Utata alipo trafiki anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi

Utata alipo trafiki anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi

Matokeo yalitoka na alifaulu kwa daraja A
Hahaha nilidhani alipata daraja I kumbe A,
Wasimsumbue trafik, sheria haziruhusu kutoa mimba. Na sheria haziruhusu trafik kumuoa.

Wangemjengea confidence na financial akasome nje ya mipaka ya Tanzania, kwasababu ndani hawaruhusu wazazi kusoma.

Sasa traffic police wa nini wamuache apige kazi alee mwanaye.
 
Katoto ka la Saba mdude mkubwa hivyo unapitaje jamani
Huyo siyo mtoto,mtoto gani anamiliki simu janja na mama yake anachekelea,ningekuwa mimi RPC,ningedili na huyo mama kwa kumchuuza mwanae kwa bei ya simu Janja,na hako katrafiki ningekapandisha cheo na kukahamishia znz au Ta.
 
Hahaha nilidhani alipata daraja I kumbe A,
Wasimsumbue trafik, sheria haziruhusu kutoa mimba. Na sheria haziruhusu trafik kumuoa.

Wangemjengea confidence na financial akasome nje ya mipaka ya Tanzania, kwasababu ndani hawaruhusu wazazi kusoma.

Sasa traffic police wa nini wamuache apige kazi alee mwanaye.
Primary kuna daraja la kwanza mkuu?!
 
Mimi labda ni mshamba ,je mtoto wa darasa la saba kumpa simu ni maendeleo au ni ushamba. Maana sijaona mantiki. Kuna ndugu yangu mtoto wake alikua anakaa kwangu akiwa form one baba yake alimnunulia simu ,lakini usiku mpaka saa 8 anaongea na wanaume . Nikamwambia baba yake ,unamharibu mtoto anaongea na wanaume muda wote. Baba akawa haelewi ila nikaonekana mbaya. Nikawaachia ,kilichomkuta baba yake na mtoto ndio wanajua,walitaka kunihusisha nikawakatalia. Jamani angalieni na pyschological maturity ya mtoto kabla ya kumpa simu. hata kama hukai naye ,tafuta njia nyingine.Simu kama zinavunja ndoa za watu wazima ,je vitoto vya miaka 14 itakuaje
Kama umesoma vizuri hayo maelezo, simu alipewa na huyo traffic. Na alikuwa akiitumia kwa siri mpaka mamake alipogundua mtoto anamiliki simu! Ndo uchunguzi ulianzia hapo
 
'Anayetuhumiwa kumjaza mimba mtoto mwenye umri wa miaka 14 wa askari mwenzake.'

Ni tatizo la kifamilia hilo(Trafiki kwa Trafiki).,watamalizana wenyewe.

dodge
shamba la bwana Heri,mahindi ya bwana Heri,na mbuzi aliyekula mahindi ni wa bwana Heri. Hamna kesi
 
Tunapoelekea hapajulikani kwa kweli wababa tumekuwa na tamaa sana tunataka kutafuna kama mchwa!
 
Hahaha sasa trafiki wanamtafuta afanye nini?! Kesha jaza mimba na haitoki.

Mlisema tuzae tu, sasa tunawajibika polisi nao mko nyuma yetu.

Huyo hata asingepata mimba darasa la sabaange fail, hataangeenda secondary ya kata, form two ange fail, na hata kamawange mrushaform two,form four ange fail.

Sasa yanini kumsumbua trafik.
Kumsumbua??

Apigwe mvua 30 kama wengine!







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni maajabu sana kwa majibu yake hayo
Yaani mtoto mdogo kafanyiwa unyama huo na yeye anajibu namna hiyo
Haya ni maajabu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Moshi. Wingu limegubika mahali alipo askari wa kikosi cha Usalama Barabarani maarufu kama trafiki, anayetuhumiwa kumjaza mimba mtoto mwenye umri wa miaka 14 wa askari mwenzake.

Januari 9, Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Salum Hamduni aliliambia gazeti hili kuwa polisi huyo anashikiliwa na jeshi hilo, lakini taarifa za uhakika zimedokeza kuwa hajawahi kukamatwa.

Vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Kamanda huyo aliagiza polisi huyo akamatwe na kushitakiwa kwa kosa la kubaka mwanafunzi huyo wa darasa la saba, lakini maagizo yake inadaiwa hayakufanyiwa kazi.

Siku hiyo Kamanda Hamduni alisema tayari wamemkamata polisi huyo na wanaendelea kumshikilia kwa mahojiano na ikithibitika kuwa na mahusiano watamchukulia hatua za kiutawala kwanza.

“Ni kweli tunamshikilia kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma zake na tutachukua hatua za kiutawala kwanza na kama ushahidi wa jinai utajitosheleza tutampeleka mahakamani,” alisema Kamanda huyo.

Hata hivyo, taarifa mpya zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa polisi huyo hakuwahi kukamatwa na polisi wala kushikiliwa, badala yake alitokomea kusikojulikana na hajaonekana kituo cha kazi zaidi ya wiki sasa.

“Hajawahi kukamatwa kama mlivyoripoti. Msala ulivyosanuka alisepa kwa kama siku tano hivi, baadaye akarudi ile kwa machale machale alipoona issue (suala) imekaa vibaya akaondoka mazima,” ilidokezwa na mtoa habari.

Gazeti hili lilipomuuliza Kamanda Hamduni jana kuhusu taarifa hizo mpya alijibu kwa kifupi tu kuwa aliagiza akamatwe na kwamba kama alitoroka kabla hajakamatwa hafahamu akaomba muda afuatilie.

Baadaye saa 10:25 alasiri mwandishi wetu alimtafuta tena kujua kama amefuatilia suala hilo, alijibu kuwa alikuwa hajapata muda wa kufuatilia kwa kuwa alikuwa ametingwa na majukumu mengine.

Vyanzo mbalimbali vimedokeza kuwa baada ya kufanyiwa vipimo vya afya yake katika hospitalini ya Serikali mjini Moshi, mtoto huyo anayesoma darasa la saba, amekutwa na ujauzito wa miezi mitatu.

Habari zaidi zinadai mawasiliano ya simu baina ya polisi na mtoto huyo, yanathibitisha kuwapo kwa mahusiano ya kimapenzi kutokana na aina ya jumbe zilizokutwa katika simu ya mtoto. “Simu ya mtoto ilikutwa na messages (jumbe) za mapenzi kutoka kwa huyo polisi na mtoto alipobanwa alisema hata hiyo smartphone (simu janja) alipewa na huyo polisi,” kilidai chanzo hicho.

Mama wa mtoto huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za maadili, alisema tayari amewasilisha malalamiko kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa, Salum Hamduni juu ya suala hilo.

Chanzo: Mwananchi
picha yake iko wapi sasa..??

Huyu bwege anachukua rushwa kwenda kuto.. bea mtoto wa mwenzie.. [emoji3526][emoji37][emoji37]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una maw
Hahaha sasa trafiki wanamtafuta afanye nini?! Kesha jaza mimba na haitoki.

Mlisema tuzae tu, sasa tunawajibika polisi nao mko nyuma yetu.

Huyo hata asingepata mimba darasa la sabaange fail, hataangeenda secondary ya kata, form two ange fail, na hata kamawange mrushaform two,form four ange fail.

Sasa yanini kumsumbua trafik.
Una mawazo finyu kama kichwa cha mpanzi.Kwa sababu ni askari wafanye kazi ya kudanganya watoto? ama kweli wanalinda raia na mali zao.Halafu wanafichana.Nampongeza aliyesema tupate picha yake humu tumtafute wenyewe.Kashfa hiyo
 
hiyo simu walikuwa wanaitumia wote na mama yake.Mama yake akitaka kuongea na mchepuko wake anatumia simu ya mtoto.Walikuwa wanafichiana siri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom