Tetesi: Utata mkubwa ripoti ya CAG , kuna uhariri umefanyika

Tetesi: Utata mkubwa ripoti ya CAG , kuna uhariri umefanyika

Ni ngumu mno kufuta legacy ya Magu, halafu hii naiona ni bad timing kwao, watu wametoka kwenye maombelezo, halafu ghafla kukatokea na u-turn kama hii?
Kikawaida, watu waliowengi washajua lengo la hiki kikundi nikutaka kumchafua tu, sijui billion ngapi zimepotea, kwendelea zao huko na unafiki wao.
Hivi wewe utawambia nini watu wa Dodoma, mwanza, dar etc kuhusu kazi za JPM? Vituo vya afya, hospital, madaraja, vivuko, miradi mikubwa ya kimkakati you name it, halafu kitokee kikundi kimoja tu kituambie kupitia report ya kinafiki kama hiyo.
Kumpoteza Magu kwenye mioyo ya watz tuliowengi, nkujidanganya tu, watafute kick nyingine siyo hii report uchwara.


Kungekuwa na kura ya maoni ya kuaminika ikafanyika ndio wangekuamini unamaanisha nini? Sana sana hapa utatukanwa na wanaoendeleza huu mkakati ulioshindwa kabla ya kuanza. Nilipo fanya sala leo viongozi hawakukumbuka hata kuongelea kulikumbuka kuliombea Taifa na Viongozi wake. Nyoyo zao zimekuwa mzito kiasi cha kufanya wasahau wajibu wao huo.
 
Tunaendelea na mjadala mzito juu ya yale yaliyotajwa na CAG ni sahihi ,ndivo yalivo au ni mwendelezo wa juhudi za kufa na kupona kupoteza Legacy ya Jpm.

Nikiendelea kufanya utafiti wangu binafsi ,jana nilikitana na taarifa ya CLOUDS media wakitolea ufafanuzi tuhuma za kwamba walilipwa kiasi cha shiling 629.7m bila wao kutoa Risiti.

Katika mjadala huo Clouds walidai kwamba waliposikia taarifa hiyo ikabidi wafuatilie kwenye makabrasha yao wakagundua kwamba risiti walizitoa TRA (AUTOMATIC EFD) na Wizara.

#Hapa ndipo mjadala unaanza ;
1. Kama risiti zimetolewa TRA na Wizarani huko na Clouds wanaujasiri wakusema hilo ,basi kuna uwalakini katika auditing ya kichere kwamba huenda amelishwa matango pori kwa makudi, kwa madhaifu ya watenda kazi au kupangwa.

2. Kama wizarani au TRA hawakumpa kichere risti hizo basi hapo napo kuna shida , kwani hawakumpa? Kuna nia gani nyuma ya pazia? Kwasababu clouds wao wanadai walitoa.Huenda ndio maana hata Kigwangalla anachekelea kwasabab anajua mchezo unaoendelea.

3.Hili suala la risiti imefanyika mwak 2018, Kichere alipaswa kulisema kwenye ripoti ya mwaka jana na si mwaka huu.

Hapa napo kuna tafakuri kubwa , .Report ya Kichere ni ya matumizi ya serikali 2019/2020, suala la risti ni la 2018 ambalo likitakiwa kutajwa 2018/2019 ,ndio maana nina wasiwasi kwamba huenda report hii imeeditiwa na kupachikwa vitu ambavo watu fulani walikusudia kuvionyesha kwa jamii ili watimize yao.

4. Report ya CAG ukiangalia kwa jicho la mbali utagundua imejikita kwenye mambo fulani ambayo mengine ni ya kwelini.

NA ILI UONGO USIJULIKANE KUWA NI UONGO LAZIMA UCHANGANYWE NA UKWELI.

Yaani unaambiwa juu ya stendi ya mbezi ITASABABISHA FOLENI , TENA KWA MIUNDO MBINU ILE ,YA NYEGEZI AMBAYO IPO KATIKATI YA MJI HATUJAAMBIWA KAMA ITASABABISHA FOLENI, DODOMA HATUJAAMBIWA ITASABABISHA FOLENI KISA INAITWA STEND YA MAGUFULI na ndo bora na kubwa kuriko zote, jitihada za kufuta Legacy ya jpm.
Unaambiwa juu ya SGR, yaani unatajiwa SGR imesababisha hasara zaidi ya 3b hatuambiwi imeingiza faida kiasi gani , mashaka matupu, nilitegemea atuambie na upande wa pili imeingizia faida kiasi gani.

Kwahiyo utagundua wazi kuwa hii report kama imepikwa ili kuweza kuharibu taswira ya jpm

5.Kuna taarifa ya siri kwamba report hii tayari ilikuwa imeshaandaliwa na CAG lakini kuanzia trh 18.3.2021 ,ilianza kufanyiwa editing ,kwa maelekezo/maagizo kutoka juu.
Ingawa taarifa hizi si rasimi lakini ninaweza kuziamini.

-Cag alianza kwa kutoa taarifa nusu ,akagusia suala la ndege watu wakaibuka na kulaumu ,ndege imekula hasara ya 60b ,wakajitokeza watetezi na kusema hio mbona hasara ndogo, ikawa imeisha.
Kama iliandaliwa tangu mwaka jana ,kwanini alitoa taarifa nusu? Au tuseme editing ilikuwa haijakamilika?
-Kama watu wanasema haya yanatokea kwasababu jpm hakutaka kukosolewa ,tujiuliza hii report imeandaliwa lini ? Wakati au baada ya kifo cha jpm? Kama ni kabla ya jpm ,basi tukubali kuna editing ya taarifa kwa maana jpm asingeikubali(kutokana na hoja zenu kuwa hakutaka kukosolewa).
Kama ilieditiwa kwa maagizo ya nani ? Kwamakusudi gani?

KAMA HATUKUSIKIA HIZO HASARA ZA NDEGE MWAKA JANA , LEO HII TENA MUDA MFUPI KWAMBA ZIMESABABISHA HASARA ,KUNA MASHAKA MAKUBWA.
Nataka kusema kwamba Huenda kichere na timu yake kwa maagizo toka juu alichambua MIRADI ILIYOKUWA INAMPAISHA JPM Na kuweka figisu ilimradi kuonyesha haifai , alikulupuka au alipiga hela kutimiza matakwa ya hao walioko juu.
#Kama ni maagizo ya kikwete ,basi ili kutimiza lengo lake kuanzisha mfumo wake wa ponda mali kifo kinakuja.
#Kama ni Samia ni kutaka kufuta kivuli cha jpm kwenye uongozi wake , yaani yeye si kama jpm ,yeye ni bora zaidi.

MWISHO
JPM aliwahi kusema "ukiona adui yako anakushangilia sana rudi nyuma ujiulize umekosea wapi"

NAONA GIZA NENE MBELE YA URAIS WA SSH, NAONA NCHI INARUDI KWENYE KIKWETISM .NAONA MIKATABA MIPYA YA MADINI ,MIKATABA MIPYA BOMBA LA KUTOKA TANGA HADI HOIMA.

LAKINI YOTE KATI YOTE NASEMA KWAMBA " WANANCHI WENGI HASA WANACCM WANAIMANI KUBWA NA JPM NA WAKO TYR KUSIMAMA NAYE MPKA MWISHO".
UPEPO HUU UTAPITA , REPORT ZITASOMWA ZITATAJWA HASARA ZA MABILIONI WATU WATASHANGILIA ,MWISHO WATU WATASAHAU LAKINI MIRADI ALIYOIANZISHA JPM ITADUMU VIZAZI HADI VIZAZI.

Asilimia kubwa ya wanaccm hivi sasa hawana imani tena na SSH ,WENGI WAKO KIMYA ILA WANAJUA WATAFANYA NINI .
Yaani asilolijua SSH na wenzake watu wengi wanamkubali JPM kuriko hata ccm, wapinzani wengi kama kafulila wanamkubali JPM kuriko ccm.Wengi wanaomshangilia ni wa upinzani ambao nao wanamtumia tu.

ASANTE JOHN
We kweli jinga unauliza SGR imeingiza faida wakati haijaanza kufanya kazi
 
Haya madudu yote anabebeshwa mzigo marehemu tu ila viongozi ambao walikuwepo kwenye hiyo serikali yenye hayo madudu wamekaa kimya kama hawahusiki na lolote vile ndio kwanza tunasisitiziwa kuwa hii ni serikali ya awamu ya sita na Mama ndio kwanza anamwambia CAG asema tu bila kumung'unya. Nadhani ingekuwa nchi za wenzetu kuna watu lazima wangewajibika ila ndio hivyo huku watu wanaishia kufurahia kufa kwa Magufuli na haya madudu yote kuelekezwa kwa Magufuli tu.
Ulitaka aulizwe nani?
 
Watu wanahangaika sana kuposti. Kusifu au kukashifu, mzee alikuwa na mazuri na mapungufu pia..ndivyo binadamu tulivyo...tukubali kulikuwa na mazuri na mabaya. Tatizo lipo kwenye mizani imeegemea upande upi......
Kwenye mabaya
 
Mjinga bibi mkubwa wako kwani umeliazimishwa kusima?
Tuliza mshono wewe kiwewe.
Habari zenu zimekwisha na sasa hivi lazima mtafute ridhiki yenu kwa nguvu na jasho haswaa.

Mkizoea kulishwa kama kinda la ndege shorwe
 
Query za CAG zinajibiwa kwa documents na mazungumzo na CAG na siyo kwenye vyombo vya habari.

Kila aliyeguswa na CAG akikimbilia kwenye media itakuwaje?

Hao Clouds wako tayari kumpa airtime yeyote aliyetajwa na CAG kujisafisha? Au kwa sababu tu wao wana media wanaamua kuachana na ethics za auditing wanakimbilia kutafuta huruma ya watu?
Inabidi waitwe hawa. Wakifungiwa kwa matumizi mabaya ya vyombo vya habari..wanaanza kulia lia.
 
#Hapa ndipo mjadala unaanza ;
1. Kama risiti zimetolewa TRA na Wizarani huko na Clouds wanaujasiri wakusema hilo ,basi kuna uwalakini katika auditing ya kichere kwamba huenda amelishwa matango pori kwa makudi, kwa madhaifu ya watenda kazi au kupangwa.

2. Kama wizarani au TRA hawakumpa kichere risti hizo basi hapo napo kuna shida , kwani hawakumpa? Kuna nia gani nyuma ya pazia? Kwasababu clouds wao wanadai walitoa.Huenda ndio maana hata Kigwangalla anachekelea kwasabab anajua mchezo unaoendelea.

3.Hili suala la risiti imefanyika mwak 2018, Kichere alipaswa kulisema kwenye ripoti ya mwaka jana na si mwaka huu.
Mnajaza server bure,....!
 
Tuliza mshono wewe kiwewe.
Habari zenu zimekwisha na sasa hivi lazima mtafute ridhiki yenu kwa nguvu na jasho haswaa.

Mkizoea kulishwa kama kinda la ndege shorwe
Shorwe...hahaha ndege wajanja wajanja hawa kuliko mbayuwayu.
 
Back
Top Bottom