Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Hiyo high sabbath ilikuwa siku gani?
 
Hiyo high sabbath ilikuwa siku gani?
Mkuu kukusaidia tu jaribu kuangalia aina mbalimbali za sabato ambazo zilishikwa na wayahudi.

Kuna sabato za namna nyingi hapa katika tukio hili yohana anaitaja kabisa ilikuwa "High Sabbath" maana yake the first day of the feast of unleavened bread yani siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu.


Pili Yesu anaitwa mwanakondoo aondoe dhambi za ulimwengu sehemu kadhaa ilikuwa lazima auwawe siku maalum sio siku yoyote tu hii ni kwa sababu lazima ishara zote na unabii ukamilike.

Mkilazimisha Friday crucifixion mnaongeza maswali mengi kuliko majibu na mnawapa haki wayahudi kumkataa kwasababu anakuwa hakutimiza unabii wowote sasa wao wata muamini vipi MTU ambae muongo??? Kwa kigezo hicho wayahudivwanakuwa sahihi kumkataa lakini hali haikuwa hivo ni hizi doctrine za kulazimisha ambazo makanisa zimeokota kutoka kwa mama yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali ni je, ijumaa jioni mpaka jpili asubuhi ni siku tatu!!???
Naona mnazunguka tu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenifumbua macho kwny kitu kimoja ambacho nilikua sijawah kuwaza mkuu.. ni kwel kabisa hakuna sehemu yoyote kwny biblia au maandiko inaonesha kua yle simoni wa irene alimrudishia Yesu msalaba wake baada ya kumsaidia.. kwa hyo labda kuna uwezekano mkubwa kua Yesu alikacha..

Pli wote tunaosoma biblia tunajua kutokana na maandiko kua ilikua imeandikwa ni lazima mwana wa Adam atasulubiwa.. yan hpa na maanisha kua kutokana na hya maandiko tunategemea kua ni lazima ilikua ytokee. Lakin tunaona tena katika hyo hyo maandiko kua Yesu kabla ya kusulubiwa alipanda mliman na kumuomba Mungu kua "kikombe kile kimuepuke, si kama atakavyo bali mapenz ya mungu yatimie" Hapa inaonesha dhahir kua Yesu pia alikua hatak kusulubiwa, hvyo bas pengine Mungu alisikia kilio cha mwanae mpndwa na Hakusulubiwa

"Ni mawazo yangu tu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umechanganya madesa. Yesu anazungumziwa kwenye Biblia. Quran ni Quran. Kusulubiwa kwa Yesu ni jambo ambalo Shetani hataki kabisa kukuliana nalo. Kushindwa kwa Shetani ni kutokana na kusulubiwa na kufa kwa Yesu. Hilo atapinga milele ili watu wajue bado hawajakombolewa.SHETANI ANAPINGA SANA KUWA YESU HAKUSURUBIWA NA HAKUFA. HATA KWENYE BIBLIA SHETANI ALITUMIA WATU WAKATAE HILO.


 
Mtukutu wa Nyaigela: hapa nadhani, Ni wazi kwa hesabu hiyo siku tatu zinagoma. Maana hata katika uumbaji zilihesabiwa kwa usiku na mchana siku Moja.

Sasa hapa ndipo ambapo wasabato huwa wanakataa sikuu hii kuwa zilipotoshwa, hata christmass huwa wanahesabu ule mwezi wa Sita kuwa Mariam alipotokewa na Malaika, na mimba ikatungwa, Sasa iweje aziliwe mwezi wa 12.? Alizaliwa njiti,?

Niliwahi soma gazeti Moja la dini, Kuna mchungaji aliongelea kuwa siku ya Christmass iliwahi kubadilishwa na kuletwa mwezi wa 12 mwezi ambao wapagani wa kiyahudi walikuwa wanakusanyika kuabudu jua. Ulipeleka kuleta doa katika sikukuu hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani unajua jinsi Wayahudi walivyokuwa wakihesabuWayahudu

Wayahudi wa kale hawakuhesabu siku kwa mfumo wa saa 24.
Hatuongelei masaa, tunaongelea usiku na mchana, kwa hesabu ya usiku na mchana, siku tatu zinafika, maana usiku inahesabika siku 1 vivyo hivyo na mchana siku 1. Hapa alikuwa sahihi na zilitimia.

Maana Biblia haijawahi taja masaa, Ila inataja muda, Yaani inasema asubuhi, mchana, adhuhuri, alasiri, jioni. Au usiku nakadharika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
Mkuu, sielewi unafeli wapi. Kama utakuwa umenielewa vizuri, ebu niambie, siku ya Ijumaa kwa kanuni za Wayahudi ilianza muda gani?

Pia je Cleopas alisema uwongo kwamba siku ya tatu ilikuwa imetimia tangu Masiha alipofariki?
Rejea Luka 24:20-21

Tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.

21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
 
Pole!
Luka 22:59
Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.

Ufunuo 8:1
Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.

Matendo 19:34
Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa kama saa mbili, wakisema, Artemi wa Waefeso ni mkuu.
 
Hebu tuthibitishie Yona alikaa katika tumbo la nyangumi masaa 72
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole wewe kwanza!

Tofautisha kitu kinachoitwa "period of time" na "time"

Mimi naongelea "time" kwa maana kwamba haisemi saa Saba na dakika tisa kilifanyika hiki. Yenyewe imetumia period of time.

Mifano hiyo hapo juu, yote inazungumzia period of time, Mkuu. Kwa maneno mengine inazungumzia kitambo Cha muda ambao Jambo Fulani lilifanyika.

Hapo utanielewa naamini, walilima shamba kwa masaa yapata mawili. Hapa unaelewa kuwa shamba lililimwa kwa muda wa masaa mawili, Ila huwezi jua saa walipo anza na kumaliza.

Ubarikiwe na bwana,



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masaa ya kiyahudi hayakuhesabiwa hivyo unavyohesabu wewe siku iliisha jua lilipotua/kuzama inamaan ijumaa ilikuwa siku ya kwanza ilipofika kumi n mbili jion ikabadilika n kuwa siku ya pili ambayo ilienda hadi jumamosi jioni ikabadilika n kuwa siku ya tatu alfajiri ndo akafufuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni fumbo la muda.
Naona tunachanganyana tu jinsi ya wazee wetu wa kale walivyokua wakihesabu masaa na enzi zetu hizi za masaa 24.

Wengi wetu humu enzi za utoto tulikua tunajua siku inaanza asubuhi na sio saa sita usiku. Baada ya kupata maarifa shuleni ndipo tukajua aah kumbe.! hapo ni baada ya kufunzwa masaa na kalenda za ulimwengu.

Sasa tukirudi kwa wayahudi wa kale kuzama kwa jua kwao ndio ilikua mwisho wa siku (kama wengi tulivyojua utotoni).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…