Uteketezaji huu wa vifaranga ni unyama uliopitiliza

Kilichosababisha soko la kuku kuanguka ni sera mbovu za rais wenu Samia za kufungua nchi!

Eti kufungua nchi,

Watu wameuza mazao yote nje ya nchi wakati soko letu la ndani lilikuwa bado halijitoshelezi.
Kilichotokea sasa ni vyakula vya kuku kupanda bei na wafugaji wameacha kufuga maana hawaoni faida ya kufuga.

Mwezi uliopita Samia akiwa arusha eti anawambia watu kwamba kipindi kile vifaranga vimechomwa haikuwa sawa kama vile yeye hakuwa makamu wa rais.

Tumwache aendelee kufungulia nchi huku wakenya wakijaza mavifaranga yao na huku wa ndani wakikosa soko.

Atajifunza akiwa amechelewa sana.
 
Kweli kabisa ni UKATILI wa hali ya JUU. Wangeuza hata kwa nusu/robo bei kisha wasimamishe uzalishaji kwa muda.

Kuna wale waliokuwa wakiruka na kudondoka chini wakijaribu kujiokoa lkn nao waliokotwa na kurushwa kwenye tanuru la moto.
 

Serikali ingejikita kuthibiti mfumuko wa bei. Ni tatizo kubwa sana.

Viwanda na biashara nyingi zitafungwa na ajira nyingi zitapotea.
 
Yote haya yamesababishwa na nchi kuvurugwavurugwa na huyu bibi ambaye ameenda kubembea marekani.kila aina ya takataka aneziruhusu kuingia nchini na matokeo yake viwanda vya ndani vimekosa soko.
Hakusababisha ukatili wa kuvichoma moto.
 
Huenda ni strategy,kuna ujumbe wanataka kuufikisha kwa Rais kwamba afunge mipaka
 
Hakika NI ukatiri mpaka najiuliza

Je nisahihi kutupa chakula ili Hari Kuna watu Wana njaa na wanaki hitaji ?

Kwanini wasinge vigawa kwa wakazi wa eneo hilo Kesho wange kula hata nyama

labda kwa mwaliko wa harusi sherehe wange bahatika kula nyama
lakini kuvichoma Hawa jamaa niwanyama 😡😡😡
 
Si kweli.

Ongea na Wafugaji.

Unaweza kuhiari kununua kifaranga kwa bei ya juu ikiwa kimekidhi sifa zote....za Mbegu bora!!

Quality ya baadhi ya Wazalishaji wa ndani iko chini.

Wafugaji wanafanya biashara...Lazima waendane na kinachowapatia faida...

Siyo kweli kwamba Mashamba yote yana ubora unaohitajika...

Kama mtu siyo Mfugaji hawezi kuelewa hiki kitu...!

Wafugaji wakubwa wanajua. .

Wa kati wanajua

Wadogo wanaweza wasijue...!
 
Hujui chochote!

Hao wazalishaji kwa taarifa yako wanategemea wafugaji wadogo wadogo ambao huchukua kukua kuanzia 200 na kuendelea, ambao kwa sasa wako hoi kiuchumi
 
mweusii yulee falaa tuuu hana uzungu wowotee... huwezi kuua vifaranga wote wale tena unawachoma wakiwa hai wakati kiukweli kuna wafugaji wengi ukiwapa bure hawawezi kukataaa.
Mkuu uwape bure alafu watawalisha nini?

Unga tu wa kula nyumbani watu unawashinda sembuse kununua chakula cha kuku ambacho mfuko mmoja una kimbilia laki 1?
 
Mkuu uwape bure alafu watawalisha nini?

Unga tu wa kula nyumbani watu unawashinda sembuse kununua chakula cha kuku ambacho mfuko mmoja una kimbilia laki 1?
wewe tangaza hata bei ndogo uonee kama utakosa watejaaa yani mnafanya overproduction mpaka vifaranga 3000 na bado mnataka muendelee kuzalisha wengine... huyo mtu wa sales nae wakufukuzaa kazi.
 
Wakishindwa hata kuwafadhili akina mama wenye vikundi na baadae walipwe hata kwa riba ndogo imenisikitisha maana wamelenga hasara ya moja kwa moja
 
Yeye ndie kakosa soko na sio soko limejaa, watu wanahangaika kusaka vifaranga, hawapati
 
Kuliko kuchoma wangeviachilia porini vikaliwe na viumbe vyote angekuwa amesaidia Sana nature, waachie hata kunguru wajipatie
 
hapo pana utata inawezekana hata wao hawajapenda ila mazingira yalikuwa ni limited kwao! Maana ilikuwa inatakiwa kuvilisha na kuvitibu kila siku, so kuliko kubiacha vife na njaa wameona bora vichomwe tu
Lo! hapana nina mabanda hayana vifaranga wagenipatia hata 1000 nigejitahidi kupata chakula .Kweli walishidwa hata kututangazia watu wa Dar hata watuuzie kwa 500 wasingekosa wateja. mm nilitamani kidogo nipige ukunga nilivyoona ule moto. hawakuwaza vyema.yule mmliliki hata sikumuelewa.
 
Mama Mzungu angetoa bure hata kwa wasio na mtaji wakaanze kufuga
 
Bora angetangaza angepata watu wengi Wana shida na vifaranga. Nadhani hakutangaza vya kutosha.
Bora angewapa hata madalali wao wanajua soko. Inatakiwa aboroshe sekta yake ya marketing Hakuna bidhaa inayokosa soko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…