Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Zamani enzi za utawala wa Nyerere, kila Mtanzania aliitwa ndugu, pamoja na Nyerere mwenyewe akiwa Raisi wa nchi. Nyerere aliitwa "ndugu raisi" sawa tu na mtu wa mtaani. Hata kwa mtu ambae ulikuwa humfahamu, ukitaka kuuliza kitu tulianza kwa kusema "samahani ndugu, sijui basi la kwenda ferry ni lipi".
Watanzania wote tulikuwa ndugu, bila kujali kama wewe ni masikini, muuza karanga mtaani, kiongozi au hata jobless, lofa tu wa mtaani, bado uliitwa "ndugu" kama ambavyo raisi wa nchi aliitwa ndugu raisi. Jambo zuri kabisa lililoondoa matabaka nchini.
Akaingia Raisi Mwinyi na umwinyi kutoka Zanzibar, watu wake ndani ya CCM wakamshawishi kwamba viongozi wa Tanzania hawawezi kuitwa kwa namna moja na wauza karanga mitaani, bali wao waitwe "weheshimiwa", na hata kuanza kuimba bila aibu kuwa CCM ina wenyewe, waheshimiwa. Nyerere akashangaa sana.
Basi leo tunaona matokeo na laana hii ya ubaguzi wa ndani ambao chama hiki kinachotawala, CCM, kiliianzisha. Matokeo sasa ni kwamba Tanzania imezaa tabaka la viongozi (vigogo) ambao wanajiona wako tofauti na hata sheria za nchi haziwahusu. Tuna hili kundi la viongozi, "waheshimiwa" ambao halitaki kusikia maoni ya mtu mwingine ambae haitwi mheshimiwa. Wao wanajiona wanajua kila kitu na hawapaswi kuulizwa, na wako juu ya sheria, na Polisi, Usalama wa Taifa na hata JW wakati fulani, wapo kwa ajili ya kuwalinda wao, nafasi zao na utajiri wao ambao kila mtu anajua umetokana na ufisadi na sio mishahara yao. Wameamua kwamba mtu yeyote asie mheshimiwa, akileta ubishi au maoni tofauti wasiyopenda, atekwe, apigwe hata kuuawa ikibidi!
Hawa "waheshimiwa" na familia zao wamekuwa wakibebana katika nafasi za serikalini, na hata kutengeneza mazingira ili watoto wao waje waurithi "uheshimiwa" hapo baadaye, jambo ambalo limeleta wingu kubwa la vigogo ambao baba zao walikuwa vigogo huko nyuma!
Siku hizi hawa "waheshiwa", hata magari yao yanatofautishwa. Wanapewa ving'ora na taa za blue kwa sababu wao wanajiona hawapaswi kukaa kwenye trafik jam (foleni) kama Watanzania wengine ambao sio waheshimiwa! Wao wana haraka kurudi nyumbani kwa familia zao baada ya kazi, kwa hiyo wapishwe barabarani! Ukikwaruza gari yao au kuwanyima kupita, mara nyingi wanauliza "unajua mimi ni nani?", mentality ya mimi ni mheshimiwa, wewe ni lofa tu!
Sasa nawauliza Watanzania wenzangu, hili linavumilika? Linakubalika? Tufanyeje ili kulikomesha mara moja?