Utaratibu wa mabasi ya Abood kuingia gereji Morogoro una faida gani?

Utaratibu wa mabasi ya Abood kuingia gereji Morogoro una faida gani?

Hiyo tiketi ulikata mwenyewe au ulikatiwa

Kiukweli ukiacha Abood ya dar moro nyingine zote mavi niliwahi kupanda Abood mwanza to Morogoro kufika Dumila gari ikaisha mafuta ikabidi wapige simu Morogoro mafuta yaletwe

Lenyewe namba iyo iyo A.. hivyo kabisa
 
Kuna habari niliwahi kusikia kuwa huwa wanaingia then gari linafagiliwa na hilo vumbi linakuwa na kazi maalumu. Ndio maana abiria hawasikiu wala kuambiwa kuhusu Abood. Ni tetesi tu lakini.
 
Kina Abood ni watu wa matukio sana wale, kila basi lifikalo pale lazima liwekwe jini kwa ajili ya ulinzi njiani na kuna yanayopangwa rasmi ili yapinduke na kuua kisha wapate mengine mapya. Wenye mabasi si watu wa kawaida.
Jini gani hilo na mimi nalitaka
 
Kuna Mada humu humu JF uhusu Abood, itafute uunganishe Matukio. Wanabodi walisema Gari za Abbod zinaingia Yard ili akusanye michanga iliyopo kwenye gari kwa mambo yake ya Ndumba. Siku nyingine tafiti, Gari ikitoka yard imekuwa safi gafla tambua kwamba umeshabebwa Unyayo wako mkuu utabaki kutengenezwa uendelee kuwa Msukule wa Abood milele ndio maaana magari ni mabovuuuuu lkn umeona kuna Misukule yake humu inaiimbia mapambio. Gari AWY mkweche wa mwaka 2002 lkn ukiunanga kuna waliobebwa Nyayo na kutengenezwa wakatengenezeka wanatoka mishipaaaa kutetea hizo Screpa.
Niliwahi kupanda Al saedy dar to Morogoro abiria wapo ndani ya gari na tiketi wakaiona Abood wakaanza kulia washuke wapande Abood [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1487][emoji1487] uchawi upo
 
Hapo kwenye mabasi yote pawekwe kwa usahihi...gari za Abood zinazoishia morogoro kutoka Arusha na Dar zinaingia msamvu kwanza halafu ofisi yake ya mjini ( nadhani kushusha vifurushi ) ndio huendelea huko karakana, itakuwa bus za mbeya / tunduma na mwanza ndio huenda na abiria huko karakana.
 
Hapo kuna Mambo mawili wanajaza mafuta au wanakabidhi documents
 
Niliwahi kupanda Al saedy dar to Morogoro abiria wapo ndani ya gari na tiketi wakaiona Abood wakaanza kulia washuke wapande Abood [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1487][emoji1487] uchawi upo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] jinga sana wewe
 
Mkuu ni kitendo Cha dakika 5 tu tunaomba uendelee kuwa mteja wetu
 
Mabasi ya kampuni ya Abood yanayotokea popote, yakifika Morogoro, lazima yapitie kwenye yard yao. Abiria wote mnashushwa nje ya geti. Basi linaingia ndani, sijui linaenda kufanyiwa nini? Halafu baada ya dakika kadhaa linatoka. Abiria mnapanda tena kuendelea na safari.

Hapo nje hakuna sehemu rasmi ya kusubiria. Mnatelekezwa juani, eneo la wazi, mnalowana vumbi. Sijui kama suala hili lipo kisheria? Serikali ya mkoa, waziri wa usafirishaji na uchukuzi. Waziri wa mambo ya ndani, waziri mkuu na hata rais wetu, sijui kama wanalifahamu hili?

Mimi kwa upande sikupendezwa na kilichotokea leo tarehe 23-10-2021. Kwangu ni mara ya kwanza, lakini nilivyosikia toka kwa abiria wenzangu tuliyotokea Mbeya, kwa basi la Abood lenye namba T830AWY, kwamba huu ndiyo utaratibu wao. Lazima mabasi yao yote yapitie ofisini kwao. Abiria wote tulishushwa, gari likaingia ndani ya ofisi zao, halaf likatoka tukaendelea na safari ya Dar. Sidhani kama na mabasi mengine yanafanya hivi? Ingawa juzi nilipanda basi la majinja sijaona mambo hayo
Wewe nawe ni wale wale tu! Yaani njia ya Mbeya Dar imejaa mabasi mazuri na ya uhakika! Akina Sauli, New Force na wababe wengineo wengi! Wewe unaenda kupanda basi la miaka ya 70, Abood!! Tena lina namba za usajili T 830 AWY!!

Siku nyingine panda basi zuri bhana! Hilo Li Abood waachie Waluguru na waluga luga wengine. Binafsi hata bure sipandi. Labda zile Yutong zake za kutoka Moro Dar! Ila siyo hayo Marcopolo ya kizamani..
 
Mabasi ya kampuni ya Abood yanayotokea popote, yakifika Morogoro, lazima yapitie kwenye yard yao. Abiria wote mnashushwa nje ya geti. Basi linaingia ndani, sijui linaenda kufanyiwa nini? Halafu baada ya dakika kadhaa linatoka. Abiria mnapanda tena kuendelea na safari.

Hapo nje hakuna sehemu rasmi ya kusubiria. Mnatelekezwa juani, eneo la wazi, mnalowana vumbi. Sijui kama suala hili lipo kisheria? Serikali ya mkoa, waziri wa usafirishaji na uchukuzi. Waziri wa mambo ya ndani, waziri mkuu na hata rais wetu, sijui kama wanalifahamu hili?

Mimi kwa upande sikupendezwa na kilichotokea leo tarehe 23-10-2021. Kwangu ni mara ya kwanza, lakini nilivyosikia toka kwa abiria wenzangu tuliyotokea Mbeya, kwa basi la Abood lenye namba T830AWY, kwamba huu ndiyo utaratibu wao. Lazima mabasi yao yote yapitie ofisini kwao. Abiria wote tulishushwa, gari likaingia ndani ya ofisi zao, halaf likatoka tukaendelea na safari ya Dar. Sidhani kama na mabasi mengine yanafanya hivi? Ingawa juzi nilipanda basi la Majinja sijaona mambo hayo
Labda pia wanasambaza dawa za kulevya kutoka mikoani nk
 
Back
Top Bottom