Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Kwanini yesu anaitwa mwana??
Inamana kuna mama mbinguni??
Kuitwa Mwana haimaanishi lazima kuwe na mama huko mbinguni.

Kwa mfano, kiongozi anapoitwa Baba wa Taifa haimaanishi taifa lina mama wa kuzaa, ni lugha ya heshima kueleza uongozi. Vivyo hivyo, Yesu kuitwa Mwana wa Mungu haithibitishi kuwepo kwa Mama wa Mungu. Ni ishara ya nafasi yake maalum, si uhusiano wa uzazi halisi.

Samia anaitwa Mama na sisi anatuita watoto wake, Je baba yuko wapi?
Huu ndiyo mfano wa swali ulilouliza.

Kuzaliwa kunamaanisha mwanzo.
Mungu wa kweli hana mwanzo (Yeye ndiye chanzo cha kila kitu).
Kwa hiyo, kuitwa “mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote” - Wakolosai 1:15 ni ushahidi kuwa Yesu si Mungu asili, bali ni kiumbe wa kwanza, mkuu juu ya viumbe, lakini si Muumba mwenyewe.

Mungu hazaliwi wala haumbiwi — Yuko daima - Zaburi 90:2.

Yesu alizaliwa – Luka 2:7, Mathayo 1:18-25.

Yesu alikua na akaomba kwa Mungu – Luka 6:12, Mathayo 26:39.

Yesu alisema Baba ni mkuu kuliko yeye – Yohana 14:28.

Hata baada ya kupaa, Yesu bado anaenda kukaa kwa Mungu wake – Ufunuo 3:12.

Kwa hiyo, kama Yesu ana Mungu wake, anazaliwa, ana mwanzo, na anatii mamlaka ya juu, hawezi kuwa Mungu wa milele aliye juu ya vyote.
 
Kwanini yesu anaitwa mwana??
Inamana kuna mama mbinguni??
Kwanini unafikiri Yesu kuitwa Mwana lazima kumaanishe kuna mama?
- Je, unataka kusema Mungu ana jinsia na uzazi wa kimwili?
Hiyo si imani ya kiroho bali ya kibinadamu.


Kwa nini unampunguzia Mungu uwezo hadi kufikiri ana mke wa kuzaa naye?
- Mungu si kiumbe wa mwili kama sisi. Mungu ni Roho.
-Huko kufikiri mama mbinguni ni kutukana mamlaka na utukufu wake.


Unaposema Yesu ni Mwana, huwa unamaanisha nini?
-Mzaliwa? Basi ana mwanzo.
-Kiumbe? Basi si Mungu.
-Au ni mfano wa uhusiano? Basi hoja ya mama inajivunjilia hapo.


Kama Mungu anaitwa Baba, je, hilo ni jina la kijinsia au ni mfano wa mamlaka?
-Kama ni mfano wa mamlaka (kama vile Baba wa Taifa), kwa nini unatafuta mama wa mamlaka?
Huoni unakufuru?


Ukitaka mama wa Yesu, si alizaliwa na Mariamu hapa duniani?
-Kwa nini unalazimisha awepo mwingine mbinguni?
Biblia haijawahi kutaja Mama wa Mungu wa milele – ni mafundisho ya baadaye yasiyo na msingi wa kimantiki wala kimaandiko.


Unaposema Yesu ni Mungu na bado amezaliwa, umevunja sifa kuu ya Mungu kuwa hana mwanzo.
-Je, kuanzia sasa Mungu ana mwanzo?
-Hilo ni tusi la dhati kwa Mungu.
-Mungu haumbwi, hazaliwi, hasali, hafufuki.


Kama unadai Yesu ni Mwana wa Mungu na ni Mungu mwenyewe basi eleza:

Alizaliwa lini?

Kwa mama gani?

Kwanini hakuwepo kabla ya kuzaliwa?

Kwanini anaomba kwa Mungu kama Yeye ni Mungu?

Na kama huwezi kuyajibu hayo bila kuharibu sifa ya Mungu wa kweli basi unapaswa kukiri kwamba Yesu ni mjumbe wa Mungu ana uungu lakini si mweza yote, mzaliwa kwa kusudi, lakini si Mungu mwenyewe
 
Trinity = Devil's doctrine to confuse the very elect.
No where in the scriptures you will find any of the Apostles including Jesus Christ himself teach of the trinity.

God is one.
His soul is one.
There is none other reigning beside him.

Jesus is the Father.
Flesh & Blood born by Marry was called son.
Holy Spirit is the spirit of God when inside of a man.

Father & Holy Spirit are the titles of God. Son is not God (for God is spirit) but spirit in Son was God.

Father, Son & Holy Spirit share the same name YHWSH (in Hebrew), Jesus in English, Yesu in Swahili.
 
Sasa kama Yesu ni Mungu na Baba ni Mungu je kuna Mungu wangapi?
Sikia, Ee Israeli: Bwana, Mungu wetu, ni Bwana mmoja - Kumbukumbu la Torati 6:4

Mimi ni Bwana, wala hakuna mwingine; zaidi yangu mimi hakuna Mungu. - Isaya 45:5

Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa kweli peke yako, na Yesu Kristo uliyemtuma. - Yohana 17:3

Mungu wa kweli ni Mmoja tu, si wawili, si watatu, si sehemu tofauti. Yeye ndiye Chanzo cha kila kitu, hana mwanzo, hana mwisho, na hafanani na chochote kilichoumbwa.

Halafu Yesu ni wa kipekee kwa sababu alitoka kwa Mungu huyu mmoja, si Mungu mwingine

Yesu alijazwa na Roho, hekima, na mamlaka ya Mungu. Ana uungu kwa maana ya kuwa na asili ya kiroho kutoka kwa Mungu, lakini si Mungu wa pili wala wa tatu.

Yesu ana uungu kwa sababu alitoka kwa Mungu moja kwa moja, akashiriki kuumba, na akajazwa Roho wa Mungu kikamilifu.

Anaitwa Mungu kwa kazi na utukufu aliopewa, lakini si Mwenyezi Mungu mwenye mamlaka yote.

Yeye ni Mwana wa Mungu, si Mungu wa milele aliye chanzo cha kila kitu.

Kumuita Yesu Mungu kunahitaji uelewa wa hali ya juu ili usimfanye mweza yote.

Kwa mtu kama mimi natambia Mtoto wa Nyoka ni nyoka ila kamwe hawezi kuwa baba.

Mtoto wa binadamu ni binafamu lakini kamwe hawezi kuwa baba wa ye mwenyewe.

Labda utajiuliza mbona nasisi binadamu ni wana wa Mungu, Je, nasisi tuna uungu?

Hapana. Binadamu hatuna uungu kwa asili.
Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26), lakini hatushiriki uungu, bali tunabeba pumzi ya Mungu.

Yesu alitoka kwa Mungu moja kwa moja na alijazwa uungu kikamilifu.

Binadamu tunatoka kwa udongo tuna roho ya uhai, si ya uungu.
 

Sasa kama unasema kuwa Yesu ni Mungu kwa sababu kajazwa Uungu, na kisha kama unasema BABA ni Mungu kwa uasili, Sasa hapo kuna Mungu wangapi?.
 
AKUNA MUNGU NUSU.YESU NI MUNGU KWELI NA MTU KWELI
 
God is one.
Jesus is not the Father, but the Son filled with God’s Spirit.
He has divine power, but He is not the Almighty God Himself.

If the Father, Son, and Holy Spirit are truly three separate persons, why did Jesus say in the name — singular — instead of in the names to show that they are in the same mission?

If Jesus is the Father, why did He pray to the Father and call Him greater than Himself?

Can the true God die, sleep, or be born — like Jesus did?
 
Sasa kama unasema kuwa Yesu ni Mungu kwa sababu kajazwa Uungu, na kisha kama unasema BABA ni Mungu kwa uasili, Sasa hapo kuna Mungu wangapi?.
Eti mkuu Mungu mkuu mwenye nguvu na yule aliyejazwa nguvu na Mungu mkuu nani Mungu wa kweli?

Baba na mtoto wote ni binadamu kamili lakini nani ni baba?
Si yule mwenye nguvu aliyemleta huyu mwana duniani.

Kuna Mungu mmoja wa pekee wa kweli - Baba.
 
Mungu ni Mkuu Sana na mambo yake hayachunguziki na anaweza kufanya lolote na wakati wowote.

Hatuwezi kumsoma Mungu lakini Yeye mwenyewe anaweza kujidhihirisha kwetu kwa namna yeyote anayotaka Yeye kujidhihirisha. Tunavyowaza sisi sivyo Yeye Mungu anavyowaza.

Kuna mambo mengi Mungu ameyafanya na bado hatujayajua na huwenda tusiyajue kabisa.

Anachohitaji Yeye, ni sisi kumcha Yeye na kufuata yale anayotaka tufanye na Mwisho twende kwake Mbinguni tukae pamoja nae milele, Amina.
 
Uzuri Mungu hakuficha uso wake ili tusimjue, alijifunua kupitia Yesu.
Kumjua Mungu ni neema, kumcha ni hekima, lakini kumpokea Yesu ni uzima wa milele.

Baraka na neema ya kweli iwe juu yako pia, mtumishi wa Mungu.
Tuko pamoja katika ukweli.
Amen.
 
Eti mkuu Mungu mkuu mwenye nguvu na yule aliyejazwa nguvu na Mungu mkuu nani Mungu wa kweli?

Baba na mtoto wote ni binadamu kamili lakini nani ni baba?
Si yule mwenye nguvu aliyemleta huyu mwana duniani.

Kuna Mungu mmoja wa pekee wa kweli - Baba.

Naam Hata Yesu mwenyewe alisema wazi kuwa Mungu wa kweli na wa pekee ni BABA. Kauli ya Yesu ya "Wakujue wewe Mungu wa kweli na wa pekee, na Yesu Kristo uliyemtuma", inamaliza utata. Sasa nashangaa wale wanaotumia thinking yao, falsafa zao kumuelezea Mungu, wakati Yesu keshawaambia kuwa BABA ndiye Mungu wa kweli na wa pekee!

Sasa hao wanaodai Mwana naye ni Mungu sijui hilo andiko wanalipata wapi?. Sana
 
Yesu hakukiri kutokujua kabisa?
Kivipi?
Fafanua.
enedelea mpaka 40-44.

hapa Yesu anaonyesha dhamira halisi ya kutoitaja siku hiyo,kumbuka atakayetakiwa kuja ni yeye huyo huyo anayejizungumzia kama mfumanizi.

ingekosa maana kabisa kuitaja siku husika,maana watu wangejiandaa wakati wanaikaribia.
 
God is one.
Jesus is not the Father, but the Son filled with God’s Spirit.
He has divine power, but He is not the Almighty God Himself.

Jesus (flesh and blood was not the Father) but Jesus (spirit) was the Father, for God is the spirit (John 4:24). Thus when saints say Jesus is Almighty God "the Father"; they refer to the Spirit inside the son/flesh and blood and when they say Jesus is son of God; they refer to the flesh and blood.


If the Father, Son, and Holy Spirit are truly three separate persons, why did Jesus say in the name — singular — instead of in the names to show that they are in the same mission?

Father and Holy Spirit are the same thing. Son was just a vessel (flesh and blood) for Father to manifest to manking without causing havoc (Exodus 33:20, John 1:18).

Now can you tell the name of the Father, and of the Son and of the Holy Spirit according to scriptures?

If Jesus is the Father, why did He pray to the Father and call Him greater than Himself?

Jesus (flesh and blood) pray to the Father (the spirit) purposely to teach his disciples a proper way of praying. Because the (flesh and blood) mission was to teach the way of doing things including prayer life in God's (spririt) way. Jesus (spirit) healed, commanded (John 13:34) and forgave sins (Matthew 9:2)

Can the true God die, sleep, or be born — like Jesus did?

Jesus (flesh and blood) carried all characteristics of a being including be born, sleep, die; and Jesus (spirit) carried all characters of Almighty God including healing, rising the dead, forgiving sins etc.

NB:
As a truth seeker you should understand the Mystery of the Godliness of God (1 Timothy 3:16).

God "the Father" = Creator of All Creation
Son = Manifestation of God "the Father" to the beings.
Holy Spirit = God "the Father when he is within his saints.

Even now; if you have God "the Father" within you, automatically you become the son/daughter of God (Romans 8:9-17, Galatians 3:26).

You also better understand that, the kingdom of God "the Father" will only be entered by the children of God. People whom God is within them.

The Glory and Peace of God be upon you and may the Spirit of truth guide you towards enlightenment. Amen!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…