Linaweza lisiwe sahihi lakini kimkakati lipo sahihi. Hii afrika yetu inazo serikali nyingi zenye kufuga maasi ya ndani kwa ndani. Mfano ni kule DRC, Burundi na hata Msumbiji.
Na hayo maasi huwa yanakuwepo maeneo ya mipaka yetu. Msumbiji haina usalama tangu magaidi waanze kufanya vurugu zao.
Mfano mwingine ni Kenya ilivyosumbuliwa na wasomali wanaovuka mipaka na kwenda kuuwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za boarding. Hatuwezi kuona faida za JWTZ kuwa ndani ya serikali lakini zipo nyingi.
..chanzo cha uasi ni walio na mamlaka kutokutenda haki, na kuongoza bila kuzingatia sheria na utawala bora.
..Tz tumejiwekea sheria inayoelekeza kwamba wanajeshi au askari kwa ujumla hawatashiriki siasa.
..mimi nadhani tujielekeze ktk kuweka mazingira ya HAKI hapa nchini ili tujihakikishie usalama na masikilizano wakati wote.