Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Mungu yupo kwa asilimia 100 - Mambo yaliyonitokea ni uthibitisho tosha.

Siyo hadithi wala kuklemishwa - Ni live bila chenga.

Kupitia maisha niliyopitia.
Thibitisha Mungu yupo, usiseme tu kuwa yupo.

Kusema tu yupo, kama hayupo, hakumfanyi awepo.

Thibitisha yupo.
 
Ukiwa na Imani umeushinda ulimwengu wala huhitaji kufanya utafiti juu ya Mungu kwa kuwa yeye ni mmoja kama vile maji yanaweza kuwa mvuke,au barafu kutokana na mazingira.Tunaweza kufananisha Mungu kama maji,Yesu kama barafu na mvuke kama Roho mtakatifu.(hii ni mifano)lakini Mungu ni yule yule mmoja.Yesu alipokuwa duniani alikuwa anatufundisha kwa tabia yake ya kutokujimwambify ndo maana wengi wanadhani alikuwa binadamu kama ss(yoh.14:8-9)
 
Thibitisha Mungu yupo, usiseme tu kuwa yupo.

Kusema tu yupo, kama hayupo, hakumfanyi awepo.

Thibitisha yupo.
Nimeshakwambia yupo kwasababu kuna jambo kubwa ambalo limenitokea mimi binafsi.

Uthibitisho ndiyo huo baada ya kumpokea Maisha yangu yamebadilika 100%.
Huo ndiyo uthibitisho wangu hakuna mwingine.

Mungu yupo, Mungu yupo, Mungu yupo.
 
Kwa hiyo hilo bandiko kwa msaada wa GPT ndio unaona ni andiko?

Mbona majibu murua wataalamu wenzangu wameshakujibu au nini kigumu

Kwa hiyo unataka na hayo majibu umuulize ndugu yako GPT hili akusaidie kupanga ?
Huna hoja, una kelele.
Kosoa kwa neno siyo maneno.

Ukitumia AI kupangilia hoja za kisiasa na uchumi hakuna tatizo ila ukitumia kupangilia masuala ya Mungu Tatizo.

Shida ya wapinzani ni kupinga kilakitu.
 
Tumia akili aliyokupa Mungu kuchakata mambo, hiyo AI ni maroboti tu ambayo wapo baadhi ya binadamu wasiomjua Mungu wa kweli wameiprogramu sasa hapo, unategemea kuja na output yenye akili.

Wewe unaonesha akili zako ni kama Artificial Intelligence (AI) maaana akili na maisha yako yamelala huko, acha ulodilofa wewe.

Shida yako wewe ni mtoto wa 2000 ndio maana akili yako ishakuwa tegemezi na AI, ushazoe kulishwa hadi keki
 
Sawa mkuu umeshinda wewe - Tumia sasa hiyo akili yako kuleta ukweli.
Wewe unaonesha akili zako ni kama Artificial Intelligence (AI) maaana akili na maisha yako yamelala huko, acha ulodilofa wewe.
Hivi unafahamu maana ya Research?
Shida yako wewe ni mtoto wa 2000 ndio maana akili yako ishakuwa tegemezi na AI, ushazoe kulishwa hadi keki
Sawa mimi ni mtoto wa elfu mbili mwenye mtoto wa miaka 20.
 
Nimeshakwambia yupo kwasababu kuna jambo kubwa ambalo limenitokea mimi binafsi.

Uthibitisho ndiyo huo baada ya kumpokea Maisha yangu yamebadilika 100%.
Huo ndiyo uthibitisho wangu hakuna mwingine.

Mungu yupo, Mungu yupo, Mungu yupo.
Habari ya jambo kukutokea wewe binafsi ni logical fallacy ya personal experoence, si uthibitisho kwamba Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:

1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.

2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.

3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.

4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.

5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.

6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.

7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.

8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.

9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.

10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu

11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)

✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.

🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
Hakuna anayeweza kusema Yesu ni bwana isipokuwa Kwa uweza wa Roho mtakatifu. Ieleweke hivyo kila wazo liheshimiwe

Hakuna anayeweza kusema Yesu ni BWANA isipokuwa Kwa uweza wa Roho mtakatifu.
 
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Yesu ndie mungu mkuu hakuna mwingine
Pamoja na maelezo yote, lakini Bado Kuna kichwa hata kutafsiri maandiko hakiwezi.
 
Hakuna anayeweza kusema Yesu ni bwana isipokuwa Kwa uweza wa Roho mtakatifu. Ieleweke hivyo kila wazo liheshimiwe
Hakuna anayeweza kusema Yesu ni BWANA isipokuwa Kwa uweza wa Roho mtakatifu.
Umeitoa wapi - Lete andiko mkuu!!
 
Back
Top Bottom