Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mku mm hil swala lipo na kuna majadiliano mingi inaendelea kwenye international forums juu ya hii ishu. Naamini ukwl utajulikana. Ni mda tu.
Ila kuna kitu nyie wat hamkisemi.
Ukweli ni kwamba mzee alikuwa mbishi. Mkuu wa idara nyeti alimwambia mkulu kuws kipindi hiki tunasimamisha ugeni wowote na uzinduz wowote mpaka hali itulie. Tunaambiwa Mkuu alikataa na akasema ataendelea na kazi km kawa. Kikawaida inapokuja suala la ulinzi, idara inatakiwa kuwa na nguvu , lakin jamaa aliizid idara nguvu , kwa protocols wakamsainisha document kuwa km unataka hivo, sawa saini hapa na wageni waje na uzurure kw ufungiz
Tukaona ugeni wa china, tukaona ugeni wa ethiopia , uganda na tukaona akija Dar kuzurura.... maisha yake yalibadilika hapo , na hata maadui wake hawakupata shida kumsukuma mlevi. Ubishi na kujiamini sana ni mbay hasa mambo ya uongozi
Ile timu iliyokuwa chato, asilimia kubwa walifululiza ,na hapa ndio penye tatizo lilipoanzia.
Hao international investigators hadi wamalize hiyo kazi tayari kila mtu kasahau.
Mkulu alizidi ujuaji ubishi na kujiamini sna. Nafasi km yake alitakiwa kuwa msikivu hasa suala la ulinzi wke
Mataifa mengine , idara nyeti ndio kila kitu na rais anaheshimu maamuz ya idara,hii ilikuwa ni tofauti sana kwa mkulu.
Poleni
It makes sense. Nadhani kama nchi tunapaswa kufanya kitu. Serikali zetu ni za kipumbavu. Na hawa hawa kwa kwenda kinyume na maslahi yao, wamekuwa ni mpango mkakati katika kifo cha JPM.
Tatizo sio awamu wala nini,Tatizo kubwa hapa ni sera(Foreign Policy) yetu dhidi ya China,Tumekuwa tukiwaona Wachina kama marafiki zetu for decades kuanzia awamu ya kwanza,hii imefanya hata tupunguze umakini wetu katika kuwafanyia screening hawa watu wanapokuja hapa nchini.
Haiwezekani watu wajanja wajanja wawepo tu,kodi hawalipi ipasavyo,maana ofisi zao ni kwenye ma go-down.This isn't about awamu, its totally about our foreign policy with Chinese.
Ila tim magu mna tabu sana! Korona bado inaondoa watu huko kijijini kwetu wiki mbili nyuma nimeambiwa watu watatu wameondoka kwa siku moja na moja wapo ni mwalimu aliyenifundisha shule ya msingi nilishtuka sana ikabid niulizie nkaambiwa ni korona na kwamba hasa pale nyumban siyo kitu ya kuuliza!It was a mind game mzee. Power is never easy. It was a total frustrations. Mzee alikuwa anapigana vita ndani na nje. Na Vita vya ndani vilikuwa ni ndani ya ndani. PSU ndani ya PSU
Mpasuko ndani ya mpasuko. Na katika kumchanganya Mzee akili, maisha ya wengi yamegharimu.
Je Corona imeondoka na JPM ? Kuna mtu yoyote anasikia kifo cha mtu mkubwa sasa.
Rais, anasema leo i am not okay , in few minutes classified information zimesha leak , who was behind this game ? Rais anazungukwa na timu maalumu.... inajulikana .
BAADA ya maziko tu, CAG anaibuka out of the blue, JPM anaaonekana he was useless na muflisi tena timu ya watendaji wake ndio wana create hizo sparks. You know maisha sio marahisi.
Lakini classified information zina muda wake na zita expire and the truth will be revealed
Umenichekesha sana kutokana na uchambuzi wa jibu lako.Sema mwenyewe mwenye upumbavu wako kwanini nikusemee
Hao form four na darasa la saba unaowaponda sio wanaosaini mikataba mibovu, mikataba mibovu imesainiwa na wasomi wasio na maadili na kukosa uzalendo.1. Vyombo vya Habari viwe Uhuru ili watanzania ambao walikuwa kwenye kifungo cha miaka 5 dhidi ya uhuru wao wa kutoa maoni wawe uhuru kujadili miradi isiyokuwa na uwazi kwa Taifa la Tanzania.
2. Tumeshuhudia Kifo cha JPM ambacho kina utata mwingi na maswali mengi yasiyojibika. Baada ya kifo hiki hata zile speed za Corona this Corona that hatuzisikii tena, badala yake maisha yanaenda kama kawaida....kwa wenye kutafakari hii inatupa TAFSIRI kubwa sana. Lakini muda ndiyo HAKIMU wa Kweli.
View attachment 1750423
View attachment 1750424
3. Mradi wa Bagamoyo ambao unapigiwa debe kwa sasa ni miongoni mwa miradi ambayo ndani yake ulikuwa na vipengele ANGAMIZI kwa taifa la Tanzania. JPM aliusimamisha mradi huu pamoja na miradi mingi ya NSSF kwa kushirikiana na wataalam wake na miongoni mwa hao wataalam ni hawa wanaopigia debe mradi huu kwa sasa.
4. Sisi kama wananchi, Tulitarajia kuona maelezo ya awali kutoka kwa SPIKA kwanini mradi huu ulisimamishwa kama ulikuwa na TIJA katika taifa letu huku yeye akiwa ni sehemu ya serikali iliyosimamisha huo mradi.
5. Tulitarajia kuona DISCUSSION ya kwanza ya huu mradi ni wananchi kuuelewa na kuona je kuna ulazima wa huu mradi, faida na hasara zake juu ya Taifa Hilo. Ielezwe pia Why Bagamoyo ? Je ni sehemu pekee yenye mlango mpana kwa TZ ?
6. Ijadiliwe terms za Procuring entity dhidi ya Supplier, tuone je zinafaida kwa taifa letu au ni hasara za long term kama tunavoona hasara za mwendo kasi na majumba yaliyogeuka kuwa magofu ya NSSF Huko Kigamboni.
Tunamsikia spika anaanza kuwa na defensive speech kuwa HAKUNA ANAYETAKA KUUZA NCHI!
Are we stupid or what ?
Why did he jump into that conclusion wakati wananchi wanahitaji kuelewa kwanza[emoji845]this is very immature kwenye majadiliano ya HOJA hasa kwa maslaha ya Taifa.
There is something fishy nyuma ya hii ishu na kuna watu wanaanza kujisogeza kwenye position zao japo wapo kimya.
7. Tunajua mradi huu ulikuwa ni dili la awamu ya 4 na serikali ya China ambapo kwa sasa ameshaanza kujisogeza baada ya kifo cha JPM.
View attachment 1750421
Swali la msingi ni Procurement Proceedures gani zilitumika kumpendekeza huyu Mtu ? Je Procurement Act dhidi ya Public Private Partnership inasema nini ?
Tunapiga kelele na CAG report ya sasa, kuna Mtanzania aliyesoma CAG report ya 2013/2014. Pitieni huko kwanza ndio mje kusema tulikuwa tunaibiwa. Haya ya sasa ni muendelezo wa kipindi cha 13/14
Mradi huu ujadiliwe kwa mapama na uwazi tena na watu ambao ni brained sio hao wasanii na form 4 leavers waliojazana mjengoni. Hakuna sababu za kuharakisha kwa hii kasi inayokuja kwa sasa.
Huenda ikawa ni HASARA nyingine kwa taifa
——
Usiwe msahaulifu ,neno corona utalisikia tena endapo kamati imetoa mshindonyuma .kuhusu IPO au haippInafikirisha hivi sasa hta sisikii Tena kuwa Tanzania hutuzingatii corona, kwamba vifo vitaongezeka...kimya kabisa
Ila tim magu mna tabu sana! Korona bado inaondoa watu huko kijijini kwetu wiki mbili nyuma nimeambiwa watu watatu wameondoka kwa siku moja na moja wapo ni mwalimu aliyenifundisha shule ya msingi nilishtuka sana ikabid niulizie nkaambiwa ni korona na kwamba hasa pale nyumban siyo kitu ya kuuliza!
Pengine inaezekana kifo cha maguna mkono lakin sasa na yeye alikua mbishi sana! Alishindwa kujua namna ya kudeal na hizo nguvu za ndan na hakutaka ushauri! Alitakiwa angate na kupuliza sasa kaz yake ilikua kungata tu eenh binadam hatuend hivo
Tuujue kwanza mkataba mana hata ndugai haujui..
Sijasema kafa na corona ila nilitaka kuonyesha corona bado ipo siyo kwamba imeondoka baada ya magu kufa kama baadhi wanavyosema period!So huyu mtu kafa na Corona kwa kuwa wewe umesikia jamaa zako wakisema kilichomua ni Corona?
Seriously!! That is your evidence based .... Hearsay !
Well, nimekusoma. All the best !
Personal cijawah muamini ndugaiBasi na Ndugai anahusika kumuondoa
Ndugai aliwah sem "taarifa alizokuw anapewa JPM kuhs ule mradi hazikuw za kwel" damn!Ule mkataba wa ujenzi wa mradi wa bagamoyo si ulivunjwa na Mh JPM ?.
Na alitueleza sababu zilizokua za msingi juu ya alicho kifanya
Hawa wanaopigia debe wanaweza kutuambia kwamba, je alicho sema JPM ni Uongo na kama Ni Uongo Ukweli ni Upi
Wakati uo Ndugai hakuiona ata MOU na nina hakiK ata akipewa kama ina page 200 hawezi kuisoma ila Magu ninahakika aliiona MOU na ata ingekuwa na page 300 Magu alikuwa na uwezo wa kuisoma na asipoelewa akaita wanasheria wafafanue.Ndugai aliwah sem "taarifa alizokuw anapewa JPM kuhs ule mradi hazikuw za kwel" damn!
Ndugai cyo mtu wa kuaminika hata dk 1
MRADI WA BAGAMOYO UKO SAWA WALA HAKUNA ANAYEKATAA,, SHIDA NI MASAHARTI YALIYOMO KUTOKA KWA WAFADHILI NJISI YA KUUTEKELEZA.Ni kwanini wanataka tuwafidie hasara wakati hawataki kuturuhu kukagua mapato yao?Kwanini wnatakea kuruhusiwa kuuza ardhi watakayopewa wakati ardhi ni mali ya Tanzania?Kwanini serikali istangaze ili walionapesa waje na nmasharti tofautu tofauti ili tichangue mtu aliye bora? Kwanini haya wawekezaji hawataki kufuata ushauri walipewa na kamati ya kunegotiate? Angali videa ya Kakoo utube akielezea ukweli wa jambo hili.Sikwamba Magufuri alikataa lakini anataka baadhi ya Masharti yarehekebishwe.Mkuu
Nimekutana na andiko hili sehemu nimeona linaweza kusaidia kuujua vema mradi huu. Hebu soma hii ingawa ndefu itasaidia sana👇
Najua topic imepita, lakini ninajua kidogo kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na napenda kumuunga mkono Mhe Spika kwa hoja zifuatazo. Na naamini Serikali yetu itazichukulia kama ushauri wa Mbunge kwa Serikali, ambao ndio wajibu wetu wa msingi kama Wabunge.
Muhimu kujua background ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Kwanza, mradi huu ulibuniwa na Serikali yetu kama Bagamoyo Special Economic Zone mwaka 2004 chini ya Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Sekta Mpya ya Viwanda. Serikali ya Japan ndio ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa “Tanzania-Mini Tiger 2020” na ulikuwa chini ya Wizara ya Viwanda.
Mamlaka ya Bandari nayo ilibuni Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028) ambao ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022 ili iwe tayari kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo. Kwahiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba: (a) Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina; (b) mradi wa Bandari ya Bagamoyo sio ni mradi wa Bandari, bali ni mradi wa Ukanda wa Kiuchumi ambao unaendana na mji wa viwanda.
Mwaka 2009 Mamlaka ya Bandari, kupitia kampuni ya Hamburg Port Counsulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kuona una manufaa kutekelezwa. Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama Mradi wa Taifa wa Kielelezo.
Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza katika Mradi wa BSEZ na Bandari ya Bagamoyo. Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia Taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute” (“STEPI”) ilikamilisha Upembuzi Yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza “Bagamoyo High Technology Park” kwa kushirikiana na EPZA pamoja na COSTECH. Kwahiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo sio uwekezaji wa Wachina pekee, kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka pesa yao nyingi. Na Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.
Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (“FYDP II), Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ni Mradi wa Taifa wa Kielelezo. Mradi huo unatarajiwa kuwa utavutia uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 10; utakuwa na Viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya Utatu wa Serikali ya Tanzania, China Merchants na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia Mikataba ya Uwekezaji kabla ya kusimamishwa.
Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: (1) utatutwika madeni kama vile Kenya na Sri Lanka ambapo Wachina walilazimika kutaifisha Bandari; (2) tutaua bandari ya Dar es Salaam; (3) haturuhusiwi kuendeleza Bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu pale Bagamoyo kwa miaka 99.
Hoja hizi zote sio za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wana-struggle namna ya kuzijibu kwasababu zinatolewa na watu wakubwa, na hao wawekezaji, hasa wa Oman, ni mamlaka za Serikali na wasingependa malumbano na Serikali yetu.
Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa sio ya kweli: kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo tunachukua. Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.
Hoja ya pili kwamba tutaua bandari ya Dar haina mantiki, kwasababu hata kabla Wachina hawajafika ilikuwa ni ndoto na mipango ya Mamlaka ya Bandari kujenga Bandari ya Bagamoyo. Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028), wenyewe Mamlaka ya Bandari walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar sio bandari shindani.
Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchi mwetu. Full stop! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port). Meli hizi, ambazo zitakuwa zinaongezeka kadri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 30, 50 ijayo, Bandari ya Dar ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi kujenga Bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.
Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza Bandari yoyote kwa miaka 99 na tuwape wao bandari hiyo bila sisi kutia mguu pale sio ya kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa hayo madai. Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka hela yake mwenyewe kwenye mradi atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession. Je, ni mingi au ni michache?
Inategemea pesa iliyowekwa (US$10bn) na standard practice kwingine duniani. Reli ya kuunganisha UK na France, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari standard practice ni miaka 25-40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji. Cha msingi kwa timu ya negotiators wetu ni kupata financial models za wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani. Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya Bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizito bandarini.
Suala lingine la kutazama katika kufanya maamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwasasa ndio kinara wa biashara ya import and exports duniani. Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 inayokuja. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China na Afrika ya Kati na Kusini, zitafikia katika moja ya Bandari za Mwambao wa Mashariki ya Afrika, kama Mlango na Kituo Kikubwa cha kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu.
Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na Reli ya Kati na TAZARA, itakuwa haina mshindani Nje ya Tanzania katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.
Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu Kaskazini yetu wanapigana kufa na kupona mradi huu usitokee. Kwahiyo mtaona disinformation nyingi kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.
Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie ule mradi Kenya kule LAMU. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzen kuzungumza na China Merchant kuwashawishi waende kwao. China Merchat walikataa na ndio walikutana na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa. Na majuzi, tarehe 25 Machi 2021 wameandika barua tena China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao (barua nimeiona).
Mwisho, nitamalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, wazungu waliona potential ya location ya Dubai kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wakajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30.
Washauri wake wakamwambia tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu. Sheikh akawauliza “sisi tuna pesa ya kujenga?”, wakajibu hapana, akawauliza “tutaipata lini”, wakasema hatujui, akawauliza “Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?”, wakajibu ndio, akawauliza “baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?”, wakajibu hapana, akasema “tuwape”. Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972.
Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya makampuni makubwa duniani. Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari, wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya logistics.
Mpendwa wetu hayati Rais Magufuli alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa kwenye mradi wa Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya negotiators itakuwa makini kuzingatia maslahi ya nchi.
Lakini mbona Hayati Rais Magufuli alishasema kwamba mtu anaeweza kukubali masharti ya huo mradi ni mlevi aliyechanganyikiwa? Sasa wanamchukulia vipi hiyu Rais wetu wa sasa?
Bagamoyo siyo msaada, ni unyonyajiTunahaki ya kuwashukuru Wachina kwa kutusaidia ila Bagamoyo bila Win win haitawezekana
Uko wapi nikuletee zawadi ya Eid❓Niliona BBC wanaripoti eti mwandamizi ktk serikali ya Jk alisema eti miaka 33 bila Tra kuchukua chochote bagamoyo ni sawa tu. Nikajiuliza mradi mkubwa mara 20 ya bandari ya dar unakubali kuuacha miaka 33 hivi hiyo ni akili ya wapi? Kwa maana hii dar tu ilivyo nchi kibao zinaitamani sasa zinatokea kama dar 20 alafu unaona poa tu, mie naamini kabisa kama JPM angekuwepo angeamua miaka 5 tu ajenge bandari ya b.moyo wala asingeshindwa katu sema kwa wavivu wa kufikiri wanadhani eti wazungu tu ndo wanaweza kufanya vitu kama hivi.
Poor leaders+poor leadership of the day!