Mimi nachojua kule nimekulia na ndo utaratibu upo mpaka leo ni kuwa kuna vyama vya kusaidiana kwenye misiba. Na vina taratibu na sheria kali kwa wanaoenda kinyume. Na utokeapo msiba kwa mwanachama yafuatayo hufanyika kwa wafiwa:
1. Mfiwa anapotoa taarifa ya msiba kwa uongozi wa chama, uongozi huwajulisha wanachama. Jukumu la wanachama ni kutoa kuni,chakula kidogo kwa kiwango kilichokubaliwa na hela kidogo ya mboga. Mchango huu mdogo ni kwa ajili ya kuwapikia watakaochimba kaburi,watakaozika na wafiwa wote kiujumla na yeyote atakayejisikia kula. Chakula hiki huliwa kabla ya mazishi na hupikwa na wakina mama. Baada ya chakula ndipo mazishi hufanyika.
Note: vinywaji eg.pombe na maji huwa ni jukumu la wafiwa ingawa sio lazima Ila ni muhimu.
2. Baada ya mazishi uongozi wa chama huwajulisha wanachama tena kutoa mchango mkubwa kwa wafiwa kwa ajili ya ndugu,jamaa na marafiki watakao kuwa kwenye matanga na hiyo huenda hadi siku kati ya 4 -7. Mcango huo hujumuisha chakula,kuni na hela ya mboga.Ndani ya hizo siku chakula hupikwa na akina mama kwa kupeana zamu. Siku huanza kwa huduma ya chai na vitafunwa na badae hufuata chakula na hiyo ni asubuhi na jioni ndani ya hizo siku.
Note: Bado jukumu la vinywaji eg. maji na pombe huwa ni jukumu la wafiwa.