Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.
nimeona maswali yako. ila hujaweka utata wowote. sema wewe ulikuwa hujazaliwa AMA ulikuwa mdogo. waliokuwa watu wazima wanajua Majibu ya maswali yako yote. je dumisan dube umewahi kumsikia? yuko hai mtafute Ana majibu yote
 
huyo kijana anaonekana kachoka kachakaa hana hata mia mfukoni hiwezi kumfananisha na riz1 kiuchumi hata kidogo.
hiyo Lazaro wakati babaake anakufa alikuja , an aonekana ni kichaa Fulani. mbona Joseph mdogo wake alielewa na hana shida yuko us ubalozini. not sure though niliwahi kuiutana naye DC akaniambia hivyo.
 
Wana JF,
Taarifa ya kifo cha Edward Moringe Sokoine ilionyesha kwamba chanzo cha ajali ilikuwa ni muingiliano na gari lililokuwa likiendeshwa na Dumisani Dube, Mkimbizi wa toka Afrika ya kusini akiwa kambi ya Dumila. Sikumbuki juu ya hukumu yake lakini baadaye aliachiwa na kurudishwa Afrika kusini. Wengi hawakuamini na hata sasa hawaamini ilikuwaje msafara unaoongozwa na pikipiki na magari mengine mbele, washindwe kuzuia gari nyingine ktk barabara.

Wakati ule Dumisani Dube alikuwa kijana wa miaka 23, kwa sasa kama bado yuko hai, atakuwa ni mtu mzima wa miaka zaidi ya 50.

Naamini tunaweza kupata habari rasmi juu ya nini kilitokea wakati ule kama tutampata bwana Dube. Kwa wale mulioko Afrika ya kusini, naomba mtusaidie kumpata mtu huyu maana kwa wa-sauzi wote waliokuwa Tz lazima wanamfahamu bwana Dube. asipofahamika, basi tutaelewa ni jina la bandia lilitumika kumuondoa Sokione.
 
Hii fukua fukua hii mwishoni tutaishia kupigana vita.Let gone be the bygones aliyekufa hafufuki jamani
 
Na ndio maana tupo katika jukwaa la Historia.

Kizazi cha sasa ambao mwaka 1984 walikuwa bado wadogo au hawajazaliwa, wanapokutana na jina la Hayati Sokoine wanaweza kujua huenda ni hadithi ya kufikirika.

Hivyo kulijadili suala hili ni muhimu kwani kama sisi ambao tulikuwepo tunaona kuna utata je itakuwaje kwa wale ambao wanasoma katika Historia ya Tanzania, kuhusu Sokoine???

mbona vifo vingi vimepita lakini watu wanahoji kifo cha Sokoine na karume pekee???

Lazima kuna jambo hapa na huu unyama nduio tumeurithi hadi leo ukiwa mpinga ufisadi lazima utafutiwe mbinu uondolewe Duniani.

Wanataka tuwaache wakubwa kimadaraka wafanye watakavyo.

Je, tutakomeshaje hali hii kama tusipoijadili????


RIP our Prime Minister Edward Moringe Sokoine


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom