Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Ninamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.

Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili

B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni

C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?

D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?

E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?

F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?

Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.

Asante.
Hata baiskeli huna!!!...

Level zako ni za kuwaza ununue labda bodaboda ama Bajaj nakupeleka mbali!!!

Ya ngoswe muachie ngoswe..... Ya kaisari mwachie kaisari!!!...
 
Ninamaanisha dege ndogo ya kawaida (aeroplane) yenye uwezo wa kubeba abiria watatu na helikopta yenye uwezo wa kubeba abiria watatu.

Naomba kufahamishwa:
A. Bei yake ikijumuisha gharama za ununuzi, usafirishaji na usajili

B. Makadirio ya gharama za kuihudumuia kwa mwezi. Wastani wa safari zake kwa mwezi ni kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam Asubuhi na kurudi Mwanza Jioni

C. Kuna ulazima (Kisheria) wa kuwa na "pilot" zaidi ya mmoja?

D. Kuna unafuu wa gharama (tozo za Serikali) ikiwa itamilikiwa na taasisi ambayo ni non-profiti organization?

E. Utaratibu ukoje kuhusu parking?

F. Sheria inaruhsu kupaki helikopta nyumbani au kwenye uwanja wa ofisi ya taasisi?

Ikiwa kuna taarifa zingine zozote ninazopaswa kufahamu naomba nisaidiwe.

Asante.
That's Bravo Roger
 
Ndege ndogo Cessna grand caravan used....ni bei nafuu kuliko.... unavyofikiri...
Ni nafuu kuliko Toyota coaster used.
TRUST ME
Mkuu, comment yako imenichekesha, imenikumbusha jambo fulani lililoonekana kama kituko kipindi hicho.

Miaka ya nyuma, Redio One, kwenye moja ya vipindi vyake viilivyokuwa vikihusika na taarifa zisizo za kawaida (sikumbuki jina la kipindi), ilitangaza kuwa gari la matangazo lilikutwa Soko Kuu Arusha likinadi ndege iliyokuwa uwanja wa ndege wa Arusha.

Upekee wa habari yenyewe ni kitendo cha wahusika kwenda kuzitangaza habari hizo kwa wauzaji wa mboga mboga, matunda, n.k.

Sasa kama ni kweli ndege used Cessna grand caravan ni rahisi kuliko Toyota Coaster Used, hakukuweko na uajabu wafanyabiashara wadogo kutangaziwa hilo. Wakiungana watu kadhaa mbona wanaichukua!
 
anaujuaji gani au hujui ukiwa na njaa unavyoweza kuwazq vitu vya ajabu ili ujifariji
Siamini kwamba mtoa mada alikuwa na njaa, na kama alikuwa na njaa, basi njaa yake ilikuwa nzuri. Inasemekana, akili humfanya kazi kwa Kasi zaidi mtu anapokuwa na njaa kuliko anapokuwa ameshiba. Shibe huweza kuchochea uvivu wa kufikiri.

Kwa hiyo kama ni njaa ndiyo iliyompekekea awaze kununua ndege, ni Bora awe anafunga mara kwa mara hadi atakapoifikia ndoto yake.
 
Huwezi kuipaki nyumbani kwako inapaki airport labda iwe helcopter, hapa kuna parking fee, huwezi kuruka bila ruhusa na unalipia ukirusha, hiwezi kutua bila ruhisa na unalipia ukitua. Inshort usumbufu tuou
Unaweza kuipaki chopa nyumbani?
 
Back
Top Bottom