Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Hii biashara imeingiliwa na wahuni.

Walishindwa nini kuwagawa bure hao vifaranga badala ya kuwachoma?
Gharama za utunzaji zimekuwa kubwa mno nadhani hata bei za vyakula vya kuku ni ghali sana hii imefanya wengi wasifuge tena........

...hata wangetoa bure huenda wasingepata wachukuaji wengi.
 
Serikali ipewe hivyo vifaranga kulisha kunguru wao weusi. Badala ya kuwaacha wazaliane na kutumalizia kuku na ndege wetu!
 
hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Wangeamua kuvigawa bure je???
 
Mbna hata binadamu original kutoka kwa Allah ni wawili tuu (Adam na Hawa). wengine sisi ni utundu wa binadamu.
 
Vifaranga vya kuku wa nyama na mayai zaidi ya elfu 30 vimeteketezwa kwa moto mkoani Kilimanjaro baada ya kukosa soko la ndani baada ya nchi kufunguliwa na kusababisha maelfu ya vifaranga kuingizwa nchini kutoka nje kiholela wakiwa wanauzwa kwa bei ya chini, hivyo kuuwa kabisa soko la ndani na kuwafanya watanzania wenye viwanda vya kuku kuangukia pua.!

Ikumbukwe kipindi Samia akiwa makamu wa rais kuna vifaranga kutoka Kenya viliingizwa kinyemela vikakamatwa na mamlaka za Tanzania na kuchomwa moto, kitendo kilichomkera sana Rais Samia na kuamua kuifungua nchi.
 
Ujue kutoa uhai wa kiumbe ni ukatili uliopitiliza, Mimi hata kuchinja
 
Wengine wanawaita kuku zezeta 😀😀😁🙄
 
Kwa hiyo mfanya biashara anaweza kuona ni heri avichime kuliko kushusha bei akauza japo 500tsh akapata nusu bei? Hivyo vifaranga vina corona.

Walete sababu nyingine ila hizo ngonjela wadangaye wajinga
Hao watakuja wamejifunza huu ubaya kwa 'jiwe'. Unakumbuka wale vifaranga wa Kenya pale Namanga?
 
Kheri wangevitoa kwa makazi ya wazee na yatima ili wavifuge, nashauri serikali ichukue hatua dhidi ya wahusika wa kitendo hicho kiovu.
 
Exactly [emoji817]...
Aisee kiukweli watu wana roho mbaya sana...
Si bora utoe bure..huu ni ushetani mkubwa sana..
 
Hiko kiwanda wamefanya hivyo kupunguza hasara. Unazalisha umuuzie mfugaji let say una stock ya vifaranga 4000 unasubiri vitoke hakuna wanunuzi utafanyaje
Kwa hiyo ukiwachoma ndo unakwepa hasara?
Wamesafirishwa hadi Dar na kurudisha tena Moshi hiyo gharama ya usafiri, kutotolesha na matunzo itafidiwa na kuwachoma moto? Vipi wangeuza hata kwa jero jero ili kupunguza hasara au kugawa kwa wananchi wenye uwezo wa kuwatunza?
 
hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Ee kuliko vingekufa ni bora wameviokoa kwa kuviteketeza kwa moto[emoji706][emoji706]
 
Ee kuliko vingekufa ni bora wameviokoa kwa kuviteketeza kwa moto[emoji706][emoji706]
Mzee kipi ni bora kati ya kufa kifo cha mateso kwa siku 20 na kufa ndani ya dk 1?. Vyote ni Vifo ila kipi kinauma zaidi?
 
Wizara iwawajibishe hao watu kufanya uteketezaji wa vifaranga kinyama namna hiyo........huwezi kuteketeza kiumbe ambaye bado ana uhai kwa moto.

Wangeweza kutumia hata 'gas chamber' na kuwateketeza kwa njia ya gesi ya sumu na wakafa bila maumivu yoyote.

Huu ni ukatili wa kiwango cha juu cha wanyama na sidhani kama watu wa haki za wanyama wameshachukua hatua zozote.​
 
Huu nchi swala la kufikiri limekuwa changamoto sana. Think [emoji35]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…