Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Uliwahi kufiwa? Kama ndio matanga kwenu siku ngapi? 3 au 4? Tuambie mnavyozihesabu hizo siku

Pili hakunaga siku Mona na robo hizo Ni siku mbili Wala Hakuna siku mbili na nusu hizo Ni tatu.

Lakini pia tunafanya kumbukumbu la Kristu mfufuka, na kumbuka kalenda iliyokua inatumika wakati ule sio sawa na kalenda ya Leo (Gregorian calendar).

Hivyo sionibhoja kwenye bandiko lako zaidi ya mapovu ya ommo pasipo na msingi work.

Kanisa Ni moja Takatifu Katoliki la Mitume lililoanzishwa na Kristu mwenyewe.
Argument ya chini mno!
Kwa hiyo Mkuu tupuuze alicho kisema Yesu kuwa atakaa kaburini Siku tatu usiku na mchana ( three days and tree nights) na tufuate jinsi tunavyohesabu matanga? Kumbuka ukisoma Mathayo 12:38 Mafarisayo walitaka ishara kutoka kwa Yesu , naye akawapa ishara ili ikitimia wamwamini na isipotimia wasimwamini. Soma neno acha kufuata mkumbo
 
Yaani

Yaani hoja yako Ni ipi maana azimisho la pasaka Ni kumbukumbu tu. Sawa na wewe unaanzimisha birthday yako unataka siku hiyo mama yako apate uchungu Kama vile anakuzaa Mara ya pili.
 
Yaani
Yaani hoja yako Ni ipi maana azimisho la pasaka Ni kumbukumbu tu. Sawa na wewe unaanzimisha birthday yako unataka siku hiyo mama yako apate uchungu Kama vile anakuzaa Mara ya pili.
Mkuu hoja yangu ni kuwa hakuna sehemu inayothibitisha kuwa Yesu alizikwa siku ya Ijumaa, hivyo ijumaa kuu ni batili, ni ya kipagani zaidi kwa kuwa hakuna andiko linalokubaliana na hiyo siku
 
tatizo la watu wakishaelimika wanaanza kupekenyua sasa...yani ndio mana mzungu Katufichia mambo kwenye ELIMU na kaamua kuweka Gharama ili kuipata maana alijua kama ELIMU ikiwa rahisi rahisi watu wakielimika Itakua tatizo.

Mi nadhani MUNGU huko alipo anatakiwa aingilie kati kama alivyoingilia swala la mnara wa babeli...Avuruge huku chini la sivyo watu watapekechua na wajue hadi Alipo MUNGU..we ngojea.
 
mkuu hutaki tufike kwa Mungu
 
Mkuu nikusaidie kwanza hakukaa kaburini robo siku ya ijumaa kwa sababu alizikwa jioni

Mathayo 27:57 Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, 60na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake

Kwa hesabu zako bado hatupati siku tatu mchana na usiku
Mathew12:40 For just as Jonah was three days and three nights in the belly of the great fish, so will the Son of Man be three days and three nights in the heart of the earth.

Kaburi maana yake ni sehemu anayolazwa,Kuwekwa mtu anayekufa. Hata msalaba ni kaburi.

Kwa hesabu za masaa ya siku hizi.hatuwezi sema alikaa kaburini kwa siku tatu mchana na usiku. Ila kwa muktadha wa siku kama siku tunasema alikaa siku tatu kaburini. Yaani aliuawa ijumaa, Akapumzika Jumamosi na siku ya juma pili alifufuka.
 
Mkuu hoja yangu ni kuwa hakuna sehemu inayothibitisha kuwa Yesu alizikwa siku ya Ijumaa, hivyo ijumaa kuu ni batili, ni ya kipagani zaidi kwa kuwa hakuna andiko linalokubaliana na hiyo siku

Mark 15:42-47 (NIV)
The Burial of Jesus
42 It was Preparation Day (that is, the day before the Sabbath). So as evening approached, 43 Joseph of Arimathea, a prominent member of the Council, who was himself waiting for the kingdom of God, went boldly to Pilate and asked for Jesus’ body. 44 Pilate was surprised to hear that he was already dead

Mkuu Mtukutu wa Nyaigela jitahidi kusoma Maandiko maana yako wazi.
Yesu alisulubiwa na kufa muda kidogo kabla ya jioni (siku ya Matayarisho/Maandalizi ya Wayahudi = Siku ya Ijumaa), siku moja kabla ya Sabato (Jumamosi).
Joseph wa Arimathea alimzika Yesu mapema kidogo kabla ya Sabato kuingia (Ijumaa jioni kabla ya saa 12) maana Sabato ikishaingia hamna kufanya kazi yoyote.
 
Alikufa ijumaa hiyo ni siku ya kwanza

Akakaa kaburini jumamosi siku ya pili

Akafufuka juma pili siku ya tatu
 
Ijumaa ni siku
Jumamosi ni siku
na Jumapili ni siku ambayo ilikuwa ndiyo siku ya kwanza ya Juma.

Sasa piga hesabu ngapi hapo
...
 
Mkuu hoja yangu ni kuwa hakuna sehemu inayothibitisha kuwa Yesu alizikwa siku ya Ijumaa, hivyo ijumaa kuu ni batili, ni ya kipagani zaidi kwa kuwa hakuna andiko linalokubaliana na hiyo siku
well said.
Na hakuna bishara iliyokamilika kuhusiano na tukio. Tuache mbembwe.
 
The fact ni kwamba Biblia tunayojengea hoja ni hii hii ambayo kwa Karne takriban 18 hakuna mwananchi wa kawaida aliruhusiwa kuishika na aidha kuihoji. Ni Maaskofu, mapadri na wachungaji tuu walioruhusiwa kuishika na kuihubiri.
Sasa kwa kipindi chote hicho hatujui ni machapisho mangapi yamewekwa na au kuachwa na au kubadilishwa maana ili kupindisha ukweli au kuaminisha watu vinginevyo.
Nijuavyo, wayahudi wengi ni watu walio mbali na Mungu - hadi leo. Ndiyo maana hata wakati huo Paulo alijifanya Myahudi ili kuwapata wayahudi ilhali yy ni Mrumi wa kuzaliwa. Watashindwa kweli kuichakachua Biblia?.

Mwenye kudhani Biblia ipo sahihi anyooshe mkono!
 
Ijumaa ni siku
Jumamosi ni siku
na Jumapili ni siku ambayo ilikuwa ndiyo siku ya kwanza ya Juma.

Sasa piga hesabu ngapi hapo
...
Mkuu unalazimisha mbona. Yesu alisema atakaa kaburini siku tatu mchana na usiku , hiyo ni kiswahili. Kwa kiingereza alisema three days and three ninghts. Sasa piga hesabu zako mkuu kama unajua hata hesabu ya darasa la KWANZA
 
Mkuu, ukihesabu 'siku' in terms of a time period utakuwa umeharibu. Wayahudi wakishaona jua limezama na nyota tatu... zimetamalaki angani basi kitendo hicho kilihesabiwa kuwa ni mwanzo wa siku nyingine hivyo ikiwa Yesu labda angefufuka siku ya Jumapili saa 10 alfajiri au siku ya Jumapili saa 6 mchana still bado ingehesabika kuwa ni siku ya tatu.

Ebu soma Kitabu cha Esta 4:16 Vs Esta 5:1 kisha leta mrejesho hapa kunako Jukwaa.
Kama Wayahudi wangekuwa wanahesabu siku kama tunavyohesabu sisi, Esta angekwenda kumuona Mfalme siku ya nne na siyo siku ya tatu.
Nimekuelewa nimesoma mahali kuwa wayahudi walikuwa wakichukulia hata sehemu ya siku kuwa ni siku kamili....so jumapili asubuhi ilikuwa ni sehemu ya siku ya tatu, kwao walihesabu kama siku ya tatu kamili!
 
Hivi kuna sehemu imesemwa muda aliofufuka? Tusaidie tafadhali
 
Nimekuelewa nimesoma mahali kuwa wayahudi walikuwa wakichukulia hata sehemu ya siku kuwa ni siku kamili....so jumapili asubuhi ilikuwa ni sehemu ya siku ya tatu, kwao walihesabu kama siku ya tatu kamili!

Shida yetu huwa tunachangia bila kusoma maandiko:
Hebu turejee kwenye maandiko kitabu Cha Esta sura ya 4 mstari wa 16:

16 “Uende, ukusanye Wayahudi wote wenye kuwa Shushani* na mufunge+ kwa ajili yangu. Musikule wala kunywa kwa siku tatu (3),+ usiku na mchana.

Kulingana na wayahudi siku huanza jua linapozama:
usiku/mchana = siku ya kwanza
usiku/mchana = siku ya pili
Usiku/mchana = siku ya tatu.
Na kwa andiko hili walianza kufunga usiku. Mchana wa siku ya tatu (Esta 5:Esta akiwaa bado amefunga alienda kwa mfalme. Na akamuomba ahudhurie kwenye karamu siku itakayofuata. Uelewa wangu.

Tuje kwenye Bishara ya Yesu:
"Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku".

NB: Tofautisha kati ya usiku na mchana na mchana na usiku.

(i)Tuchukulie ijumaa.
Mchana wa ujumaa/usiku wa jumamosi = siku 1
mchana wa jumamosi/usiku wa jumapili = siku 2
NB: unakosekana mchana wa jumapili/usiku wa jumatatu. Na Pia hatuwezi kuiweka ijumaa yote kama siku kwa vile haikuwa desturi ya walivyokuwa wanahesabu wayahudi.
Proof: Void.
(ii) Tuchukulie kwa hesabu ya kiyahudi
usiku wa jumamosi/mchana wa jumamosi = siku 1
usiku wa jumapili/mchana wa jumapili = siku 2: Hapa mchana wa jumapili unakosekana.
Proof: Void.

Hence the whole scenario is void and dubious!
Nabii wa Mungu hawezi kuwa Muongo!!!
 
Je Yesu alikufa siku tatu kama alivyojitabiria au siku tatu (masaa 72) hazikufika au hakumaanisha siku tatu kamili? ( siku tatu za Yesu zilikuwa za masaa 72?)
Mathayo 12: 40 '' Kwa maana kama vile Yona+ alivyokuwa katika tumbo la yule samaki mkubwa siku tatu mchana na usiku, ndivyo Mwana wa binadamu+ atakavyokuwa katika moyo wa dunia+ siku tatu mchana na usiku'' (Mathew 12:40For as Jonah was three days and three nights in the belly of a huge fish, so the Son of Man will be three days and three nights in the heart of the earth.)
Kumbuka hili ni jibu la Yesu wakati akitaka kuwathibitishia mafarisayo na walimu waliotaka ishara kutoka kwake Mathayo12.38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” . Hivyo akatumia mfano wa Yohana kwa kuwaambia atakaa chini ya moyo wa ardhi kama alivyokaa Yona kwa siku tatu. Kwa hiyo hii ilibaki mioyoni mwao kama kipimo cha ukweli wake. Angefufuka kabla siku hizo tatu hazijafika mafarisayo wasingemuelewa. Wangemuita muongo na hakutoka kwa Mungu.

Kuna waalimu hufundisha kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa na wanaiita Ijumaa kuu ( Good Friday) na akafufuka Jumapili asubuhi na mapema.Je kuna ukweli hapo? Tukiamini kwamba Yesu alikufa Ijumaa mchana na akazikwa jioni kabla ya Sabato na kufufuka Jumapili asubuhi sana, Je siku Tatu zilitimia?
Kwa hesabu hizi alilala ijumaa usiku, akashinda jumamosi mchana na jumamosi usiku.
Je hizo ni siku tatu mchana na usiku kwa maana ya three days and three nights.

Wajuzi wa mambo tuelimishane hii ipoje
Kitu pekee ambacho hujajiuliza ni yona alimezwa saa ngapi? Siku ya kwanza na alitapikwa saa ngapi za siku hiyo ya 3.

Katafute kwanza muda ya tukio la kumezwa na tukio la kutapikwa zen urudi hapa tujadiri
 
Utaratibu wa Wayahudi ktk kuhesabu siku enzi zile, haukuwa sawa na huu wa kwetu - mfumo wa saa 24.
Siku ya Ijumaa ilianza siku ya Alhamis jioni baada ya jua kushuka - siku ya kwanza
Siku ya Jumamosi ilianza siku ya Ijumaa jioni baada ya jua kushuka - siku ya pili
Siku ya Jumapili ilianza siku ya Jumamosi jioni baada ya jua kushuka - siku ya tatu.
Good reasoning
 
Back
Top Bottom