UTATA WA KIMIPAKA: Waziri Makonda kutoa amri kwenye Vivuko Mwanza—Anasimama kama nani kisheria na kiprofeshinali?

This is purely duplication of efforts which led into inefficiency in performance na badae kupelekea kuleta conflict among actors. This is pathetic!!
 
This is purely duplication of efforts which led into inefficiency in performance na badae kupelekea kuleta conflict among actors. This is pathetic!!
Ni mlezi wa Mkoa wa Mwanza kama ilivyojidhihirisha kwenye Katiba ya JMT Sura ya 26760 ibara ya 3200 (i) kiongozi kufutana na watalaam waliobokea katika Consitution Law mdau Viali Senior Member LLB, LLM, PhD zote kutoka Yale University
 
 
Andiko lako limenisaidia kujua kiasi kidogo cha uelewa wako vinginevyo ni chuki uliyonayo aidha kwa makonda, samia au serikali, kujificha kutaja vifungu hakutokusaidia.

Jiulize maswali madogo tu;
1. je makonda hajui kama yeye sio waziri wa ujenzi mpaka aende kwenye hayo maeneo?
2. Kwann aende mwanza na sio mkoa mwingine?
3. kwann rc, mwenyekiti wa chama na wataalamu wengine wampokee na kumpa ushirikiano kikazi?
4. kwann baada ya kusikia changamoto amesema atampigia waziri husika kumpa feedback kwann asingemaliza mwenyewe palepale?

Nakusaidia tu katika vichache unavyovijua ongeza na lingine kuwa nchi haiongozwi na katiba pekee skama utakikosa kitu kwenye katiba usishupaze fuvu utazipata aibu ndogondogo rejea nyaraka mbalimbali na mazoea.

Nikuulize tu unataarifa zote za vikao vya baraza la mawaziri maamuzi na maazimio yake?

Kama unadhani kuna sehemu katiba imekiukwa hii nchi ni ya utawala wa sheria nenda Mahakamani ukafungue shauri upate tafsiri sahihi lkn sio hizi chuki za wazi.


unaweza kutuma au umeshawahi kuiona public barua iliyomteua dc kukaimu wilaya nyingine? kwahiyo unataka barua ya rais uione public kuwa kamtuma makonda au unadhani rais na mifumo ya nchi haijamuona makonda Mwanza na wamekaa kimya, unadhani sheria za nchi hii unazijua peke yako? au unadhani viongozi wa nchi hii hawajui uatwala wa sheria au hawaijui katiba? ni mara ngapi rais anamtuma kikwete akamuwakilishe ikiwa makamo, pm wapo? agizo na kauli ya rais ni maelekezo ya mamlaka sio kuvunja sheria.

haya 'mwanetu' great thinker rejea ibara hii ya katiba 34(4) ikusaidie kupunguza chuki binafsi.
 
je alienda hapo kama nani? kama alienda kwa niaba ya kiongozi fulani basi aliyetamka si yeye bali aliyemtuma hapo ndiye aliyetamka.
 
Ni mlezi wa Mkoa wa Mwanza kama ilivyojidhihirisha kwenye Katiba ya JMT Sura ya 26760 ibara ya 3200 (i) kiongozi kufutana na watalaam waliobokea katika Consitution Law mdau Viali Senior Member LLB, LLM, PhD zote kutoka Yale University
katiba ya jmt ibara ya 34(4)
 
katiba ya jmt ibara ya 34(4)
Kaka Viali, Ibara ya 34(4) uliyong'ang'ania inaongelea mamlaka ya utendaji ya Rais na uwezo wake wa kuwapa majukumu wasaidizi wake kiserikali. Hakuna neno wala nafasi ya 'Mlezi wa Mkoa' kwenye Katiba yote ya nchi hii. Katiba inamtambua Mkuu wa Mkoa (RC) pekee kwa mujibu wa Ibara ya 61.
Hiyo 'Sura ya 26760' uliyotaja haipo duniani, Katiba yetu ina Sura 10 tu! Huyo Profesa wako wa Yale atakua alikufundisha Katiba ya nchi ya kufikirika. Au labda na wewe umeshakuwa 'Profesa Viali' wa kutunga vifungu vyako mfukoni?
Sasa msikilize mtaalamu nikunyooshe kidogo, 'Profesa' Viali:
  1. Katiba haina shortcut za maneno ya mdomo jukwaani. Hicho cheo cha 'Waziri Mlezi' ni cha kisiasa tu, hakina nguvu yoyote ya kikatiba kuingilia 'Instrument of Office' (Hati ya Majukumu) ya waziri mwingine aliyepo kazini na anayelipwa mshahara na kodi zetu.
  2. Rais akitaka kukasimu madaraka kwa Waziri wa Michezo kwenda kutoa amri kwenye sekta ya Viwanda au Ujenzi, lazima atoe Hati Maalum ya Kimaandishi (Written Instrument). Huwezi kwenda kwenye ziara ya kusaka kiki na sifa za kisiasa mbele ya kamera halafu ukaingilia wizara ambayo huna dhamana nayo kisheria wakati waziri mwenye sekta yupo ofisini anachapa kazi.
Inabidi tu unyooshe mikono juu ukubali kashindwa hoja, 'Profesa' Viali! Nenda kanywe maji kwanza kisha rudi darasani ukasome Katiba halisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siyo hizi unazozinukuu kwa kukariri bila kuzijua!"
 
Hiyo namba 2 mbona hujasite kifungu kwenye katiba unaongea maneno yako? weka kifungu.

hii nchi ni ya utawala wa sheria kwa kufuata katiba kama unahisi imekiukwa nenda Mahakamani upate tafsiri sahihi.

hiyo ibara ya 34(4) nimeona umehangaika nayo kama una kamba shingoni.
 
Ndugu Viali,
Umerudi kwa kasi ukiwa umeshikilia hiyo Ibara ya 34(4) ya Katiba kama ngao yako ya mwisho naona unaikimbilia kila unapobanwa huku ukidai nahangaika nayo kama nina "kamba shingoni". Ila kwa bahati mbaya sana unaisoma hiyo ibara kishabiki mno bila kuelewa hata misingi midogo ya Sheria za Kiutawala (Administrative Law). Ngoja nikutoe kwenye huo mtego wa fikra ulionaswa nao.

1 Kuhusu Hoja ya "Mikoa ya Kulea" (Yale niliyokubatiza wanasomeshaga hivi?)
Unaniuliza kwa msisitizo hapa: "Mbona hujasite kifungu kwenye katiba, weka kifungu?"
Viali hapa sasa ndipo ninapoona nilipatia sana nilivyoamua kukubatiza kwa utani zile digrii za LLB, LLM, na PhD za Yale University. Ule ulikuwa utani wangu tu uendane na huu ujuaji mwingi unaouleta hapa jukwaani lakini naona umeubeba mazimazima na unautolea jasho.
Hivi kweli mtu mzima unataka nikuonyeshe kifungu cha kitu ambacho nimekwambia hakipo kabisa kwenye Katiba? Katiba ni waraka unaotaja mambo yaliyopo kisheria sio kamusi ya kuorodhesha maneno ya kufikirika. Kama mfumo wa "Mikoa ya Kulea" ni kitu rasmi cha kiserikali kinachompa Waziri wa Michezo rukhsa ya kwenda kukagua na kuamuru vivuko vianze kazi basi wewe msomi wangu wa Yale unayeutetea ndio unapaswa utuwekee hicho kifungu hapa mezani. Ukweli kwamba umeshindwa kukitaja unathibitisha pointi yangu: hiyo dhana ni porojo za ndani ya chama chenu tu haina uhusiano wowote wa kisheria na usimamizi wa miradi chini ya TEMESA au TASAC.

2 Mnyambuliko wa Ibara ya 34(4) na (5) — Ukasimishaji Madaraka sio "Hadithi za Mdomo"
Umekimbilia Ibara ya 34(4) inayosema Rais anaweza kutekeleza mamlaka ya nchi mwenyewe au kwa "kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine". Unadhani kifungu hiki kinampa Rais nguvu ya kumtuma mtu yeyote kufanya kazi yoyote wakati wowote kwa maneno ya mdomo tu ya jukwaani. Hapa ndipo unapofeli kisheria kwa sababu hizi mbili:
a) Uliruka neno "Bila ya kuathiri..." Hiyo ibara ya 34(4) inaanza kwa maneno mazito sana: "Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii..." Maana yake ukasimishaji madaraka hauwezi kufanyika kwa namna inayovunja ibara zingine au sheria zilizotungwa na Bunge.

b) Ulikimbia Ibara ya 34(5)(a) inayokunyoosha Umesoma namba (4) ukakimbia ibara ndogo ya (5)(a) iliyo hapo hapo chini. Inasema wazi kuwa masharti ya ibara hiyo yasitafsiriwe kama yanahamisha kwa Rais mamlaka yoyote ya kisheria yaliyokabidhiwa kisheria kwa mtu mwingine. Bunge lishapitisha bajeti na kuipa Wizara ya Ujenzi na TEMESA mamlaka ya vivuko kisheria chini ya Sheria ya Fedha za Umma (Cap 348). Kila wizara ina Katibu Mkuu (Accounting Officer) wake anayewajibika kisheria. Rais hawezi kuhamisha mamlaka hayo kwa Waziri wa michezo kwa maneno ya jukwaani bila kufuata taratibu za kimaandishi. Sheria haitambui ukasimishaji wa kutumia kipaza sauti na makofi ya wananchi lazima kuwe na Hati rasmi ya Majukumu (Instrument of Office) au Waraka wa Serikali (Government Circular).

3 Kichaka cha "Nenda Mahakamani"
Kila ukizidiwa hoja unakimbilia ule usemi wako wa kawaida: "Kama unaona imekiukwa nenda Mahakamani". Huu mchezo wa kukwepa hoja unachekesha sana na haukusaidii. Jukwaa hili ni la Great Thinkers kwa ajili ya kujenga uelewa wa wananchi (Civic Awareness). Hatuhitaji kusubiri mpaka Mahakama Kuu itoe hukumu ndio tujue kuwa kuweka majini kivuko ambacho hakijawa commissioned kisheria na TASAC ni kucheza na usalama wa abiria na ni kuvunja sheria waziwazi.

Ushauri wangu kwako mdau Viali Senior Member: Yale makaratasi niliyokutunukia kwa utani yashushe kidogo ulinganishe na sheria halisi za Tanzania. Nchi haiongozwi kwa "mazoea" au hadithi za vijiweni inaongozwi na Nyaraka Taratibu na Kanuni zilizopo kwenye Gazeti la Serikali.

Haya leta hapa kifungu kinachoruhusu Waziri wa michezo kuingilia miradi ya ujenzi na vivuko bila karatasi yoyote ya kimaandishi kutoka mamlaka za juu. Ukshindwa rudi kijiweni ukaendelee na siasa za kushangilia lakini hapa tuachie Great Thinkers tujadili misingi ya Utawala Bora.
Mwisho kabisa nikuweke wazi kuwa mimi sijakimbia kukujibu hata kidogo. Nilikupa tu uwanja uandike porojo zako zote ili nikuonyeshe kwa ushahidi hapa jukwaani kuwa hukijui kabisa unachokitetea. Umekalia ushabiki wa kisiasa huku upande wa sheria ukiwa mweupe kabisa!
 
........bila kuathiri.....ni ibara gani imevunjwa?

kuna sehemu nilikwambia hujasite kifungu nilidhani uttasite kifungu kumbe unaongea maneno yako ambayo hayana nafasi.

Makonda ameshamaliza ziara mwanza na ameacha maelekezo kuhusiana na vivuko na watendaji wanafanyia kazi na wananchi watanufaika, una lingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…