Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Mkuu hujanielewa pamoja na utukutu wangu. Nilichokisema huu utaratibu wa kuhesabu masaa kuanzia saa sita usiku haukuwepo wakati Yesu akisulibiwa. Ulikuja baadaye.

Hivi kwenye maandiko kuna sehemu biblia inasema Yesu alizikwa Ijumaa? Nionesheni neno "Ijumaa" kwenye biblia na mnioneshe neno "Jumamosi".
 
Na hii hesabu ndio inayotuletea mvurugano huku kwetu kwenye dunia ya sasa.

Ndio maana wanasema kuwa siku ya kwanza ya juma (Jumapili) Yesu alifufuka katika wafu...na hii ndio sababu ya wakristo wote ulimwenguni kusali siku ya kwanza ya juma ambayo ni Jumapili
 
Kwa hesabu za zamani:
Ijumaa siku ya kwanza....jua likizama moja imekwenda hiyo....
Jumamosi siku ya pili...jua likizama mbili imekwenda hiyo...
Jumapili siku ya tatu....
Ref.Kwa kalenda ya mfalme Augusto
 
Kwani Jonah alikufa alipokuwa tumboni mwa samaki?
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
Kwani nyie SDAs mnaamini kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alifufuka siku gani?
 
.......inawezekana pia kwa hesabu za kipindi hicho jumapili ikawa sio siku ya kwanza ya juma!

muhimu ni kwamba alikufa na alifufuka, mengine hayo ni kuchanganyana, kwa sababu hii ya kusema alikufa ijumaa na jumapili akafufuka inapingana kabisa na unabii wa Yona.......

kwakua tunatakiwa kuamini zaidi unabii kuliko hesabu za wanadamu, basi yatupasa pia tuamini hakufa ijumaa na kufufuka jumapili kama wana mapokeo wanavyodai....
 
Kwa hesabu za zamani:
Ijumaa siku ya kwanza....jua likizama moja imekwenda hiyo....
Jumamosi siku ya pili...jua likizama mbili imekwenda hiyo...
Jumapili siku ya tatu....
Ref.Kwa kalenda ya mfalme Augusto
ukihesabu hivi unapingana na unabii wa Yona kukaa tumboni mwa nyangumi siku 3 usiku na mchana!

maana ili unabii uonekane kwamba umetimia ni jambo litendeke vile vile kama lilivyotabiriwa
 
ukihesabu hivi unapingana na unabii wa Yona kukaa tumboni mwa nyangumi siku 3 usiku na mchana!

maana ili unabii uonekane kwamba umetimia ni jambo litendeke vile vile kama lilivyotabiriwa
Hata yule nyoka wa shaba ni unabii pia....pia Isaka kumtoa mwanae nao ni unabii.
 
Unahoja usikilizwe
 
N kweli mkuu walikuwa wanahesabu kwa utaratibu kwamba jua likizama siku inaisha na nyingine inaanza.Kwa hiyo kama alizikwa Ijumaa jioni na kufufuka jumapili asubuhi siku tatu hazifiki
Ni siku tatu kwa majira Yao Acha kujifanya mtafiti, we vipi.

Kwahiyo unataka kusema watu wanaosema miaka 2000 iliyopita zamani yesu alishuka kuzimu mpaka Leo ni elfu mbili ?

Tunazungumza nyakati za biblia sio za dot com
 
Umeweka maelezo mazuri sana
 
Hata yule nyoka wa shaba ni unabii pia....pia Isaka kumtoa mwanae nao ni unabii.
na ulitimia,
nyoka wa shaba kuinuliwa ni Yesu alipoinuliwa,..

Ibrahimu kumtoa mtoto wake wa pekee ulitimia kwa Mungu kumtoa Yesu
 
Ni siku tatu kwa majira Yao Acha kujifanya mtafiti, we vipi.

Kwahiyo unataka kusema watu wanaosema miaka 2000 iliyopita zamani yesu alishuka kuzimu mpaka Leo ni elfu mbili ?

Tunazungumza nyakati za biblia sio za dot com
three days, three nights
labda niandike kiingireza ndo utajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…