Utaratibu wa kuteua wanajeshi kushika nyadhifa za kiraia haufai

Utaratibu wa kuteua wanajeshi kushika nyadhifa za kiraia haufai

Hao wakuu wa mikoa ndio wako kwenye katiba hii tunayoilalamikia lakini hawa wakuu wa wilaya wenyewe hawamo kwenye katiba ila wamo kwenye sheria zilizotungwa na bunge (Parliamentary Act).
Kuna DC, DAS, DED, Mbunge na Mwenyekiti wa halmashauri, wote hawa wanafanya nini?
 
Nazidi kusikitika kuona utawala na mamlaka ya raia yanapokonywa. Wanasiasa kama unaona huna uwezo wa kuwaongoza hao militant bila kuwaingiza kwenye siasa basi waondoe kwanza jeshini wabaki civilian then ndiyo uwateue.

Kitendo cha karibia mkoa mzima wa Kigoma kuwapelekea wanajeshi kuwaongoza pia haijapendeza hata kidogo.

Civilian leader ana nguvu na maono zaidi ya military. Acheni kufanya mambo kwa utashi, fuateni katiba.

Jeshi lazima liongozwe na raia na si jeshi kuongoza raia. (Civilians must rule the military and not otherwise)
Vipi una rabies? Nani alikuambia kuwa maafisa wa jeshi hawana maono? Tena utashangaa kuwa nature ya kazi yaoa huwafanya wawe na maono zaidi ya raia wa kawaida. Hebu taja afisa wa jeshi yeyote yule aliyepiewa kazi ya kiraia akaishindwa, na katika miaka sitini ya uhuru wetu tumekuwa nao wengi sana including Luteni Kanali Kikwete na Kapteni Mkuchika.
 
Unaelewa nini maana ya utawala wa kiraia?
Tatizo huwa mnasoma na kuwa rigid kwenye mlichosoma au kuaminishwa. Wakati waliotuletea hizi taratibu wao kuna mazingira inabidi wawe flexible.

Nenda USA, UK, ISRAEL, Russia, FRANCE nk. Nimekutajia hizi za Western kwakuwa ndiko tulikokopi kila kitu.
 
Nadhani sio vibaya kuwa na wanajeshi sababu ni kazi tu unajua hata Hawa MaDC wengine ni watumishi wa umma so unakuta akitenguliwa anaweza kurudi ofisini kwake kama kawaida sema sababu wengi wanakuwa wanaona kurudi cheo cha chini kama atadharauliwa.

Mfano, Angela Kairuki wakati anateuliwa kuwa Waziri alikuwa ni State Attorney pale AG Chambers. So akitaka arudi kuwa state attorney apangiwe mafaili ya mahakamani. Pia kuna aliyekuwa DC wa Tabora Erick Kitwala nae ni mwanasheria ofisi ya wizara ya ardhi.

So hata mwanajeshi anateuliwa kulingana na mahitaji ya anakopelekwa, Ila uteuzi ukiisha anarudi kikosini kama kawaida, hii ipo sana kwa watu wa TISS unakuta akiteuliwa anarudi zake kwenye ofisi yake anapangiwa kazi kama kawaida.

Sioni tatizo especially uteuzi huu pamoja ni mbovu Ila umezingatia sana maeneo yenye uhalifu wamepelekwa wanajeshi nadhani sababu Wana mbinu zaidi za kijeshi kupambana na majambazi kule maporini, ukimpeleka bishop akawe DC Kasulu ntakuta wamemmvua suruali.

Kama ni hivyo hata Rais basi awe mwanajeshi..
Watu wanatetea logic ya kijinga sana.
Kweli mkuu. Na mawaziri wote.
 
Nazidi kusikitika kuona utawala na mamlaka ya raia yanapokonywa. Wanasiasa kama unaona huna uwezo wa kuwaongoza hao militant bila kuwaingiza kwenye siasa basi waondoe kwanza jeshini wabaki civilian then ndiyo uwateue.

Kitendo cha karibia mkoa mzima wa Kigoma kuwapelekea wanajeshi kuwaongoza pia haijapendeza hata kidogo.

Civilian leader ana nguvu na maono zaidi ya military. Acheni kufanya mambo kwa utashi, fuateni katiba.

Jeshi lazima liongozwe na raia na si jeshi kuongoza raia. (Civilians must rule the military and not otherwise)
Hatujui tunatoka wapi na tunaenda wapi.

Kina Kikwete, Nnauye Senior, Mkuchika, Kinana, Makamba Senior etc walitoka jeshini ili waendelee na nyadhifa za kisiasa.

Siku hizi tumerudi kule kule kuwapa wanajeshi nyadhifa za kisiasa.
 
Nafikiri ni strategic move. Mkoa uko mpalani.. a lot of security issues. So lazima waweke watu ambao ni security focused guys
Nope, Hakuna Kitu kama hicho, huo ni ushamba na ulimbukeni tuu!!!!

Kwani tunaishi kwenye zama za akina Napoleon Hill au Alexander the Great ambapo kutwa nzima watawala walikuwa wakiendesha campaign za kuongeza maeneo??

Sasa hivi ulimwengu ni kistaarabu watu wanaheshimu mipaka ya nchi. Acha wanajeshi waendelee na shughuli zao za kijeshi na utawala kiraia acha utamalaki maeneo ambayo yanastahili kuongozwa na raia.

Asante!!
 
Hatujui tunatoka wapi na tunaenda wapi.

Kina Kikwete, Nnauye Senior, Mkuchika, Kinana, Makamba Senior etc walitoka jeshini ili waendelee na nyadhifa za kisiasa.

Siku hizi tumerudi kule kule kuwapa wanajeshi nyadhifa za kisiasa.
hao uliowataja walitoka jeshini ili kufanya kazi za kisiasia, siyo kazi za kiserikalii kama mkuu wa mkoa, waziri, mkuu wa wilia katibu mkuu wa wizara, balozi na nyadhifa kama hizo za kiserikali.

Colin Powell akiwa mwanajeshi alikuwa mshauri mkuu wa mambo ya usalama kwenye serikali ya rais reagan, baada ya utumishi huo akarudi jeshini na kuendelea hadi kuwa mkuu wa majeshi ya marekani.
 
Mkoa kama Kigoma na mingine ya mipakani inaingilika kirahisi na wageni. Wapo wenye nia njema na wapo wageni wenye usumbufu.

Sisi wa Kagera tunayafahamu sana matatizo tuliyoletewa na majirani kutoka Burundi, wanapopewa nafasi wanajeshi maana yake ni watu wakakamavu wenye utayari wa kuimarisha ulinzi.

Mfano wa faida za wanajeshi ni kule Mtwara, tukumbuke kuwa wale waliofanya mauaji ya Kibiti na Mkuranga wamekimbilia Msumbiji na muda wowote wanaweza kutaka kuanzisha vurugu hivyo makamanda wanaziweza hizo pilika za maisha yenye hali tete.
 
Ungeuliza sababu ya hao wanajeshi kuteuliwa sio unalaumu tu bila kujua wanateuliwa kwa usalama wako wewe mlalamikaji huko mipakani.

Mipakani ujambazi ni mwingi, vurugu zipo nyingi, magendo ni mengi pia hao wanajeshi huwa wanafanya kazi kubwa kuliko hawa wemgine waliopewa kazi za mikoa ya mjini huko....
Tatizo letu watanzania ni kutofahamu gharama ya amani tuliyonayo. Mtu akijiona anaweza kulala na kuamka salama na mwisho wa wiki akakaa bar akanywa na marafiki zake anadhani hali ile imejiotea tu kama uyoga.

Unapolala kwa amani na kukoroma kitandani mwako tambua kuna watu hawalali usiku kucha wanazunguka mpakani wakiwa na bunduki begani.
 
..basi wangeteuliwa kwenye nafasi ambazo hawatashiriki siasa za CCM.

..CCM ina utaratibu kwamba mkuu wa wilaya ni mjumbe wa vikao vya kamati ya siasa ya wilaya ya CCM.

..Tunaunga mkono kuimarishwa kwa usalama maeneo ya mipakani lakini tunakwazwa na utaratibu wa CCM kuwatumia askari wetu ktk masuala ya chama chao.
 
Kulala na kukoloma si kwa sababu ya kuwa na jeshi imara Bali ni matokeo ya siasa safi. Angalia nchi kama Israel na Palestine wanamajeshi imara lakin bado hawalali kwa aman.
 
Kumbe shida yako ni CCM. Vumilia tu mkuu, ndio siasa za Tanzania zilivyo. Tunaweza mimi na wewe kutangulia mbele ya haki huku CCM ikiendelea kuwepo madarakani.
 
Kulala na kukoloma si kwa sababu ya kuwa na jeshi imara Bali ni matokeo ya siasa safi. Angalia nchi kama Israel na Palestine wanamajeshi imara lakin bado hawalali kwa aman.
Adui wa nje yupo mkuu. Usipuuzie hata siku moja umuhimu wa jeshi la wananchi.
 
Kumbe shida yako ni CCM. Vumilia tu mkuu, ndio siasa za Tanzania zilivyo. Tunaweza mimi na wewe kutangulia mbele ya haki huku CCM ikiendelea kuwepo madarakani.

..Naunga mkono kuwa tuwe na uvumilivu.

..lakini pia tusiache kusema UKWELI tunapoona mapungufu.

..hili la wanajeshi ambao ni ma-RC na ma-DC kushiriki ktk siasa za CCM siyo sahihi.
 
..Naunga mkono kuwa tuwe na uvumilivu.

..lakini pia tusiache kusema UKWELI tunapoona mapungufu.

..hili la wanajeshi ambao ni ma-RC na ma-DC kushiriki ktk siasa za CCM siyo sahihi.
Linaweza lisiwe sahihi lakini kimkakati lipo sahihi. Hii afrika yetu inazo serikali nyingi zenye kufuga maasi ya ndani kwa ndani. Mfano ni kule DRC, Burundi na hata Msumbiji.

Na hayo maasi huwa yanakuwepo maeneo ya mipaka yetu. Msumbiji haina usalama tangu magaidi waanze kufanya vurugu zao.

Mfano mwingine ni Kenya ilivyosumbuliwa na wasomali wanaovuka mipaka na kwenda kuuwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za boarding. Hatuwezi kuona faida za JWTZ kuwa ndani ya serikali lakini zipo nyingi.
 
Nope, Hakuna Kitu kama hicho, huo ni ushamba na ulimbukeni tuu!!!!

Kwani tunaishi kwenye zama za akina Napoleon Hill au Alexander the Great ambapo kutwa nzima watawala walikuwa wakiendesha campaign za kuongeza maeneo??

Sasa hivi ulimwengu ni kistaarabu watu wanaheshimu mipaka ya nchi. Acha wanajeshi waendelee na shughuli zao za kijeshi na utawala kiraia acha utamalaki maeneo ambayo yanastahili kuongozwa na raia.

Asante!!
Nope thats the way it is. especialy kama umepaka na nchi ambazo zimekuwa kwenye mapigano for a long time. Jirani hauko safe..

but then again uko right sehem moja tu.
ila kwangu mm hayo maeneo hata kama kiongoz ni raia awe na experience.. au awareness na masuala ya usalama mipakani.
 
Back
Top Bottom