Utaratibu wa urejeshwaji wa Watanzania 301 kutoka Marekani

Wapiga kura wa CCM hao...... tena imekuwa vyema wamerudishwa mwaka wa uchafuzi......watapokelewa na zile Yutong za chama.....kila mmoja akipewa t-shirt imeandikwa MAMA SAMIA TUPOKEE......

Watakodishiwa hotel kwa mapumziko alafu ndio watapelekwa makwao wakiwa na kadi za chama, na fungu la kuanzia maisha

SAAMIA TUVUSHE
 
Huna lolote, nia yako ni kutaka kuwajua ili nafsi yako ya 'kimasikini' iridhike.

Deportation ni utaratibu wa miongo kwa miongo, watafuata taratibu wanazofuata kila wakati.
 
Kwani Trump kasema anawarudisha wageni wote, akiwemo mke wake?
Nilichosema kwa Wasafiri lolote linaweza kutokea sio ishu ya Trump..sisi wengine tuna hadi Uraia wa hizi Nchi tunazokaa ila wakiamua muda wowote wanakufuta na home narudi...
 
Wale ni wazamiaji!! Unataka tuwachukulie kama mashujaa? Acha ujinga
 
Nilichosema kwa Wasafiri lolote linaweza kutokea sio ishu ya Trump..sisi wengine tuna hadi Uraia wa hizi Nchi tunazokaa ila wakiamua muda wowote wanakufuta na home narudi...
Hakuna mtu anayerudishwa bila kuwepo na sababu ya/ za msingi.

Trump hawezi kusema anakurudisha ulikotoka kisa nywele zako za kwenye pua ni ndefu na chafu.

Marekani siyo banana republic [ingawa Democrats walitaka kuifanya iwe].

Kama status yako ya kuwepo Marekani imenyooka, hakuna atayekugusa.

Na hata ikitokea umekamatwa na ICE, utapewa due process.
 
Kwenda kunipokea wapi?

Btw, nafurahi kuwepo kichwani mwako.

Binafsi huwa najichukulia poa ila kumbe kuna watu mpo ambao hadi usingizini mnaniota ilhali mimi wala sina muda mchafu wa kuwawaza…
Usiichukulie serious wengine ni watani na marafiki zako SI unajua wewe ni mkongwe na maarufu humu jukWani?
 
Haya mambo ni Tanzania tu husikii kenya wala Nigeria wala Ghana ambapo ndio wengi wapo huko kinyume na taratibu kabisa..
Bongo wachawi sana ni watu tupo na unafki wa kiwango cha lami.
 
Home is where your heart is. Tutawakaribisha watakaorudishwa. Watakaongia mitini tunawatakia kheri. Ila wakumbuke wanakwao.
All and all we wish all them the best in life.
 
Mimi mara ya mwisho kufika Dar-Es-Salam kutokea mipaka ya Zimbabwe tu kama 10 years ago.

Kasheshe ilikuwa kwenda kuweka mafuta tu, nakumbuka ilikuwa kituo cha Mwanamboka (manyanya).

Yaani nipo na RAV4 kwa wazungu (mkweche) kibongo-bongo deal. Mafuta Dar ilikuwa unawekea na wahudumu, wewe unaenda lipa counter.

Sasa nimeshuka kwenda kulipa yule dogo aliekuwa ananiwekea mafuta alivyoninunia simjui, hanijui; tena najichekesha kwa ucheshi anione wa kawaida.

Sijui wageni wenyewe wanakuwa wanawajua maana hata sielewi, lakini unakuta mtu kakunia balaa (sio wote, ni asilimia ndogo sana, if I am honest). Wengi ni poa.

Baada ya hapo nikasema mimi kwenda Tanzania ni kuangalia makaburi ya wazazi tu,

Yaani watanzania wana wivu na majungu hatari, hao watanzania ambao wapo kwenye misuko suko huko US ukute 90% hawana hata ushiriki wa JF wanachangamoto zingine kabisa za maisha.

Sasa wewe unashangilia iweje, kukosa kwake kunakuongezea nini au kufaidika kwake kunakupunguzia nini.

Binafsi ile experience yangu ya kituo cha mafuta ya mwanamboka nikasema sirudi tena Tanzania, zaidi ya kwenda kutambika kwenye makaburi,

Mnadhani rahisi huko walipo watu, unakuta mtu huko anavita yake ngumu, na wewe unampelekea matatizo yako. Asipokujibu unaona dharau wakati hujui changamoto zake.

Hizo nchi sio rahisi kama mnavyodhani, inategemea umetua na mguu gani (vinginevyo cha moto utakiona).

Halafu huko kuna wanga wanakuwangia hawajui changamoto zako. Yaani kuna baadhi ya watanzania wana roho za kimaskini balaa hasa wanaosherekea kuona wenzao wanarudishwa Tanzania kutoka USA na ulaya.
 
Jana orodha imeongezeka kuna member alipost humu niliona kama ni 400+
 
Ushamba na umaskini vinawasumbua. Wakiona una mkweche wanajua umeukata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…