Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

Utata kifo cha Afisa Usalama Kijitonyama

This is too sad, Poleni wafiwa M/Mungu awatie nguvu na awape subra katika kipindi hiki kigumu!

Ukweli una kawaida ya kudhihiri hata ukichelewa!
 
hii ndio tanzania tuliyo nayo kwa sasa cjui tnaelekea wapi!!!!
:A S-fire1:😛izza:
 
Kuna mijitu humu inajifanya mijuaji sana .angalia coment za lizaboni huyu jamaa yeye anajifanya kama vile yuko uwt kumbe ni shabiki wa maccm.
 
Huyo atakuwa walimpeleka quater guard au torture chamber ..kutakuwa kuna kosa alifanya ....la kiutendaji....huenda hawakuwa na nia afe ..labda gwaride likawa gumu!!
Nashangaa kwa nini wakakubali kuonesha amefia kisimani ...inaonekana sikuhizi TISS hakuna smooth operators ......la sivyo angetakiwa tu akutwe Mortuary...na msg tu kuwa aliokotwa barabarani ....
Taarifa kama hizi kwa kipindi hiki sio nzuri zinaleta tension bure bungeni ..... unless alikuwa anauza siri na wametaka kutuma message kwa waliokuwa wakimtuma na wengine wenye tabia kama zake

Watakuwa wamefanya kosa kubwa kama kweli nia ilikuwa hiyo.Maana mhusika atakuwa amekwisha pata mwanga na nafasi yakujipanga.

Na mbaya zaidi ukute Siri zenyewe za kuuza Meno ya Tembo au Unga au pesa za Uswisi na mambo mengine ya 2015.
Tutaona mengi in road to 2015
 
Kujifanya kichaa na kuendelea kufanya kazi UWT ni sehemu ya kazi ili mradi kichaa hakikukuanza ukiwa kazini eneo lingine!!! Vifo vya kutatanisha ni sehemu ya UWT kwa kuwa ulikula kiapo cha kutumikia kwa uadilifu bila kuvujisha siri hata kwa paka. Na makosa yake hayana mahakama so hakuna kifungo, ni kimoja tu!!!!! Rest in Peace Msalama.
N.B Msitegemee taarifa public kuhusu hiki kifo, hakuna kitu kama hicho. Taarifa yake ya kifo ni siri pia ya UWT kwa hiyo not piblic even to family members. Taratibu za UWT kikazi ni tofauti na taratibu zozote kwa mtumishi wa serikali japo siku hizi kuna some reforms katika UWT.
 
dah huu ni ukatili uliopitiliza sasa naamin kwel usalama watu hatari hapa hakuitaj upelelezi usalama wamemtoa usalama mwenzao maskani baba yetu, hawa watu ni washenzi sasa watamcngzia nan? Maana jengo wanaingia wao tu, hao watasema alidondoka akiwa anaumwa hawa ni washenzi jaman piga mawe hao
 
[h=2]Maswali yagubika kifo cha Ofisa wa Usalama wa Taifa[/h]01/06/2013
0 Comments


Utata umeibuka kuhusiana na kifo cha Ofisa Usalama wa Taifa, Peter Tyenyi, ambaye mwili wake umekutwa ndani ya kisima cha maji kilichopo eneo la ofisi za idara zilizopo Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu, msemaji wa familia ambaye ni kaka wa marehemu, John Tyenyi alisema mwili wa Peter (53) ulikutwa juzi ukiwa ndani ya kisima cha maji kilicho ndani ya eneo la Ofisi za Usalama wa Taifa, Kijitonyama baada ya kutoweka tangu Jumatatu ya Mei 27, alipoaga kwenda kazini.

“Peter alitoweka tangu Jumatatu alipoaga kwenda kazini. Mimi nimepigiwa simu jana saa tano asubuhi nikiwa Mombasa nchini Kenya kwamba amepatikana akiwa ndani ya shimo la maji,” alisema John.

Baadhi ya ndugu zake waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina wakiwa msibani Kigamboni jijini Dar es


Salaam, walisema kuwa baada ya ndugu yao kutoweka mkewe Joyce Mwakilama aliwataarifu na kuwasiliana na ofisi yake, lakini aliambiwa kuwa hata huko hayupo.

“Tuliwajulisha Usalama wa Taifa wakasema hata wao hawajui. Lakini jana (juzi) wakatupigia simu kuwa amekutwa kwenye kisima cha maji baada ya kutokea shida ya maji,” alisema mmoja wa wanafamilia kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza: “Walisema kuwa kisima hicho huwa kinalindwa, lakini tunashangaa ndugu yetu aliingiaje humo.”

Ndugu mwingine alisema: “Awali tuliambiwa kuwa ndugu yetu yuko Muhimbili, tukaenda kuulizia tukamkosa. Baadaye tukaambiwa yuko hospitali ya Lugalo, huko tukamkuta ameshaandaliwa kwa mazishi. Tulipouliza tukaambiwa kibali cha kuzika kiko tayari na usafiri wa ndege uko tayari tujiandae kusafirisha.”

Hata hivyo, msemaji wa familia John Tyeni alisema kuwa ndugu hao walipinga kuusafirisha mwili huo, hadi ufanyiwe uchunguzi (post mortem).

“Tulipokwenda hospitali tukakuta maofisa usalama wamemchukua OCD wa Wilaya ya Kinondoni Wilbrod Mutangungwa na askari wawili na kwenda kufanya post mortem. Yaani kulikuwa na ujanja ujanja unafanyika. Sisi tukamchukua Ofisa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni, RCO Kimola na askari wawili na wapiga picha ndiyo tukafanya post mortem,” alisema John.

Akizungumzia matokeo ya uchunguzi huo, John alisema kuwa watapewa matokeo hayo baada ya kutoka kwenye mazishi yatakayofanyika Musoma mjini mkoani Mara, baada ya kusafirishwa leo. Hata hivyo alisema kuwa macho yake yalikuwa yametoka nje kwa sababu ya kujaa maji. Baadhi ya ndugu wa marehemu walidai kuwa mwili wake ulikutwa ukiwa umetumbuliwa macho huku nguo na viatu vikiwa bado mwilini.

Akizungumzia kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alikiri kutokea tukio hilo na kusema kuwa bado uchunguzi unaendelea: “Ni kweli kuna ofisa usalama amefariki ndani ya kisima, lakini bado tunachunguza. Kwa sababu itabidi tupate taarifa ya daktari ndiyo tuunganishe na uchunguzi wetu,” alisema Kenyela.


---
via gazeti la MWANANCHI



Source: Maswali yagubika kifo cha Ofisa wa Usalama wa Taifa - wavuti.com
 
Poleni wafiwa!hizo kazi walishakula kiapo cha kufa au kupona!kwao sio issue tena!kama ni bahati mbaya au planned kwao ni kitu cha kawaida!naona bandiko hili limerudiwa mara 2 sasa,wana ndugu waende huko huko labda watapewa maelekezo mazuri zaidi badala kulalamika kwenye mitandao!kazi zao nyeti sana na siri sana!kila kitu kwao siri!huwezi share na mwenzako chochote!
 
kifo na uhai ni vitu visivyoweza kutenganishwa ukiwa jasusi.

mengi yatasemwa sana lakini marehemu ndiye aliapa kufia huko.

Ukishaingia huko ndugu hawana mamlaka ya kuihoji jamhuri na ndio maana ya kiapo.

Huko unaweza kufa kwa kifo cha kawaida au kufa kiutata kama utakiuka kiapo.

Jamaa yangu aliyeko huko anasema huyo jamaa alikuwa na matatizo ya akili na alikuwa kwenye matibabu kwa muda mrefu hata ndugu zake wanafahamu kuwa Idara hiyo ndio ilikuwa inamtibu tangu apate tatizo hili hadi kifo chake. Kifo hicho kinahusishwa na tatizo hilo.

Na akasema ndio sababu marehemu alifia katika kisima cha hospitali akiwa katika mwendelezo wa matibabu.
 
Huyu aliyeleta hili andiko mi namshangaa kwanza kalirudisha kwa mara ya pili sijui anaagenda gani na hao maafisa uaslama au alishakutana kashikashi zao,kitu cha ajabu ni kwamba hawa jamaa hatuwajui wala hatuwezi kwenda huko kwenye majengo yao kutafuta ukweli wa jambo hili kutuletea tujadili ni kudanganyana na kupoteza mda wao waliapa kuwa huko na kufia huko hao ndugu zake kama kunakitu hawakielewi waende huko wakaulize kwa wakuu wao ili wapate majibu.
 
Poleni wafiwa!hizo kazi walishakula kiapo cha kufa au kupona!kwao sio issue tena!kama ni bahati mbaya au planned kwao ni kitu cha kawaida!naona bandiko hili limerudiwa mara 2 sasa,wana ndugu waende huko huko labda watapewa maelekezo mazuri zaidi badala kulalamika kwenye mitandao!kazi zao nyeti sana na siri sana!kila kitu kwao siri!huwezi share na mwenzako chochote!

Bora umewapa elimu. Wao wamwachie MUngu.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wakuu, ni bora huyo kaka yake angeeleza ukweli au inawezekana alimweleza ukweli mwandishi ila aliandika kivyake. Angeeleza kuwa kaka yake alikuwa na matatizo ya akili na pengine hilo ndo lilikuwa chanzo cha yeye kutumbukia kisimani.
Kwani Lizaboni wewe unafahamiana na marehemu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom