Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JPM ndo source ya mambo yote, alivurugavuruga mambo mengi hamkuyaona? Alitawala kibabebabe hamkuona?Hatuta msahau jpm
Hilo nakubaliana na wewe kabisa ila hapa nawaning'iniza Lumumba kwa sababu ndio hasa ambao tayari wamesha-prove failure!I bet sio Lumbumba tu, hii hoja ipo kitaifa zaidi. Inawezekana kabisa taifa halina watu madhubuti kuongoza. Tutalalamika hivi hadi vizazi vyetu vipite...
Nakubaliana na wewe.SSH ni failure, kwa vile anapigiwa vigelegele vya kinafiki mitandaoni na wale haters wa JPM anajiona na yeye eti ana akili, hili ni shimo na litaidondosha Tz yote.
CCM ni failure ila vyama vingine ni disaster.Hilo nakubaliana na wewe kabisa ila hapa nawaning'iniza Lumumba kwa sababu ndio hasa ambao tayari wamesha-prove failure!
Kwamba ni tatizo la kitaifa, binafsi nishawahi kusema mara kadhaa huko nyuma kwamba nchi hii pale Magogoni/Chamwino iwepo CCM, CHADEMA, au ACT bado yatakuwa yale yale tu kwa sababu hata hao wengine wanatoka kwenye jamii ile ile wanayotoka Lumumba!!!
Sema hao wengine nalazimika kuwapa benefit of the doubt, kitu ambacho CCM hawa-deserve!!!
Mkuu tusizunguke Sana! Tatizo ni TFF, wao walishindwa nini kutafsir sheria? Au zile sheria zpo Kama mapambo??Unajichanganya, hiyo amri kama imetoka juu ndio uongozi wa Samia unahusika, usizunguke mbuyu.
Kama nilivyosema, kwa ujumla Watanzania, kama sio Miafrika, sie viumbe tuna matatizo makubwa sana lakini hao wengine I mean upinzani, sina budi kuwapa the benefit of the doubt!CCM ni failure ila vyama vingine ni disaster.
Hii nchi ina changamoto nyingi sana.
Umeongea ukweli halisi mkuu. Tutaongea hadi vizazi vyetu viishe, vile natamani tu upinzani nao upate chance ya kuongoza. Ili hii hoja iwe na mashiko.Hilo nakubaliana na wewe kabisa ila hapa nawaning'iniza Lumumba kwa sababu ndio hasa ambao tayari wamesha-prove failure!
Kwamba ni tatizo la kitaifa, binafsi nishawahi kusema mara kadhaa huko nyuma kwamba nchi hii pale Magogoni/Chamwino iwepo CCM, CHADEMA, au ACT bado yatakuwa yale yale tu kwa sababu hata hao wengine wanatoka kwenye jamii ile ile wanayotoka Lumumba!!!
Sema hao wengine nalazimika kuwapa benefit of the doubt, kitu ambacho CCM hawa-deserve!!!
Acha ujinga wewe.KITENDO cha kuahirishwa kwa pambano la Simba na Yanga lililokuwa lichezwe jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kumewafanya wadau wa soka kucharuka na kudai ni aibu kubwa kwa soka la Tanzania, kwa mechi kuahirishwa kienyeji kwa sababu za kisiasa, huku wengine wakisema kuna kitu nyuma ya kilichotokea.
Wadau mbalimbali wakiwamo wachezaji wa zamani, makocha sambamba na mastaa wamelizungumzia tukio hilo wakisema linaoonyesha ndani ya TFF na Bodi ya Ligi (TPLB) kuna mambo yanayohitaji kuondolewa ili soka lisonge mbele.
Mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, George Masatu alisema: “Yanga wamefuata taratibu za ligi zinavyoelekeza, muda ulikuwa saa 11 mechi ianze, wamefika na wamefanya ‘warm-up’ na kusubiri dakika zinazotakiwa.
“Wametoka baada ya kumaliza taratibu za uwanjani na kwenda vyumbani, wapo sahihi maana sababu ya msingi haijawekwa wazi, uamuzi ama kama kuna adhabu kwa Yanga kuondoka uwanjani itajulikana baadaye.
“Ni aibu kubwa sana kwa wasimamizi wa soka nchini kutozingatia kanuni na sheria za ligi zinavyoelekeza, maana zipo wazi kwamba kama kuna mabadiliko yoyote yafanyike kabla ya saa 24 za mechi, kwanza ni lazima mabadiliko hayo yatolewe kwa maandishi sio kupigiana simu.”
Kocha wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa amesikitishwa na wasimamizi wa ligi kutofuata kanuni zinavyoelekeza na kubadilisha ratiba kwa namna wanavyotaka.
ADVERTISEMENT
“Kubadilisha muda wa mechi ghafla kama hakuna sababu za msingi sio jambo linaloleta afya kwenye mpira, kwani hata kwenye timu yangu iliwahi kunitokea, huwa inaumiza sana, kiukweli hawazingatii wala kujali kanuni zinasemaje.
“Yanga wameingia uwanjani kwa mujibu wa kanuni inavyoelekeza kuwa timu ifike saa 1.30 kabla ya mechi kuanza, Bodi ya Ligi na TFF walikuwa na muda wa kufanya mabadiliko jana (juzi) kama kuna jambo la msingi lilikuwepo na sio kutoa taarifa muda mfupi kabla ya mechi kuanza.
“Ikumbukwe kwamba mashabiki waliingia uwanjani mapema sana, wengine wakiwa na watoto wadogo, kuna suala la kufuturu hilo wanaliangalia vipi, watu wameingia hasara kwa kulipa viingilio, ni aibu sana,” alisema Mkwasa.
“Wamesema kuwa wamepokea taarifa kutoka serikalini, je serikali inafanya mambo yake ghafla namna hiyo, nadhani nao wana muda ambapo wangetoa taarifa toka jana (juzi). Yanga wameheshimu ratiba na muda uliopangwa ingawa labda wangetumia busara tu kusubiri muda walioamua wenye mpira, maana haiwezekani ukae na wachezaji muda mrefu baada ya kupasha.”
Mchezaji wa zamani wa Simba, Azizi Nyoni alisema: “Yanga haikupaswa kutoka uwanjani kama timu ilikuwa imejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo, soka letu tunalijua wenyewe namna linavyoendeshwa.
“Haya mambo hayajaanza miaka ya sasa, hata enzi zetu mambo kama haya yalikuwepo sema tu watu waliona kama vitu vya kawaida.”
Upande wake Emmanuel Gabriel, nyota wa zamani wa Simba na Stars alisema: “Kisheria Yanga si ipo sahihi? Hata mimi nililifikiria sana jambo hili, TFF wamechemka aisee.
“Hadi hapa nashindwa kuzungumzia, ina maana asubuhi hawakukaa kikao (pre match meeting)? Hayo yote yalikuwa yazungumzwe hapo na sio vinginevyo.”
MITANDAONI KWALIPUKA
Mwanasiasa maarufu hapa na mbunge wa Bumbuli aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa: “Kwa kutambua kwamba inawezekana mamlaka za mpira zisifanye maamuzi sahihi, umewekwa utaratibu wa malalamiko. Kama timu haikubaliani na maamuzi ya mamlaka husika, inaweza kucheza ‘under protest’ huku ikiwa imeweka malalamiko kwa maandishi, kama kanuni zinavyoeleza.”
Mchambuzi wa soka kutoka Wasafi Fm, George Ambangile aliandika: “Muda wa kifo tu ndio unacheleweshwa, lakini lazima leo mmoja atachinjwa ...sijui nani huyo, eti wadau nani anakufa leo kwa Mkapa baada ya futari.”
Edo Kumwembe, mchambuzi wa Mwanaspoti na Wasafi FM alituma picha ya mchekeshaji Joti kisha aliandika: “Joti sisi watu wa mpira hautuwezi...mpira wetu unachekesha kuliko wewe.”
Mchambuzi wa kituo cha redio cha E Fm, Oscar Oscar ‘Mzee wa Kaliula’ aliandika hivi: “Timu zote zinapaswa kugomea haya mabadiliko ya kiholela, mpaka sasa Simba na viongozi wake ndo wamepost mabadiliko hayo kwenye kurasa zao rasmi, lakini Yanga hawajasema chochote, katika hili viongozi wangu wa Simba wameonyesha kutokututhamini sisi mashabiki tulioingia uwanjani kuanzia asubuhi, labda kwa kuwa wao wanaingia na ving’ora hawajui shurba ya hili jua kuitafuta saa 11. Mpira wa miguu ni kwa ajili ya wanamichezo na siyo mali ya kiongozi yeyote wa kisiasa. Timu zote zinatakiwa ziheshimu mashabiki au washinikize mechi ichezwe muda uliopangwa au isichezwe kabisa.”
Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na mchambuzi wa E Fm, Jemedari Said Kazumari aliandika: “Wadau mmepokeaje taarifa hii kutoka TFF? Weka comment yako hapa chini. Mimi nasema hii ni hali ya kukosa mpangilio (disorganized). Kuna dharura gani? Vinginevyo mambo yanafaa kutabirika na kwenda kwa mtiririko uleule.
“Halafu kubadilishwa kwa lisaa hiyo sawa, lakini saa 8 tuko kiwanjani tunaambiwa mechi ni saa 1 jioni masaa zaidi ya manne.
“Kiwanja hakina miundombinu ya kupata vitu muhimu kama vyakula (futari) kwa waliofunga, mazingira hayawezi pia kukupa wasaa mzuri wa kukaa hapa kwa hayo masaa manne. Kiwanja chetu ni kuja kuona soka unaondoka.”
Msaani wa muziki wa Bongo Fleva ambaye ni shabiki maarufu wa Arsenal na Yanga, Madee aliandika: “Kwa Mkapa tayari...Yanga wawili na kimkia kimoja..mechi yetu ni saa 11:00. Saa moja tunajua ni Manchester City na Chelsea.”
Zitto Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo pamoja na John Heche wa Chadema wamefagilia uamuzi wa Yanga waliouita wa kijasiri na kutaka waliohusisha kulichezea na kulivuruga pambano hilo iwe wizarani au TFF na Bodi wachukuliwe hatua kali kurejesha furaha ya mchezo wa soka nchini, sawa na alivyotoa kifagio Boniface Jacob, aliyewahi kuwa meya wa Ubungo aliyedai yeye ni Simba damu kama kina Heche na Zitto, lakini amefagilia walichokifanya Yanga.
Ahsateni Wananchi ahsanteni watani wa jadi.
Kwa mpira tu ndiyo umeona mambo yanakwenda kizembe?Hii ni reflection ya jinsi mambo ndani ya nchi hii yanavyoenda kizembe.
Mkuu, una kichwa/akili kizito.Kwa mpira tu ndiyo umeona mambo yanakwenda kizembe?
Hata kama nimetumia miguu, siwezi ku judge performance ya Rais kwa kutumia mechi ya Simba/YangaMkuu, una kichwa/akili kizito.
Nakubaliana na wewe. TFF walikuwa na uwezo wa kakataa kutii amri kwa kuzingatia kanuni zao hata kama amri ingetoka Ikulu.Mkuu tusizunguke Sana! Tatizo ni TFF, wao walishindwa nini kutafsir sheria? Au zile sheria zpo Kama mapambo??
EXACTLY...Umeongea ukweli halisi mkuu. Tutaongea hadi vizazi vyetu viishe, vile natamani tu upinzani nao upate chance ya kuongoza. Ili hii hoja iwe na mashiko.
EXACTLY...
...tena sio tu ili hoja iwe na mashiko bali hiyo itatupa fursa ya kujitathimini kama taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo tunalazimika kuwabembesha jumba bovu CCM, na kwa bahati mbaya sana kwao , hawana legitimacy ya kukana shutuma zote tunazowapa kwa sababu ni wao ndio wanaendesha nchi for 60+ years now!!