Tetesi: Utata kuhusu chanzo halisi cha utajiri wa Jumanne Kishimba

Sidhani kama ni kweli, wenyeji wa kagongwa _ Kahama tutaelewana vizuri. Kuna jamaa yangu ambaye anamuita Kishimba mjomba anasemà hakuna cha ndumba wala uganga huo utajiri ni wa ukweli.
Kabisa Mkuu watu wa Kagongwa - Isagehe tunajua hakuna ndumba pale Mzee alipambana kihalali kabisa
 
Mkuu wewe andika kitabu tutangazie tunakipata vipi..hayo maneno ya wajuaji achana nayo...hata The bold alipotangaza kitabu chake aliambiwa atawapata mateja wa story zake ila ameandika na kitabu tumenunua..so mkuu andika mateja wa story tupo
 
Kwa ujumla ushirikina ni imani tu.Mambo yanayohusiana na hayo hata stori zake hazinishawishi kuzisikiliza.
 
Shit happens !
 
Likud usije kumsahau Mzee NYAMAGATI Mzanaki Katiri zaidi ya Alshabab mastermind wa Mauaji yooote ya kulipiza kisasi ktk Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla. Kwa sasa amesha RIP baada ya lile tukio la Mauaji ya watu 17 huko Musoma. Ana historia ya kutisha inatosha kwa kuiandikia kitabu. Work on it mkuuu
 
1994 wakati wa mauaji ya kimbari j4 alikua tayari tajiri akimiliki jengo la ghorofa 5 pamba road,lenye duka kubwa la jumla na godown kubwa mali ya ncu.
Alikua anapakua meli nzima ya mzigo wake kutoka kisumu kenya utajiri wake ulianza 1989 au 1990
 
Alitajirika kwa magendo ya sabuni za mche na maziwa ya kopo kutoka kenya kwani baaada ya vita ya kagera sabuni ilikuwa kama na maziwa ya kopo ilikuwa kama dhahabu.
 
Huo mwaka unaosema 1994 Kishimba tayari alikuwa na MOTO wa hatari.
Utajiri wake umetokana na Uaminifu wake na kujituma.
Wakati kuna uhaba wa bidhaa TZ Kishimba alipata Mchongo wa kuleta Bidhaa mbalimbali za viwandani kutoka Kenya hapo ndio alikusanya pesa kama Mchanga.
Pia alikuwa anakusanya Dhahabu na kupeleka huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…