Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine


Bila shaka maelezo yako ni majibu tosha juu ya mauaji ya mpendwa wetu na kijana mahiri wa kimasai
 

Taarifa za Polisi inaweza kuwa tofauti na hali halisi uliyopewa? Jaribu kuwasiliana n Polisi maana kuna mtu alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa hilo.
 

Ili iweje?
Vitu vingine ni state matters kwamba ajali yake ilipangwa ama ilikuwa ajali ya kawaida haibadilishi dhana kwamba alikufa!
 
Ila ukweli kabiiisa tu ni kwamba hiki kifo cha SOKOINE kilikuwa na mikono ya watu siyo bure.Haiwezekani wanafamilia wakataliwe hata ile kuuosha tu mwili wa MAREHEMU kama vile hakuwa ndugu yao.CCM hii tabia ya kuuana wameianza kitambo saaana na watanzania wanajua kila mauaji yaliyokuwa yakifanywa na hawa wenzetu ila mikwara iliyokuwa inapigwa na government hapo nyuma iliwafanya watu wasihoji chochote juu ya maovu yaliyokuwa yakifanywa.
 


Mkubwa nakwambia umenikumbusha kitu gani tena? Usinilize Mkubwa! Nakumbuka kabisa mvua kubwa ilinyesha pasipo kukatika takrban masaa 7 na RTD enzi hiyo ambayo leo ndiyo TBC ikitangaza moja kwa moja mazishi yake!
Nilikuwa mdogo sana kwani nilikuwa darasa la kwanza ila nilikuja barabarani kuomboleza kifo ya shujaa huyo wa Tanzania mzalendo wa Nchi yetu!
Nakumbuka kabisa wanakijiji wote wababa kwa wamama walijitokeza barabarani na huku vijana karibu wengi wa kabla lake (Maasai) Morani wakiumiza miili yao kwa mori siku hiyo ya mazishi nilikuwa mdogo lakini sitokaa nikasahau msiba huu mchungu kwa Watanzania walio wengi kwa JEMBE huyo Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Mwenyenzi MUNGU mwingi wa Rehema na ampe pumziko la milele shambani mwake Bwana wetu!

Ameeen!
 

mwili wake ulikuwa ktk land rover pick up,jeneza lilipambwa na mauwa ya kutosha na mbele yake iliwekwa picha yake kubwa...black and white .....rtd nyimbo za maombolezo zilipigwa......
 
nilikua bado mdogo sana,ila nakumbuka kipindi wanatangaza ndo nilikua natoka RTC kununua sukari ,ndo nikasikia ulikua mshituko na hudhuni sana tulifuatilia mazishi live kupitia RTD.

Kisha nikiwa sec miaka ya 90 tukawa na urafiki na mtoto wa mmoja wa mkuu wa majeshi ambae pia kwao ni butiama karibu kabisa na kwa jk,akawa anatuambia ni siri kubwa ila mwili wa sokoine ulikutwa na jeraha la risasi mgongoni.
Ila sikuwahi kuamini asee.
 


Naunga hoja yako mkono IKINGO. Hili ccm ilihusika moja kwa moja.

Ni swali. Mwaka huo 1984 Edward Lowassa alikuwa wapi ndani ya serikali hii?
 
Last edited by a moderator:


Hiyo green,Ilikuwa siku ya alhamisi saa 7:15 mchana
 
1.Itasaidia nn ukijua leo au unajifunza mbinu mbali mbali za assasination na unajaribu kuvuta theory ipi ili apply.
2.Kama ni ajari ya gari moja tu picha inaonyesha kuwa iligongwa upande wa dereva. Na ni benzi ngumu upande wake yeye aliumiaje kama sio kazi maalum.
3. kumbu kumbu za mahakamni zinaonyesha vp kuhusu debi sijui aliachiwa kwa ground zipi?maana ulikuwa ni msafara na unajulikana gari ipi ni ya waziri mkuu.

Na kama princense Diana alikufa mbele ya makamera na bodyguard si ajabu kama wao wazungu walijifunzia kwetu maana hii ndio TZ ilianza .
5.Kaka zangu walio nizid umri na waliokuwa wanaishi upanga na uhindin kisutu wanadai miaka ile wahindi walikuwa wanaacha mipesa bara barani mnapita mnaokota.
6.Na BOT iliungua mwaka 1984 na mwaka huo huo jk alitangaza kung'atuka sababu aliona usalit wa serikali yake kutoka kwa watu anaowategemea sana.
 

Siyo Dumila bali jirani na Dakawa(kijiji cha Luhindo). Pamejengwa kumbukumbu ku muenzi.
 

RPC wa Morogoro wawakati huo,alipigiwa sim kutoka makoa makuu dakaki kadhaa baada ya tukio kuulizwa kama anajua kinachoendelea(hali ya usalama),binafsi hakuwa na taarifa yoyote mpaka baadae alipokuja kutaarifiwa na vijana wake kuwa waziri mkuu kafariki katika ajali..Utata pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…