Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Yesu ni Mungu, Whats your point? Kama Mungu ana mamlaka, and so Yesu, Hana Makubwa zaidi maana He is the same!
 
Ngoja na mimi nitengeneze assumptions kuhusu Holly Trinity.
kwamba Mungu-Yesu aliyekuja kuishi duniani ilikuwa hard copy ya Mungu...soft copy ilisalia kulekule Mbinguni ambae ni ndiye MUNGU mkuu...

Kwahiyo UUNGU ni kama nakala 3 katika barua/document ileile..

Hardcopy ndio ule mwili uliokuja duniani na kuzaliwa na Mariam.....mwili ule uliishi kama binadamu, ulionwa live na binadamu...mwili ukamaliza kazi yake ukarejea kwenye mbinguni kwny kivuli kikuu.

Wakati Hardcopy ikiwa Duniani, Soft copy ilibaki mbinguni iki-operate shughuli zote kama Mungu mkuu.....
Soft copy ndie MUNGU MKUU asiyeonekana na wala hata hataonekana..

Holy spirit ni image/copy nyingine ya Mungu yuleyule iliyotumiwa kwa assignment maalumu..

Kwahiyo hapa tunahangaika na nakala za yuleyule.....
 
Sawa - lete andiko ili twende sawa.
Matendo ya Mitume 13:2
[2]Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
As they ministered to the Lord, and fasted, the Holy Ghost said, Separate me Barnabas and Saul for the work whereunto I have called them.

Matendo ya Mitume 16:6
[6]Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
Now when they had gone throughout Phrygia and the region of Galatia, and were forbidden of the Holy Ghost to preach the word in Asia,

Energy/power/etc can not speak..Kama ROHO Mtakatifu asingekuwa NAFSI asingeongea au kuonya
 
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.
Mwanzo 1:26
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.”

Mungu akasema na si Mungu wakasema; Mungu ni Roho moja tu yenye nafsi tatu; hana mwili



GOD.png
 
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:


1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.


2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.


3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.


4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.



5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.


6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.


7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.



8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.


9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.



10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu


11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)


✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.


🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
By the way; kuna tofauti gani kati ya majukumu na mamlaka?
 
Matendo ya Mitume 13:2
[2]Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
As they ministered to the Lord, and fasted, the Holy Ghost said, Separate me Barnabas and Saul for the work whereunto I have called them.

Matendo ya Mitume 16:6
[6]Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.
Now when they had gone throughout Phrygia and the region of Galatia, and were forbidden of the Holy Ghost to preach the word in Asia,

Energy/power/etc can not speak..Kama ROHO Mtakatifu asingekuwa NAFSI asingeongea au kuonya
Voice of God through the power of God!!
 
By the way; kuna tofauti gani kati ya majukumu na mamlaka?
Majukumu ni kazi au mambo unayopaswa kufanya.

Mamlaka ni uwezo au nguvu ya kuamuru au kusimamia kazi hizo.

Majukumu ni mfumo wa kikazi, mamlaka ni nguvu za kuongoza kazi hiyo.
 
Majukumu ni kazi au mambo unayopaswa kufanya.

Mamlaka ni uwezo au nguvu ya kuamuru au kusimamia kazi hizo.

Majukumu ni mfumo wa kikazi, mamlaka ni nguvu za kuongoza kazi hiyo.
SASA KAMA UNAELEWA HIVI, KWA NINI USEME MAJUKUMU SI MAMLAKA WAKATI HUWEZI UKAWA NA KIMOJAWAPO BILA KUWA NA KINGINE? UNAWEZAJE KUSEMA JICHO SIYO MWILI WAKATI JICHO NI SEHEMU YA MWILI, NA HIVYO JICHO NI MWILI PIA?

INAONYESHA UNAJUA MAANA YA MAMLAKA, NA PIA UNAJUA MAANA YA MAJUKUMU ISIPOKUWA TITLE ULIYOWEKA KWENYE POST YAKO, HAIKO SAHIHI KUTOKANA NA UKWELI KUWA INAPINGANA NA KILE UNACHOKIFAHAMU KUHUSIANA NA NYANJA HIZI MBILI.

NYANJA HIZI ZIKO RELATED IN SUCH A WAY THAT ONE IS A SUBSET OF THE OTHER NA HIVYO IS IMPOSSIBLE TO HAVE ONE WITHOUT THE OTHER KWA MAANA KUWA HUWEZI UKAWA NA MAJUKUMU HALAFU UKAKOSA MAMLAKA AND THE VICE VERSA IS TRUE

REKEBISHA HEADING YAKO HAINA MANTIKI
 
QURAN 5: 116-119

116
. Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa mwana wa Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Wewe umetakasika! Haiwezekani mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi wa yaliyo fichikana.

117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye ulikuwa Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu.

118. Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hekima.

119. Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa.


 
Huwezi kuonaaa

Yohana 14:16-19
[16]Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

[17]ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

[18]Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
ISijaona mahala Yesu amesema yeye ni Roho kama ulivuodai bali alisema atamuacha roho kama msaidizi.
Yesu atakuwaje roho wakati roho ndiyo anakaa n
Yesu ni Mungu kwasababu ametokana na Mungu direct kwani ni sawa na wewe ni Binadamu sababu una DNA za ubinadamu lakini wewe ni sawa na baba yako mzazi?

Lakini hilo halimfanyi awe Mungu wa pekee wa kweli thats why akasema "Wakujue Mungu wa pekee wa kweli" kwamba yeye pia anajijua ana Uungu ila siyo sawa na babaye.
Yesu ndie huyo baba mzazi unaedhani kuna mwingine
 
Mungu ananafsi moja tuu . Isaya 45:15
Mwanzo 1:26
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.”

Mungu akasema na si Mungu wakasema; Mungu ni Roho moja tu yenye nafsi tatu; hana mwili



View attachment 3398232
F
 
Back
Top Bottom