Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Mimi ninayo maelezo kamili kuhusu ukristo ....injili ni sahihi mbona hata mudi boy kakili kuhusu injili ambayo ndiyo ukristo ..tatizo lililopo ni kujua injili ya kweli isiyo chakachuliwa ambayp mimi naijua ...uislamu ndiyo upuuzi ulio dhahiri kabisa ....nimeuliza hapa jf waislamu wote maswali mnashindwa,kunijibu ...nimeuliza SHETANI IBILISI YULE ALIYE LAANIWA LAANA YA MILELE NI DINI GANI? sijajibi

Weka jibu tena mbona unaogopa ...shetani ibilisi ni dini gani
Iblisi hatukuambiwa ni wa dini gani,yeye ni muovu na yupo kwa ajili ya kuwapoteza wanadamu

Labda wewe uniambie wa dini gani na uje na udhibitisho
 
Habari zenu wakuu - Nitatoa ufafanuzi kama kichwa kinavyoeleza, Hizi hoja zote ni matokeo ya uchambuzi wangu wa kina wa biblia:

NInakubaliana na fumbo la utatu wa Mungu - Baba, Mwana na Roho lakini katika mtizamo wa kimajukumu na siyo Mamlaka.

Tuweke theology pembeni kisha tujadili neno lenyewe, Kwanini nasema Utatu ni wa majukumu na siyo mamlaka ? [Kama christians wengi wadaivyo kwamba YHWH, Yesu na RohoMtakatifu wana uwezo sawa kimamlaka], Sababu zangu ni:


1. Mungu ni Mmoja, Nafsi Moja — Sio Nafsi Tatu.
“Sikia, Ee Israeli, BWANA Mungu wetu, BWANA ni mmoja.”
(Kumbukumbu 6:4)
“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu hapana Mungu.”
(Isaya 45:5)
Mungu ni nafsi moja tu, anasema “Mimi,” si “sisi.” Hakuna viini vitatu vya Mungu.


2. Yesu ni Mungu kwa Sababu ni Mwana wa Mungu — ila si Mkuu Kama Baba.
-"Kwani kijana wa miaka 35 si mtu mzima aliyekomaa sawa tu na baba yake-Je hilo linampa nafasi ya kuwa sawa na baba yake? Bado atabaki mtoto anayepaswa kutii simple.
“Naye Neno alikuwa Mungu... naye akawa mwili...” - Yaani Yesu pia alikua ni Mungu kamili kwasababu alirithi uungu ule kwa baba yake na akaja kupitia mwili.
(Yohana 1:1,14)
“Katika yeye unakaa utimilifu wote wa uungu...” - unakaa utimilifu wa uungu - Si kwamba yeye ndiye Mungu mkuu.
(Wakolosai 2:9)
“Baba peke yake ndiwe Mungu wa kweli...”
(Yohana 17:3)
Yesu ana uungu, lakini anamtambua Baba kuwa Mkuu kuliko yeye.


3. Yesu si Baba — Wanatenda Majukumu Tofauti
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)
“Sishuki kutoka mbinguni kufanya mapenzi yangu, bali ya Yule aliyenituma.”
(Yohana 6:38)
Yesu anatenda kazi ya Baba, si Baba mwenyewe.


4. Roho Mtakatifu si Nafsi ya Mungu, Bali ni Nguvu ya Mungu.
“Roho Mtakatifu atakujilia juu...”
(Luka 1:35)
“Mtapokea nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajilia...”
(Matendo 1:8)
“Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” - Hutuombea kwa nani ikiwa watu wanaclaim Roho ni YHWH.
(Warumi 8:26)
Roho ni nguvu ya YHWH, si nafsi huru.



5. Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza — YHWH Hana Chanzo wala hazaliwi.
“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”
(Wakolosai 1:15)
“Mimi nalitoka kwa Mungu...”
(Yohana 8:42)
Yesu ni mwanzo wa ufunuo wa Mungu; Baba hana mwanzo.


6. Yesu Anafanya Kazi Maalum — Uumbaji na Ufunuo.
“Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa...”
(Wakolosai 1:16)
“Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana.”
(Wakolosai 1:15) - Amebeba sifa zote za YHWH asiyeonekana.
Yesu ni mtendaji mkuu wa Mungu, si chanzo kikuu.


7. Yesu Alijinyenyekesha — Hakujijaribu Kuwa Mkuu Kuliko Baba.
“Alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii hata mauti...”
(Wafilipi 2:6-8)
Alijua kuwa ana sifa zote za Uungu lakini alimuachia Baba mamlaka ya mwisho.



8. Yesu Hakupewa Ujuzi wa Mwisho — Baba Pekee Anajua kila kitu.
“Siku ile au saa ile hakuna ajuaye, hata malaika, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
(Marko 13:32) - Hata Mwana mwenyewe haijui siku ya mwisho bali Baba.
Majukumu tofauti - mamlaka tofauti.


9. Roho Mtakatifu ni Nguvu ya YHWH Inayotumika na Baba mwenyewe, Mwana, na Sisi kama tukikiri kwa moyo wa dhati tunashare pia.
“Pokeeni Roho Mtakatifu.”
(Yohana 20:22)
“Nitaimimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili...”
(Matendo 2:17)
“Roho wake akaaye ndani yenu...”
(Warumi 8:11)
Roho hutenda kazi ndani ya Mungu na sisi.



10. Mungu Mmoja, Nafsi Moja, Anayetenda Ndani ya Wote.
“Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote, na ndani ya yote.”
(Waefeso 4:6).
Mungu ni mmoja, na anatenda kazi zote tatu:
I. Baba kama chanzo na mkuu.
II. Kumtuma Mwana kama mtendaji na mfunuo.
III. Kuachilia Roho kama nguvu inayotenda ndani ya sisi na ulimwengu


11. Yesu ni Mungu Kamili — Anatenda kama Mungu, Lakini Hadai Usawa na Baba kwasababu Baba ni Baba.
“Umesamehewa dhambi zako.”
(Luka 5:20)
“Wewe u Mwana wa Mungu.”
(Marko 3:11)
“Mungu alikuwa katika Kristo akiupatanisha ulimwengu...”
(2 Wakorintho 5:19)

Yesu anasamehe, anatoa pepo, anapatanisha — ni kazi za Mungu ila;
“Yeye kwa asili alikuwa Mungu, lakini hakudhani kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho...”
(Wafilipi 2:6) - Alijinyenyekesha, hakutaka kuwa sawa na Mungu mkuu.
“Baba ni mkuu kuniliko mimi.”
(Yohana 14:28)


✅ Yesu ni Mungu, lakini hachukui nafasi ya Baba.
✅ Alinyenyekea, akatenda kwa mamlaka ya Baba.
✅Yesu ni Mzaliwa wa Kwanza - Mungu hazaliwi na Hana chanzo, Kama angezaliwa ilitakiwa biblia ijibu alizaliwa toka kwa nani?
✅Mwana wa Mungu = Mungu [Genetically].
Lakini Baba ni mkuu kuliko yeye.
✅Roho ni nguvu ya Mungu, inayoshirikiwa na wote — Baba, Mwana, na sisi.
✅Huu ndio Utatu wa Majukumu — si uungu wa nafsi tatu, bali kazi tatu za Mungu mmoja aliye juu ya yote.


🧠 Tufungue mjadala:
Unakubaliana au unapinga? Tufanye hoja kwa hoja - siyo hisia na mihemko kwa heshima ya maandiko ili tupate kuujua ukweli.
📖 Biblia iwe mbele, Theology nyuma.
Yawezekana wewe tayari una 40+ lakini bado haumjui Mungu wako aliyekuumba Ili umuabudu

Na ndio maana mkichinja mnyanya sisi waislam hatuli Kwa sababu nyinyi Mungu aliyewaumba hao wanyama hamumjui

Mchungaji A Mungu ni 3
Mchungaji B Mungu 1 nafsi 3
Mchungaji C Yesu Mungu mkuu
Mchungaji D Yesu Mungu mtoto
Mchungaji E Yesu sio Mungu

Jahanamu inakusubirini Kwa hamu sana
 
Iblisi hatukuambiwa ni wa dini gani,yeye ni muovu na yupo kwa ajili ya kuwapoteza wanadamu

Labda wewe uniambie wa dini gani na uje na udhibitisho
Mudi boy kamsilimisha ibilisi sasa ibilishi akisha silimishwa ni dini gani na ni swahaba wa muhammad...waislamu hata kilicho andikwa kwenye msahafu wenu amjui 😁😁😁😁
 
Mudi boy kamsilimisha ibilisi sasa ibilishi akisha silimishwa ni dini gani na ni swahaba wa muhammad...waislamu hata kilicho andikwa kwenye msahafu wenu amjui 😁😁😁😁
Tatizo lako ni moja,unajifanya unajua mambo kumbe mweupe kabisa

Niletee hicho kilichoandikwa kwamba Iblis kasilimishwa na Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wa sallamu

Usipoleta wewe ni mzushi ambaye unatakiwa kupuuzwa
 
Tatizo lako ni moja,unajifanya unajua mambo kumbe mweupe kabisa

Niletee hicho kilichoandikwa kwamba Iblis kasilimishwa na Mtume Muhammad swalla aallahu alaih wa sallamu

Usipoleta wewe ni mzushi ambaye unatakiwa kupuuzwa
Asili ya majini ukrasa wa 20
 
Ngoja nikuletee video waislamu wenzako tena mashekh awakuweza kukanusha wewe tumbili ndiyo unabisha


View: https://youtu.be/pQYuoinjbrw?si=iGnGDINxMksNWPn-

Haya maswala ya kila anaongea unamuona sheikh unafeli

Hii video sitaangalia,nataka unipe ushahidi kwamba Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kuwa alimsilimisha Iblis

Haya ndio yalikuwa mazungumzo yetu ya mwisho

Ukishindwa kuleta ushahidi nitakupuuza daima
 
Haya maswala ya kila anaongea unamuona sheikh unafeli

Hii video sitaangalia,nataka unipe ushahidi kwamba Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kuwa alimsilimisha Iblis

Haya ndio yalikuwa mazungumzo yetu ya mwisho

Ukishindwa kuleta ushahidi nitakupuuza daima
Siyo tu kumsilimisha shetani bali hadi majini aliyasilimisha na alikuwa na jini lake likimwongoza katika uislamu
 
Siyo tu kumsilimisha shetani bali hadi majini aliyasilimisha na alikuwa na jini lake likimwongoza katika uislamu
Wewe huna ushahidi,kuanzia leo sitapoteza mda wangu kujadili na wewe

Jioni njema
 
Haya maswala ya kila anaongea unamuona sheikh unafeli

Hii video sitaangalia,nataka unipe ushahidi kwamba Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kuwa alimsilimisha Iblis

Haya ndio yalikuwa mazungumzo yetu ya mwisho

Ukishindwa kuleta ushahidi nitakupuuza daima
Hapo kuna mashekh zaidi ya wa 4
 
Wewe huna ushahidi,kuanzia leo sitapoteza mda wangu kujadili na wewe

Jioni njema
Kwanini kwani ni uongo kuwa Muhammad alisilimisha hadi majini na yeye mwenyewe alikuwa anafuga jini la kiislamu alililo.kuwa linamwongoza 🙄🙄🙄
 
Mungu ni cheo ambacho kimetokea baada ya Neno kufanya uumbaji Malaika na viumbe wengine kabla uumbaji kufanyika kulikuwa hakuna Mungu kwa sababu cheo Cha Mungu kina demand ibada
MUNGU Nİ MMOJA. ILA HUJIFUNUA KULINGANA NA WAKATI NA UTENDAJI WAKE. TUNAMUOMBA MUNGU KWA JINA LA YESU ABARIKI CHAKULA LAKINI TUNAPOKULA TUNAKULA NA ROHO WAKE.
MUNGU NI UWEZO NA SIFA SIYO CHEO
 
Yawezekana wewe tayari una 40+ lakini bado haumjui Mungu wako aliyekuumba Ili umuabudu

Na ndio maana mkichinja mnyanya sisi waislam hatuli Kwa sababu nyinyi Mungu aliyewaumba hao wanyama hamumjui

Mchungaji A Mungu ni 3
Mchungaji B Mungu 1 nafsi 3
Mchungaji C Yesu Mungu mkuu
Mchungaji D Yesu Mungu mtoto
Mchungaji E Yesu sio Mungu

Jahanamu inakusubirini Kwa hamu sana
Imani inayojengwa kwa hofu - hiyo imani imekufa. Kama unaabudu sababu unaogopa Jehanum unaabudu hofu - haumuabudu Mungu.

Jehanum haipo kwa waaminio bali wasioamini.
 
jadili na huyu hamis77
Ukiona muislamu anakimbia mada na kuwakana hadi mashekh wake ujue umembana ...hao mashekh zaidi ya wanne tena wasio wa bakwata kawakana kuwa siyo mashekh....ametaka sura nimemuwekea kuwa ni sura ya majini 20 sasaxanataka nini
 
Issue ni kwamba umeanza mada yako kwa kusema uongo. Huo sio uchambuzi wako. Baada ya kukubana kwamba umetumia chatGPT ndio unasema imekusaidia kupangilia hoja.
Nakuombea kwa Bwana Mungu akupe moyo wa upole na kiasi, hekima na utambuzi juu ya haya unayoyaandika in Jesus name - Amen 🙏🏿
Mbona hukusema hivyo tangu mwanzo? Ulitaka ujionyeshe kuwa unajua. Hayo ndiyo majivuno.
Nisamehe ili Bwana anisamehe - huenda nimejivuna bila kujua kwamba nimejivuna maana mimi sioni kama ninajivuna.

Lakini kumbuka nyuzi zako zote humu umeandika kwa kutumia AI bila kusema hii si akili yangu - Sikulaumu wala sikukosoi.

Ila pitia tena Mathayo 7:3-5 inasema - "Kwa nini waona kibanzi kilicho jichoni mwa nduguyo, na huoni boriti lililo jichoni mwako mwenyewe? Au watawezaje kumwambia nduguyo, ‘Niruhusu nitoe kibanzi jichoni mwako,’ na kumbe boriti liko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki! Toa kwanza boriti jichoni mwako, ndipo utaona sawasawa, na kisha utoe kibanzi kilicho jichoni mwa nduguyo."

Pitia na Warumi 2:1 inasema - “Kwa hiyo huna udhuru, ewe mwanadamu, ye yote ahukumuye; kwa maana katika hayo umhukumuye mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe unayehukumu watenda hayo hayo.”
Kama kukuambia umesema uongo ndio kiburi basi ni dhahiri Maandiko huyajui..
Kuniambia ninasema uongo bila kuleta neno la kweli ni Kiburi cha ujuaji na ni Unafiki pia.

Kusema sijui maandiko si neno geni kwangu hata Maandiko yenyewe katika 1 Wakorintho 8:2 yanasema - "Mtu akidhani ya kuwa anajua neno lo lote, hajui bado kama impasavyo kujua."

Tumia hekima katika 2Timotheo2:23-25 inasema - “.......Na mtumishi wa Bwana hana budi kutengana na magomvi, bali awe mpole kwa watu wote, awe na uwezo wa kufundisha, mvumilivu, akiwaonya wapinzani kwa upole; labda Mungu atawapa kutubu wapate kujua kweli.”

Kumbuka hata Yesu mwenyewe alisema katika Marko7:6-9 - "Mnayaacha maagizo ya Mungu, na kushika yaliyo ya wanadamu"

Hivyo kama usipojibu kwa neno sitakujibu kamwe kwani hayo yatakua ni maagizo na hisia za kibinadamu.

God bless you.
 
Back
Top Bottom