Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Utaratibu wa kumiliki ndege ndogo Tanzania ukoje?

Huwezi kuipaki nyumbani kwako inapaki airport labda iwe helcopter, hapa kuna parking fee, huwezi kuruka bila ruhusa na unalipia ukirusha, hiwezi kutua bila ruhisa na unalipia ukitua. Inshort usumbufu tuou
Ndio maana miaka ya nyuma angalau Wakulla kadhaa waliegesha ndege zao kwenye mashamba yao.
 
Sorry wakulima.i.e.Herman Steyn etc
Wakulima walikuwa wanamiliki ndege?

Ndiyo zile, inasemekana, zilizotaifishwa na Serikali kipindi, nafikiri cha Nyerere?

Kumbe si kitu cha ajabu kivile kwa mtu binafsi kumiliki ndege Tanzania!
 
Siamini kwamba mtoa mada alikuwa na njaa, na kama alikuwa na njaa, basi njaa yake ilikuwa nzuri. Inasemekana, akili humfanya kazi kwa Kasi zaidi mtu anapokuwa na njaa kuliko anapokuwa ameshiba. Shibe huweza kuchochea uvivu wa kufikiri.

Kwa hiyo kama ni njaa ndiyo iliyompekekea awaze kununua ndege, ni Bora awe anafunga mara kwa mara hadi atakapoifikia ndoto yake.
Acheni akili za kimaskini ,hapo Kenya tu kuna wakulima wa kawaida wanamiliki chopper na cesna kwa ajili ya uangalizi wa mashamba yao na shughuli zao , used helicopters na cesna planes ni bei ndogo tu za kawaida
 
Wakulima walikuwa wanamiliki ndege?

Ndiyo zile, inasemekana, zilizotaifishwa na Serikali kipindi, nafikiri cha Nyerere?

Kumbe si kitu cha ajabu kivile kwa mtu binafsi kumiliki ndege Tanzania!
Kitu cha kawaida tu ,nashangaa watu wanavyobishana humu as if hizo ndege used na chopper ni kitu cha ajabu saana ,
 
Ndege ndogo Cessna grand caravan used....ni bei nafuu kuliko.... unavyofikiri...
Ni nafuu kuliko Toyota coaster used.
TRUST ME
Uongo Cessna 208 haiwezi zidiwa bei na Coaster

Bali C152/172 tena za mwaka 1970 ndo zinazidiwa ila ukiifanyia repair na cockpit ukabadilisha inavuka mfano garmin tu ni zaidi ya dollar 15,000
Hapo ukiweka AC inaongezeka bei
 
😅😅😅Ukienda NIT na pale DMI kuna wazanzibar kibao kwa hyo hayo majina ni mengi.

Yaani hao jamaa kozi zao ni hizo atakuwa mzenji tu.
Waapii na wakati wachaga ndo wamedominate kwenye aviation😆😆😆🙌🏿👆🏿👌🏿
 
Kumiliki ndege ni gharama sana kwa hapa bongo.... bora uwe unatumia tu hizi private zipo nyingi tu mfano Dar Mwanza 6 people $13k one way na hiyo ni xmass season 2 hrs flight.
Inawezekana mleta mada anataka kuepuka usumbufu kukodi ndege n.k.

Inaelekea ana shughuli au anatarajia kuwa na shughuli zitakazomfanya awe anatumia ndege kila siku Asubuhi na Jioni. Akiwa na yake itampa uhuru wa kupangilia ratiba yake kulingana na uhitaji wa siku husika.

Na pengine, inaweza ikamsaidia kupunguza na gharama zingine, ila sina uhakika.
 
Acheni akili za kimaskini ,hapo Kenya tu kuna wakulima wa kawaida wanamiliki chopper na cesna kwa ajili ya uangalizi wa mashamba yao na shughuli zao , used helicopters na cesna planes ni bei ndogo tu za kawaida
Nawafamu Watanzania wawili waliokuwa wakimiliki ndege, japo wote kwa sasa ni marehemu.

Advocate MAWALLA, alikuwa akiishi Arusha, na mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Bob Sambeke, nafikiri alikuwa mfanyabiashara. Naye alikuwa na makazi yake Arusha.

Bob Sambeke alikufa Arusha kwa ajali ya ndege aliyokuwa akiirusha.

Naamini kuna na Watanzania wengine wanaomiliki ndege. Hawafahamiki tu kwa vile, pengine, si watu maarufu kwenye vyombo vya habari.

Kipindi fulani nilisikia Askofu Gwajima naye alinunua chopa.
 
Yeap kama Kuna helipad na ina meet vigezo vya mamlaka za viwanja vya ndege Tanzania.
Acha na mimi nidream big! Kwani itanigharimu nini kuwa na ndoto ya kwenda kutalii kwenye mweizi hata kama sijawahi kufikia Kenya? (Ni mfano tu lakini)

Siyo dhambi na mimi nikiwa na ndoto ya kupaki chopa kwangu, hata kama nitakuwa nikitumia mara mbili kwa wiki.

Sijawahi kupanda chopa lakini naamini ni usafiri mzuri.
 
Kitu cha kawaida tu ,nashangaa watu wanavyobishana humu as if hizo ndege used na chopper ni kitu cha ajabu saana ,
Nafikiri pia kuna baadhi ya watu wana mtazamo hasi linapokuja suala la Mtanzania kumiliki vitu vinavyoaminiwa ni vya gharama! Kwani ndege ziliundwa kwa ajili ya Wazungu na Waarabu peke yao?

Isije ikawa uke mtazamo wa "Watanzania hawawezi" umewaathiri.

Kumiliki ndege si muujiza.
 
Back
Top Bottom