Kiongozi nikupe tu ushauri ,ndgu hawabebiki na huwa wanamthamini wakati mtu ana kitu ,
Mtakupa historia fupi ya mzee wangu (binafsi nimepata funzo ) kipindi mzee ana uwezo na mali zake ,nyumbani watu hawakauki ,ndgu walijaa kibao mpaka sisi watoto tukawa tunaminyika au kupunjika maswala ya msosi kwa ajili yao ,maana alikuwepo ma mdogo akijipakulia basi alikuwa anajijazia yeye na sisi kutupunja chakula ,hiki kitu huwa sikisahau mapaka utu uzima huu,Baadae mzee alikuja filisika sana na ndgu hawaji hata kusalimia ,jambo ambalo lilikuwa likimuumiza mama na alikuwa akinilalamikia ,wanavyonyanyapaa ndgu zake kisa hana kitu ,kama mtoto ilikuwa inaniumiza sana ,ni kaapa ntatafuta maisha kwa hali na mali ,
Si haba kwa sasa nnakijiuwezo ,kiasi na nimekuwa na msimamo ,familia yangu kwanza (mke watoto baba na mama ) hao wengine wanasubiri ,Habari mtu kaja kwangu kutembea bila taarifa huwa sitoi nauli hata kama ninayo maana ukiwazoesha huwa wanajenga tabia ,Na ukiwaonyesha kwamba ww unazo watakufanya chuma ulete ,siku huna kitu watakukimbia ,
Nimewekeza nguvu na akili katika kujijenga mm kwanza bila kumtanguliza mtu mwingine na hata nnachopata juwa najitahidi kuwaneemeshe familia yangu na wazazi wangu ,Hao wengine nasaidia panapouhitaji ,
Pia nimeweka msimamu kuwa sibebi mzigo wa mtu (kwa kulea mtoto wa mtu) mimi mwenyewe nimejibana niwe nawatoto wachache ili kuwapa malezi bora ,Kila mtu abebe msalaba wake ,
Usiposimama imara na kuwajengea watoto wako msingi imara kesho na kesho kutwa hao hao ndgu watakuja simanga watoto wako na kuwaambia baba ako alikuwa na pesa ila akachezea ,watasahau kwamba ulikuwa unajitoa kwao na wamesababisha kushinda kuwatimizia watoto wako kwa kuwajengea misingi mizuri