Janey da prince
Member
- May 31, 2023
- 5
- 6
Utawala Bora ni namna ya kuwaongoza watu katika namna inayofaa,kwa kutumia rasilimali za taifa husika ili kuleta maendeleo katika taifa Hilo. Utawala Bora huchochewa zaidi pale anapokuwepo kiongozi Bora.
SIFA ZA KIONGOZI BORA.
1. Mwajibikaji.
Kiongozi Bora huyapa kipaumbele majukumu yanayomkabili kwa ajili ya taifa lake, pia huhangaika usiku na mchana kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
2. M'wazi na mkweli.
Kiongozi Bora huwa mkweli kwa raia na nchi kwa ujumla. Huwashirikisha watu kuhusu masuala yanayoendelea katika taifa lao. Huweka wazi changamoto zinazolikabili taifa ili watu waweze kuchukua hatua, pia huweka wazi mafanikio ya taifa na namna yanavyopatikana.
3. Asiye mbinafsi
Kiongozi Bora hajijali mwenyewe Wala kujipatia kipaumbele, hushirikisha watu kuhusu fursa zilizopo na pia hutumia fedha na rasilimali nyingine za taifa kwa ajili ya taifa na siyo kwa ajili yake binafsi.
4. Anayependa usawa.
Kiongozi Bora huona kwamba watu wote katika jamii yake ni sawa, hivyo huwaongoza kwa usawa pasipo ubaguzi wa rangi, jinsia, dini, Wala kabila.
5. Asiyepokea Wala kutoa rushwa.
Kiongozi Bora hapokei rushwa Wala kutoa rushwa ili aweze kuficha au kufichiwa Jambo Fulani alilolifanya yeye au mtu mwingine Bali hulianika hadharani na kumshughulikia mtu huyo ipasavyo. Pia huwajali watu wote kulingana na Sheria na siyo kulingana na Mali walizo nazo.
VIASHIRIA VYA UTAWALA BORA KATIKA JAMII AU TAIFA
1. Mahusiano mazuri Kati ya viongozi na raia wao.
Hii ni kwasababu viongozi wanapowapa nafasi raia wao, raia hao huwa huru kueleza changamoto zinazowakabili kwa viongozi ili ziweze kutatuliwa. Hii hufanyika kwa njia ya mikutano ya hadhara, vikao n.k.
2. Upendo, umoja na mshikamano Kati ya raia.
Hii ni kwasababu katika utawala Bora raia wote huonekana kuwa ni sawa, kwahiyo kutokana na kusikilizwa na kutendewa kwa usawa na viongozi wao, wao pia hujiona sawa hivyo kuamua kupendana na kusaidiana tofauti na kwamba wasingekuwa wanaoneshwa usawa, kwa sababu ukosefu wa usawa hupelekea majungu na visasi Kati ya raia kwa raia na hata viongozi wao
3. Amani
Taifa lenye utawala Bora huwa na amani kwasababu raia wanakuwa na Imani na viongozi wao wakiamini kwamba wanaongozwa katika misingi ya haki, ukweli, usawa na uwazi. Pia ni kwasababu watu wote wanakuwa chini ya Sheria kwamba hakuna mwenye haki ya kufanya makosa.
4. Maendeleo endelevu yasiyo na Kikomo.
Hii ni kwasababu raia hufanya kazi kwa bidii ili waweze kulipa Kodi kwa serikali kwa sababu viongozi hutumia fedha hizo zilizopatikana kwa njia ya Kodi na njia nyingine kihalali kwa ajili ya maendeleo ya taifa bila ubadhirifu wowote. Mapato haya hutumika katika ujenzi wa miundombinu Kama vile madarasa na madawati ili wanafunzi waweze kusoma kwa amani, njia za usafiri Kama vile reli, barabara, na madaraja kwa ajili ya usafirishaji wa watu, vitu, bidhaa na malighafi kutoka sehemu moja Hadi nyingine, njia za mawasiliano Kama vile minara ya simu n.k ili kurahisisha mawasiliano baina ya watu, ujenzi wa hospitali na vituo vya afya pia ununuzi wa dawa kwa ajili ya usalama wa afya za raia. Hali hii huchochea maendeleo kwa sababu miundombinu inakuwa rafiki kwa raia na shughuli zao za uzalishaji za kujipatia kipato.
5. Kuwepo kwa namna ya kuwasaidia raia pale wanapokumbwa na majanga mbalimbali.
Kwa mfano kutenga eneo maalumu kwa ajili ya waathirika wa majanga ya asili Kama vile vimbunga, mafuriko, tetemeko la ardhi n.k. kuwa na namna ya kuwasafirisha watu kutoka katika maeneo ambayo majanga haya yametokea kuwapeleka katika maeneo salama labda kwa kutumia magari au ndege au namna nyingine yoyote. Pia kutenga kiasi Cha fedha kwa ajili ya kutoa misaada kwa raia walioharibikiwa na kupoteza Mali zao kutokana na majanga haya ya asili, kwa sababu majanga haya yamekuwa tishio Sana katika kipindi hiki kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
6. Demokrasia.
Raia wanakuwa na haki ya kupiga au kupigiwa kura Kama tu watakuwa na umri wa kuanzia miaka kumi na nane (18) na kuendelea, pia Wana haki ya kuwachagua viongozi ambao wanawataka. Pia raia wana haki ya kuikosoa serikali pale wanapoona Kama Mambo hayaendi sawa.
7. Kuwaunga mkono wananchi katika shuguli mbalimbali zinazoweza kukuza Pato la taifa.
Kwamfano shughuli za kilimo na ufugaji kwa kutoa pembejeo za kilimo ambazo ni dawa pamoja na vifaa ili kuongeza uzalishaji katika nyanja hiyo pia kuingilia Kati Bei ya mazao na utafutaji wa masoko ili kuwapa motisha wakulima katika shughuli zao. Pia katika suala la biashara kwa kupunguza Kodi ili kuwatengenezea wafanyabiashara mazingira mazuri kwa ajili kukua zaidi na zaidi. Pia kuunga mkono suala Zima la michezo ili kuimarisha na kukuza vipaji vya raia hasa vijana wa kike na wa kiume katika jamii, kwa kusaidia katika masuala ya jezi mipira na hata zawadi kwa wale wanaofanya vizuri ili kuwapa motisha kufanya vizuri zaidi.
MAMBO AMBAYO HUTIA DOA UTAWALA BORA NA KUZOROTESHA MAENDELEO.
1. Rushwa
Kutoa au kupokea rushwa ni chanzo au kiashiria Cha mmonyoko wa maadili ya uongozi bora. Hii ni kwasababu rushwa ndio chanzo Cha matatizo mengi Sana ambayo hutokea katika jamii ya Sasa. Rushwa huzorotesha maendeleo, rushwa huhamasisha visasi, husababisha matabaka n.k katika kipindi hiki rushwa imekuwa ikitikisa kwa kiwango kikubwa katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo
Katika siasa rushwa imekuwa ikishika Kasi pale ambapo wagombea wa nafasi za uongozi wanapogawa fedha kwa raia ili waweze kuchaguliwa, Jambo ambalo siyo sawa kwani kiongozi Bora hutambulika kwa Sera na matendo yake na siyo kwa kugawa fedha.
Katika elimu pia kumekuwa na changamoto ya kwamba waalimu au wakufunzi huhitaji rushwa ya ngono kutoka kwa wanafunzi wakike hata wakiume ili waweze kupatiwa matokeo mazuri kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu matokeo ya mwanafunzi yapo mikononi mwa mkufunzi pia kutokuhusishwa katika adhabu mbalimbali kwa wanafunzi wa sekondari ambapo Kama wanafunzi Hawa hawatakubali watafeli na pia kupatiwa adhabu Kali sana Jambo ambalo linawaathiri Sana wanafunzi kisaikolojia na pia kushusha ufaulu wao.
Katika afya ambapo wenye uwezo ndio ambao hupatiwa matibabu Bora na ya haraka huku wasio na uwezo kusubiri kwa muda mrefu na kuambulia huduma zisizo Bora na Mara nyingine kulazimika kwenda kununua dawa hata Kama walikuwa na bima za afya, Jambo ambalo hupelekea vifo vya wanyonge kwa kiasi kikubwa.
Katika ajira watu wenye kitu Cha kuhonga au wenye ndugu au marafiki katika nafasi mbalimbali za serikali ndio ambao hupewa vipaumbele katika ajira huku wale wasio na chochote kukosa vipaumbele na hatimaye kukosa ajira.
Katika mahakama ambapo haki hununuliwa kwa fedha kwamba mwenye fedha ndiye mwenye haki hata kama ndiye mwenye makosa, Jambo ambalo hupelekea kuongezeka kwa unyanyasaji wa wanyonge na matukio ya kinyama katika jamii
2. Kutokujali.
Pale ambapo viongozi wanashindwa kujali changamoto zinazowakabili raia wao hupelekea kushuka kwa maendeleo ya nchi. Kwamfano Kama wananchi wanakabiliwa na changamoto ya maji serikali isipochukua hatua raia hawa wanaweza kutumia maji yasiyofaa ili tu waweze kuishi, wanaweza kutumia maji ya mifereji, mabwawa, mito ambayo siyo salama kwa afya zao ambapo yanaweza kuathiri afya zao na kupunguza uzalishaji. Pia katika suala la miundombinu Kama Barabara ni mbovu wafanyabiashara watashindwa kusafirisha bidhaa zao kutoka sehemu moja kwenda nyingine pia hata huduma nyingine zitashindwa kuwafikia watu hivyo kushusha kiwango Cha uzalishaji na kupunguza molari katika ulipaji Kodi wa serikali.
3. Kukosa uaminifu katika matumizi ya rasilimali.
Kwa mfano rasilimali fedha. Inapotokea bajeti ya kufanya Jambo Fulani kwa ajili ya maendeleo Mara nyingi hushindwa kutumika kwa namna stahiki ambayo imeelekezwa. Hii ni kutokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waaminifu, hutumia kiasi Cha fedha katika bajeti hiyo kwa ajili ya manufaa yao binafsi Jambo ambalo linazorotesha maendeleo katika jamii.
SASA NINI KIFANYIKE?
1. Upendo, umoja, na mshikamano baina ya viongozi ili kwa pamoja kazi zao ziweze kuleta Tija kwa taifa.
2. Ufuatiliaji wa maendeleo katika nyanja mbalimbali ili kuweza kubaini changamoto na kuzitatua.
3. Uaminifu, ukweli na uwazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Upvote
1