Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

Dah nimecheka utadhani mazuri, yaani mnakua hamlali. Mnachangishana Hadi kukopa kisa kuwalisha Watu wanaokuja kuwafariji! Si heri ukodi Watu wa kukufariji ujue Moja, msiba ukiisha unalipa invoice maisha yanaendelea
Hayo maisha yapo kwenye jamii hii tuliyopo?
 
Yego chimura siga omururu ouja ukwita abhanu nomweko
 
Kwa kweli ustaarabu wetu ni mgumu sana jamii zetu za kitanzania.

Mtu kafiwa bila shaka katumia gharama nyingi tu kuuguza pia bado ana kibarua kigumu tu katika kusitiri marehemu.

Kiubinadamu nzengo ilipaswa kuwa na jukumu la kufariji na kushiriki mazishi kwa mwenzao huyo. Msiba ni jambo gumu sana kwa mwanadamu hivyo nzengo inapaswa kuwajibika effectively kwa kila hali na mali.

Wananzengo tunapaswa kusitiri marehemu ikiwemo na kuficha aibu ya umasikini lakini leo hii utakuta wananzengo wanaohudhuria msibani wako 200 lakini mchango wanaotoa kwa mfiwa hauzidi hata 200k na hapo wapo msibani si chini ya siku tatu hadi mazishi aisee inasikitisha sana.

Lakini hili ni suala la mindset tu ndugu zangu tunapaswa kubadilika. Hizo changes huanzia kwako wewe na mimi tuhurumiane na kuchukuliana matatizo na madhaifu yetu hapo jamii inaweza kubadilika.
 
Bora wale halafu watulie basi, wengine wakishashiba wanaiba nyama, maandazi, wali wanapelekewa watoto home[emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekuelewa sana[emoji1666][emoji1666]
 
Utaratibu wa wafiwa kulisha waombolezaji ni wa kijima sana. Yaani mtu kafiwa tena aanze kuwaza masufuria na sahani ziko wapi kha!!
Ndo hapo sasa!

Inapaswa jamii ibadilike
 
Sisi wengine DINI yetu inakataza kabisa kitendo cha mtu ambaye si mfiwa kula msibani,usahihi ni kwamba wale wanao enda msibani ndiyo wanatakiwa kuwahudumia wafiwa.

Tangu nilipopata hii Elimu kwenye dini yangu sikuwahi tena kula msibani na sitokula tena,huwa wakati wa kula ukifika natoka kidogo.
 
Mkuu wewe hayajakufika bila shaka
Mantiki ya post yangu ilikuwa naijibu commemt #44 si vinginevyo!

Angalia alichoandika hiyo comment, ndiyo nilicholenga kujibu.

Kunifika yalishanifika sana, hata mwaka jana yalinifika pia.
 
Kwa waislamu swala la ndowa na mazishi dini yao imewapa maekekezo mazuri sana.

Hizi shida waachieni wakristo lakini kwa mwislamu kupata shida hizi ni kujitakia.

Dini ya kiislamu inaelekeza mtu akifa azikwe haraka.

Familia haiwezi kuumia kwa kuwapikia uji na sukari inatosha kabisa, mambo ya catering waachieni wakristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…