Utaratibu wa kulazimisha mtoto wa kwanza kuanza kufunga ndoa kwanza kisha ndio wafuate wadogo zake

Last born vs last born nimekuwahi kuelezea pale juu[emoji1787]
Katika makosa siji kufanya basi ni kuolewa na last born wallah sitaki [emoji23][emoji23][emoji23]
Last born ni mtoto wa mama,yaani mbona katashinda na njaa kila siku [emoji1787]
Sema nyie ma-last born nawapendea kitu kimoja tu! Huwa hamtaki kutoka home, na ukiona last home ameiacha nyumba alipo mama ake, basi ni vile tu hana jinsi!!

Mimi binafsi mambo ya kuishi home nilikuwa siyapendi tangu nikiwa kavulana!! Na ile nimepata kanafasi ka kuingiza tusenti ka kula, fasta nikahamia zangu Uswahilini!!

Madogo wangu wengine na wenyewe wakavunja hadi rekodi yangu; manake yale majamaa yalianza kujitegemea wakati hata makamasi hayakauka!! Nakumbuka mmoja wao ilikuwa ugomvi home... Bi Mkubwa hadi anaenda alikopanga na kwenda kutoa vitu ili arudi home, lakini haikusaidia hadi akaacha!!

Huyo Last Born sasa!!

Kuanzia akiwa A-Level hadi chuo, ingawaje alikuwa anaishi hostel, piga ua Ijumaa lazima arudi kwa mamake!!!

Leo hii ingawaje uwezo wa kujitegemea anao huku akiwa 26, lakini bado yupo home na wala haielekei kama ana mpango wa kuhama leo au kesho...

Yaani hii ndo inayonifanya nimpende yule dogo manake at least home kuna mtu wa uhakika baada ya sie wengine kukimbia home mapema!!

Na nyie wanawake mkishaolewa, bora muwe mnaishi mbali vinginevyo itakuwa kila wakati hodi hodi badala ya kutulia kwa waume zenu!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi ni watu wa uhakika kabisa tunabaki nyumbani
Nyumba inakuwa kwenye mikono salama

Kwahiyo nyie mkamkimbia bimkubwa mapema[emoji28]Hamfai nyie[emoji23]
 
Waafrika tunaongozwa na matarajio ya jamii, na matokeo yake, katika harakati za kutaka kuyafikia matarajio hayo, wengi wanajikuta wanafanya makosa yanayobaki kuwa kidonda cha maisha yao!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi ni watu wa uhakika kabisa tunabaki nyumbani
Nyumba inakuwa kwenye mikono salama

Kwahiyo nyie mkamkimbia bimkubwa mapema[emoji28]Hamfai nyie[emoji23]
Lakini kweli aisee! Unajua Bi Mkubwa hajakaa kabisa na watoto wake except haka ka-last born ambako ndo kameendelea kuishi nae hata baada ya kuwa "keshamaliza" chuo!!!

Sema sie wengine tulisepa wakati Bi Mkubwa akiwa bado "msichana"! Tena si unajua kama sie ma-first born! Mtu unafikisha 20 something wakati ndo kwanza Bi Mdashi na mwenyewe akiwa in early 40's; kwahiyo hata ukimkimbia, poa tu!!!

Sema nyie last born ambao mnafika 20's wakati madingi wapo 60's ndo hamtakiwi kuondoka home!!!
 
Vitu vingine ni upuuzi mtupu.sasa kwa Nini walipokea mahari wakati wanajua hawatomuoza binti yao,.!
 
Kama unanisema Mimi, nilipokuwa 20s wazazi wangu walikuwa 60s
 
Update
Habari za toka jana wana MMU sio siri siku ya leo ilikua ni siku ndefu sana kwangu katika wiki hili hasa ni kuhusu hizi changamoto za maandalizi ya hii ndoa.

Basi bana asubuhi na mapema tulijianda na kuanza safari ya kwenda ukweni nashkur tulifika salama na tulipokelewa vyema kabisa na kama tulivyo kubaliana na wazazi wa bint kikao kilianza.

Kwa upande wa bint walianza kuongelea historia fupi ya ukoo na familia yao kwa ujumla na kusisitiza kuwa ni aibu, fedhea pia ni kumvunjia heshima mzaliwa wa kwanza (dada mtu) endapo bint yao mdogo ataanza kuolewa kabla ya dada mtu.
Hivyo japo kuwa kwenye kikao cha mwisho tulikubaliana na kuwekeana ukomo wa muda wa kumsubiria bint mkubwa lakini msimamo wa wazee ulikua palepale.

Aysee....! Ukimya ulitawala kisha na sisi wa upande wa bwana harusi mtarajiwa tukanza kuongea;

Ujue tulihitaji kufahamu kama wanahitaji ndoa ya bint yao ama laa (hapa walijibu kuwa wanahitaji)

Pia tukahoji je, wanafahamu ni mwaka gani bint yao mkubwa ataolewa (hapa walikosa jibu)
Hivyo basi tukawambia itakua sio busara kusubiria kitu ambacho hakipo na hatujui kitatokea mwaka gani na wala hakina dalili yoyote. Pia kwanini suala hili halikuwekwa wazi kipindi cha kupokea barua ya uchumba na likaja kuibuliwa wakati wakiwa wameshapokea mahari ni dhahiri walikua tayari kumwozesha bint yao ila hizo mambo zao za mila za ukubwa ndio zinazoleta mkwamo wa ndoa, na kama hali hii ya usumbufu ikiendelea tutaghairisha kuoa bint yao pamoja na kudai kurudishiwa gharama zetu zote.

Jamani wale wazee wao wa familia wana misimamo hatari yaani hadi kikao kinamalizika ilikua bilabila hatukupata muafaka wowote ila tumewapa muda wa wiki mbili wajitafakari kisha watupatie majibu.

Tumeondoka tumemwacha bibi mtu na bint mdogo (mtarajiwa) wanalia kwa kama wamefiwa vile.
 
Basi unajiona mkubwa mwenyewrme na wakati tupo wote kwenye 30's[emoji16]
[emoji2098][emoji2098][emoji2098]
 
Ila hii familia nayo ni kiboko chaa!!
Yaani watu hadi wanapeleka mahari halafu wanagomea ndoa!!
Si wangekataa tu mwanzo wamkatalie binti kuleta mtu
 
Ila hii familia nayo ni kiboko chaa!!
Yaani watu hadi wanapeleka mahari halafu wanagomea ndoa!!
Si wangekataa tu mwanzo wamkatalie binti kuleta mtu

Nadhani kuna jambo wanatuficha na kwahili joto tulilowaongezea natumai ukweli tutaubaini
 
Nadhani kuna jambo wanatuficha na kwahili joto tulilowaongezea natumai ukweli tutaubaini
Yaani hivi kwamba wanawaona nyinyi ni wapumbavu Kiasi hicho!?!

Kama mila zao zipo hivyo kwanini wasingewakatalia mapema kabla hamjaanza mchakato??!
Yaani wamewakuta nyie wavumilivu mno..ningekuwa mimi wallah ningekuwa nishavuruga vikao kitambo.
 
Mimi pia sijaolewa...Ila ningependa kuwa na familia yangu...NINA VIPAUMBELE LAKINI HICHO NACHO KIMOJAWAPO
Familia muhimu, Ila yapasa kujiandaa as a woman lazima utimize ndoto zako kwanza since ukiingia ndoani lazima uzike ndoto zako Kama ulikuwa hujazitimiza.
 
Waafrika tunaongozwa na matarajio ya jamii, na matokeo yake, katika harakati za kutaka kuyafikia matarajio hayo, wengi wanajikuta wanafanya makosa yanayobaki kuwa kidonda cha maisha yao!
Na wengi wanaishi na machungu mengi ili kufuraisha jamii loh, honestly Mimi furaha na amani ya moyo wangu Ni muhimu kuliko jamii wanachofikiria
 
Kwa kweli huo utaratibu kwetu haupo. Kila mtu ana wakati wake na bahati yake: atakayewahi anasonga mbele na harusi yake. Siwezi kuacha wakati na bahati yangu vinipite kisa kumsubiri mtu.

Nilishawahi msindikiza ndugu kutoa mahari sehemu; mtarajiwa alikuwa ni dada mdogo. Ndo kuja kutuambia ilibidi wamuulize kwanza dada mkubwa kama ameridhia; na yeye alikuwa ameridhia. Sikuona umuhimu wa kumuuliza dada mkubwa. As a matter of fact kila mtu ana mipango yake; mwingine labda hajawaza kuolewa bado. Ndo ukae unamsubiri tu hadi aje awe tayari kuolewa na ampate wa kumuoa khaaa
Hao wazazi wenye akili hizo nina hakika wanatoka nyanda za juu kusini [emoji1787][emoji1787][emoji1787]!!! Wanakuaga na misimamo ya kingese kweli. Heaven Sent ongea na washua tutaisusa hio mahari yetu sio ishu
 
Mimi naomba unieleweshe kidogo mdogo angu. Kwa mfano wewe ndiyo ukatangulia kuolewa; huyo dada ako utakuwa umemvua nguo kivipi kwa kuolewa kabla yake?
 
Familia muhimu, Ila yapasa kujiandaa as a woman lazima utimize ndoto zako kwanza since ukiingia ndoani lazima uzike ndoto zako Kama ulikuwa hujazitimiza.
@cariha haupo sahihi kabisa dada yangu

Kwa hiyo kama hutotimiza ndoto zako hutoolewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…