bado kuna ndugu zake wanakuja tu wikend wakijisikia na wakiondoka hawana nauli wanakuomba tena shemeji nauli hasa namuuliza hawa nao wanakuja kila wikend kufanya nini, anasema kama sitaki ndugu zake waje atawaambia ila tatizo sio kuja tatizo hata nauli hawana ukiwapa ndogo wanakuimbia kuna sehemu ya kupanda bodaboda.

Ajabu wao wenyewe kwa wenyewe hawatembeleani ni kama vile wanaamua kunimalizia pesa hivi. Nipeni busara kudeal na hawa watu nahisi kuanza kukata mahitaji.
Kwani we dini gani ? Kama ni muislam dini inatoa muongozo kwenye mambo ya ugeni mgeni anatakiwa asikae zaidi ya siku 3 ugenini ni rahis sana kuwakimbiza kwa kutumia njia za kiimani usiishi kwako kama msela nondo lazima uweke misingi yani simamia upande mmoja kua strict watu hao wanapenda anasa ikiwezekana siku wakiwa wanakuja we geuza siku ya ibada yani muite shekh au mchungaji pigeni maombi bila kula[emoji16] alafu unawaambia kabisa kwangu ni lazima wote mmshiriki ibada mnapiga dua tu siku nzima apo hata mke wako mwenyew anaweza kimbia usipoangalia
 
Mkuu kama hutajali chukua ushauri wa jamaa fulani aliwahi kicomment humu jf ,
Ndugu walipomtembelea,alimpigia rafiki yake simu ambaye anafanya kazi hospital..
Akauliza nafasi zipo?rafiki yake akamwambia zipo .
Basi aliwabeba wale wageni Hadi hospital wodini ..akawalaza huko..
Kesho yake asbh akawahi kuwachukua.

Walivyofika tu walifunga safari na kuaga.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
hahaa ngoja nimtag hapa ......😂😂

Huyu hapa Ushimen
 
Nimesikitika hadi hapo hujawala shemeji zako, mbuzi kufia buchani bahati iliyoje.!!
 
Kiongozi nikupe tu ushauri ,ndgu hawabebiki na huwa wanamthamini wakati mtu ana kitu ,
Mtakupa historia fupi ya mzee wangu (binafsi nimepata funzo ) kipindi mzee ana uwezo na mali zake ,nyumbani watu hawakauki ,ndgu walijaa kibao mpaka sisi watoto tukawa tunaminyika au kupunjika maswala ya msosi kwa ajili yao ,maana alikuwepo ma mdogo akijipakulia basi alikuwa anajijazia yeye na sisi kutupunja chakula ,hiki kitu huwa sikisahau mapaka utu uzima huu,Baadae mzee alikuja filisika sana na ndgu hawaji hata kusalimia ,jambo ambalo lilikuwa likimuumiza mama na alikuwa akinilalamikia ,wanavyonyanyapaa ndgu zake kisa hana kitu ,kama mtoto ilikuwa inaniumiza sana ,ni kaapa ntatafuta maisha kwa hali na mali ,
Si haba kwa sasa nnakijiuwezo ,kiasi na nimekuwa na msimamo ,familia yangu kwanza (mke watoto baba na mama ) hao wengine wanasubiri ,Habari mtu kaja kwangu kutembea bila taarifa huwa sitoi nauli hata kama ninayo maana ukiwazoesha huwa wanajenga tabia ,Na ukiwaonyesha kwamba ww unazo watakufanya chuma ulete ,siku huna kitu watakukimbia ,
Nimewekeza nguvu na akili katika kujijenga mm kwanza bila kumtanguliza mtu mwingine na hata nnachopata juwa najitahidi kuwaneemeshe familia yangu na wazazi wangu ,Hao wengine nasaidia panapouhitaji ,
Pia nimeweka msimamu kuwa sibebi mzigo wa mtu (kwa kulea mtoto wa mtu) mimi mwenyewe nimejibana niwe nawatoto wachache ili kuwapa malezi bora ,Kila mtu abebe msalaba wake ,
Usiposimama imara na kuwajengea watoto wako msingi imara kesho na kesho kutwa hao hao ndgu watakuja simanga watoto wako na kuwaambia baba ako alikuwa na pesa ila akachezea ,watasahau kwamba ulikuwa unajitoa kwao na wamesababisha kushinda kuwatimizia watoto wako kwa kuwajengea misingi mizuri

Kwenye hiyo unayoita familia yako i.e wewe mkeo watoto na wazazi wako, sijaona wazazi wa mkeo…. au hujui kuwa hiyo ni familia ya mkeo ambayo ni yako.!
 
Napenda sana kuishi na ndugu, yaani napenda familia kubwa ila hofu yangu ni migogoro ya hao wageni wenyewe kwa wenyewe au kuniharibia familia yangu.

Nikifanikiwa kudhibiti hiyo hali tu maisha ni murua kabisa kwenye palace. Sina wasiwasi kuhusu vitu vidogo kama vyakula sijui tamthilia, chakula uhakika ndo fahari yangu kama baba.

Mleta mada unalialia hapa kwa vile ni ndugu wa mkeo wanajazana hapo kiasi cha ndugu zako kukosa nafasi, mkeo naye anatetea nduguze.

Tafrani.
 
Back
Top Bottom