Utata mkubwa wazunguka KIFO Cha Mtoto wa JB MPIANA Oceane aliefariki kwa ajali

Utata mkubwa wazunguka KIFO Cha Mtoto wa JB MPIANA Oceane aliefariki kwa ajali

Tochuku

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
5,322
Reaction score
8,412
Mwanamuziki nguli na mkongwe wa DRC wale wapenzi wa muziki ya Congo , rhumba , soukouss, n k watakua sio jina geni kwao, JB MPIANA , akiwa mapumzikoni South Africa, alitaarifiwa juu ya kifo cha Binti yake Océane kutokana na ajali ya gari.

Océane alikua na mazoea yakwenda mara kwa mara mazoezini ilikujiweka sawa kimwili na kiafya.

Wakati akirudi nyumbani pande za saa nne usiku wa Ijumaa tarehe 21 March, ndipo umauti ulipo mkuta pale alipogongwa na gari na kwa bahati mbaya derava wa gari hilo alikimbia na wala hakufahamika ni nani.

Polisi Jijini Paris bado inaendelea na uchunguzi juu ya tukio Hilo la kusikitisha.

Océane Mpiana, ni binti ambae JB Mpiana kamzaa na Mama "Nicole Longondo" yule ambae Koffi Olomide kamtungia Wimbo (Miss Nicole).

Kwasasa Mama huyo ni Mchungaji, kadhalika marehemu Binti yake Océane alikua pia Mwimbaji wa nyimbo za injili.

Océane Mpiana kafariki akiwa na umri wa miaka 27.

JB MPIANA kapitia changamoto kubwa saana maana katika kipindi cha miezi michache kafiwa na Wanamuziki wake mashuhuri wawili, ambao ni SEGUIN MIGNON MANIATA na Yaya ZULEMA.

Utata kwenye msiba baba mzazi ambaye ndio JB MPIANA hakuwepo makaburini, watu walihoji na Bado wanahoji kupitia kwenye viunga vya mitaa ya kongo..wengi wakisema yawezekana ni "kafara" ama masharti kwamba yeye kashindwa kufika kumzika mtoto wake...kiafrika , kwa baba mzazi upo hai na unajua mtot wako amefariki na anazikwa , hautokei kwenye msiba? Ni jambo la ajabu sana. Ajabu nyingine ni kule makaburini jeneza lilitangulizwa wima na kulikua hakuna sehem kama kumechimbwa kwa ajili ya kuzika kama desturi za kiafrika zilivyo ila ni sehem ilikua ishaandaliwa na kusakafiwa kabisa ila uwazi ni kama mraba kuweza kupitisha jeneza likiwa wima...kwahio minong'ono ilikua mingi msibani na hata Sasa watu wanaongea ila mwisho wa siku atkayeumia zaidi ni mama na kaka na dada zake Oceane , wengine walimwengu watasahau na kuendelea na mambo yao. Kwaio JB kabakiwa na watoto 5 pekee..badala ya 6.

Wengi wanasema Mziki wa kongo kuweza kudumu kwenye "game" sio jambo dogo, watu wametolea hata mifano mbalimbali, kama fere "alivyomtoa" ndugu yake na hata audio za watu wanaojua hio Siri zilisambaa, na wasanii wengine...

Mungu aendelee kumpa pumziko jema binti Mrembo Oceane.
 
Ila kuna mambo watu wanapenda tu kuyakuza.
Sasa kisa mtu hajatokea makaburini basi ndio yeye katoa kafara!? Mnajua yanayoendelea kwenye familia? Mama mchungaji..baba ndio hivyo. Kwann msifikirie vingine?
Haya, makaburini hajakwenda na bado kuna mazonge huko yametokea sijui jeneza limefanya nini sijui, sasa mtu hayupo ,hayo anasababishaje?
 
Hizi kafara wanatoaga wapi? Nina mjomba wangu mmoja mlevi mlevi nikipewa hata milioni 50 natindua tu hii ng'ombe.
Huu ulimwengu kila kitu kipo kwenye kalenda, hakuna jambo litafanyika liwe nje ya hapo.
 
Marehemu kagoma picha zake zisitumike.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom