Tetesi: Utata mkubwa ripoti ya CAG , kuna uhariri umefanyika

Mataga kazi mnayo siyo mchezo
 
achaneni na CAG....mbona hatukusikia awamu ya nne watu wanamlalakia CAG....Utoh alipokuwa anaibua uozo?.....
 
Ulitaka aulizwe nani?
Sio kuulizwa bali nasema tu kuwa viongozi ambao walikuwepo kwenye awamu ya tano ambapo ndio hayo madudu yamefanyika wao wamekaa kimya kana kwamba sio wao, wenyewe wanasisitiza kuwa hii ni awamu ya sita kwahiyo wao hawawajibiki na yaliyotokea awamu ya tano hayo yote ni madudu ya marehemu tu wao wako safi kabisa.
 
Heri kuwa na mwizi anaefanya vitu vya kuonekana!
Deni la taifa ni kubwa mno. Unalijua hilo?. Isitoshe, miradi hiyo itakufa moja baada ya mwingine. Ni ya umma, hakuna usimamizi. Ikifa, deni hili la taifa litalipwa na nini? Dunia nzima sasa hivi serikali haifanyi uzalishaji. Uzalishaji unafanywa na sekta binafsi huku serikali ikikusanya kodi. Sasa magufuli amefanya kinyume. Ameshaiua nchi hii kama alivyokufa yeye.
 
Kwahiyo utagundua wazi kuwa hii report kama imepikwa ili kuweza kuharibu taswira ya jpm

Hapa ndipo ulipoharibu......Huyo Shujaa wenu wa Africa kajiharibia yeye mwenyewe.....Soma Taarifa ya mbowe ...JIWE alikuwa katili na Mwizi.
 
Kwani magu ana mpango wa kugombea tena mpaka watu watumie nguvu kumchafua?

Je umewahi kuona report yoyote ya CAG kabla ya hii ya kichere? unafahamu zinafananaje?

Binafsi wewe kwanini unadhani watu wameamua kumchafua magu ikiwa tayari ameshafariki? Mnazungumzia as if amesafiri watu wanatumia kusafiri kwake kumchafua ili akirudi asikubalike, Ni lini mtaelewa kuwa hakuna anayechafuliwa bali wananchi wamepata wasaa wa kusikia yale yaliofichwa gizani kwa miaka 5. Vitu mnavyovikiria pro Magu havipo practically ni hisia zenu tu zinazotokana na hali ya kuwa katika "denial".
 
toa huu uchafu
 
😂😂😂 mleta uzi kaniacha hoi hapo anaposema SGR imetengeneza hasara ya 3B sasa anauliza kwanini hawasemi faida iliyotengenezwa, jama jama kuna hasara sasa faida inatoka wapi, sasa hiyo faida si wangeitumia kucover hiyo hasara ndugu yangu.
 
Nilivyosoma hapo uliposema kuwa mnaambiwa SGR inatengeneza hasara ya 3B na hamjaambiwa faida nikaamua nipuuze hili bandiko.

Hivi mleta mada maboss zako wakiona huu utetezi watakulipa kweli? Huko Matagani hakuna mwenye akili timamu anayeweza walau kupangua hoja? Jibu ni kuwa hoja za CAG hazipanguliki, mnagusa gusa tu mnaishia kutuletea viroja.
 
Jamani ndugu zangu Wasukuma.. Kubalini ukweli kwamba Meko Kafa.. Jamani Meko Kafa.. Yaani Kafa. Hawezi rudii.. Mbona Hamuaminii? Naona design kama Hamtaki kukubali.. Mlitaka awe Raisi wa malaika? Basi yeye Meko kakataa.. anataka awe Kiranja Kule aliko. Japo baada ya report ya CAG amevuliwa Ukiranja wake.
 
Wenye akili wanajua kua ukiona unapambana na legacy, Basi kunajambo lisilo la kheri linakuja.
Haiwezekani upambane na marehemu!!
Si Alisha kua marehemu hana madhara? Fanta yako yaonekane, watu wakukubali!
Shida ni kua marehemu kaacha viatu vikubwa mno na warithi Wana pima upepo.

Ccm achaneni na Ilani yenu ya uchaguzi na iueni miradi mkakati alio ianzisha Marehem halafu njooni mpambane na nguvu ya walalahoi ambao sikuhizi Wana smart phone.

Naamini hizi ni ngonjera tu Ila legacy ya JPM itamalaki.

Nahisi ccm na TISS wanawaingiza chaka Wapinzani ili kujenga umoja wa kitaifa.

Or otherwise, kunakaburi la ccm linachimbwa.
My own mtazamo(views)
 

Ilo ndio linalowaumiza kichwa ,hawaamini kabisa kwamba MEKO KAKATA KAMBA aka KANG'ATA SHUKA.
 
😂😂 Kiukweli hawana hoja za kumpinga CAG kabisa. Na hii inasababishwa na ukosefu wa data na taarifa sahihi, wanakosoa ripoti kwa kuchomoa taarifa kutoka kwenye hiyohiyo ripoti halafu wanapinga kijanja janja ili kujifariji.

Waipinge kwa kuleta taarifa zao ambazo ni sahihi sio kusema tu sio sahihi na kilichosahihi hamleti.

Mkuu huyu leo atajua atakapokula hapati mgao huyu kajiharibia mwenyewe😂😂
 
Nataka uniambie mwaka ambao CAG ,hakuona madudu sehem yoyote ktk hii nchi,alaf ndio urud uniambie CAG uyu amepewa maelezo kutoka juu

"3.Hili suala la risiti imefanyika mwak 2018, Kichere alipaswa kulisema kwenye ripoti ya mwaka jana na si mwaka huu.



Hapa napo kuna tafakuri kubwa , .Report ya Kichere ni ya matumizi ya serikali 2019/2020, suala la risti ni la 2018 ambalo likitakiwa kutajwa 2018/2019 ,ndio maana nina wasiwasi kwamba huenda report hii imeeditiwa na kupachikwa vitu ambavo watu fulani walikusudia kuvionyesha kwa jamii ili watimize yao.
"
 
Ni ujinga mtupu tu, ina maana CAG hakufanya ukaguzi ofisi ya makamu wa rais? Au huko hakuna madudu? Mungu hafanyiwi unafiki muda utaongea, CAG mwenyewe sura mbaaaya.
 
"Wenye akili" akina nani mataga? Na mimi nikikwambia "wenye akili" wanafahamu hakuna anayepambana na Hayati bali uhuru wa kutoa maoni ambao umepelekea hata report ya CAG kusoma na kuchambuliwa hadharani ndio yameleta haya utanibishia? Ni kipimo kipi kinaonesha ni wapi wenye akili kati ya ninaowazungumzia mimi na unaowazungumzia wewe.

FYI, Hayati hakuwa anatekeleza ilani ya chama, alikuwa na ilani yake kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…