Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Mbona matusi ndugu kuwa mstaarabu. Tujadili kwa hoja na sio matusi au hasira, wewe kila mtu hapa unamtukana kwa nini uko hivyo?
Naona kila ninapokuelekeza unakuja na majibu ya KEBEHI na nshakuele several times kwamba mi sio msemaji wala mwajiriwa wa Tume, natumia uzoefu wa kuchambua rufaa kwa 5+ years kabla ya kuondoka kuelezea process zilivyo.

Kuna watu wanauliza swali ili kueleweshwa na wengine wanaamua kubishana (kama wewe)
Nadhani unajua vema ofisi zilipo.

Kama una kitu unataka kuwelewa niulize. Kama una malalamiko
Ntakupa physical address na postal pia
 
Mkuu kama simu kupokea ni shida ndio barua hahahahahahahah
 
Mkuu kama simu kupokea ni shida ndio barua hahahahahahahah
NIAMINI MIMI ANDIKA BARA UONE KAMA NDANI YA 14DAYS HUTAJIBIWA.

Shida ya simu inaenda direct kwa PS wa bosi na mbaya zaidi pale kivukoni wapo kwa muda saivi nimeambiwa wanajiandaa kwenda Dodoma. so extension foni hazikuunganishwa jambo lilipelekea PS kupokea simu nyingi na kulazimika kwenda kwa muhusika (ambaye huwezi kuambiwa jina lake wala kupewa namba yake). Sa imagine atatembea ofisi ngapi kupeleka simu?? (HUO NDIO UKWELI JAPO HAUPENDEZI)
 
Mkuu Taasisi nyingi za serikali zimeoutomate shughuli zao nyingi sana mfano wizara ya fedha, Tamisemi wanatumia mifumo iliyoandaliwa na wataalamu kutoka eGA kwahiyo ni muhimu kwa Tume kuwatumia ili kuautomate shughuli zao ili kupunguza paperwork
 
Sasa huo ni utendaji gani Tume haioni aibu ofisi kubwa kama hiyo simu moja tuu? Hao tume wapo hapo kwa zaidi ya miaka 3 simu anapokea mtu mmoja tuu??? ambae anajibu vibaya no customer service mara hapokei simu, mara anakukatia simu kabda hujamaliza ongea mara anaongea kwa speed bila kukusikiliza! hao maboss hapo na makamishna hawalioni hilo? utetezi eti mnahamia dodoma hiyo ndio sababu ya kuwa na huduma mbaya ya simu? na huduma mbaya kwa wateja?
 
Mkuu Taasisi nyingi za serikali zimeoutomate shughuli zao nyingi sana mfano wizara ya fedha, Tamisemi wanatumia mifumo iliyoandaliwa na wataalamu kutoka eGA kwahiyo ni muhimu kwa Tume kuwatumia ili kuautomate shughuli zao ili kupunguza paperwork
Huu ushauri mimi haunihusu mkuu nadhani nshajieeleza huko juu, was just helping
 
Mimi nimefuatilia rufaa ya ndugu yangu tokea mwaka juzi mpaka yeye mwenyewe anaona sifuatilii kwasababu majibu ninayoyapata yanafanana kila siku wasipobadilika ninauhakika malalamiko hayataisha
 
Sijui unaongea kufurahisha jukwaa hili. Una uhakika na hili kweli wewe? Eti sio kila mrufani akichelewa kupeleka rufaa yake inatupiliwa mbali? Je TUME inafanya hivyo? Je TUME inaangalia sababu ya mrufani kuchelewa? Je huwa TUME inaangalia kama mamlaka ya nidhamu imemuelekeza mtumishi akate rufaa wapi? Hayo unayoeleza humu yangekuwa yanatekelezwa na TUME malalamiko kwayo yangepungua sana.
 
Msemaji wa TUME katika ubora wake wa majibu wa wateja wake.
 
e huwa TUME inaangalia kama mamlaka ya nidhamu imemuelekeza mtumishi akate rufaa wapi?
Hiki ni kigezo cha msingi sana mtu anapopeleka rufaa yake tume HATA IKIWA NJE YA MUDA.

KIPO KWENYE PROCEDURES kama mrufani alielezwa MUDA, NA MAHALI PA KUKATA RUFAA.

HII ITAONEKANA KWENYE BARUA YA UAMUZI.

UKIWA NA SABABU NYINGINE UWE NA SABABU NA BACKups za msingi. HAIWEZI KUTUPWA NJE.
 
Msemaji wa TUME katika ubora wake wa majibu wa wateja wake.
Wewe ni rahisi kuwasiliana nao waje wasome hoja za wadau hapa
NAOMBA NIWAACHE NIENDELEE NA KUFURAHIA MAJUKWAA MENGINE.

KILA LA HERI WAKUU.

BEST SOLUTION ANDIKENI BARUA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI NAKALA IKULU KWA KUSPEED UP ISHU ZENU AU ANDIKE MAKALA GAZETINI BILA KUWEKA MAJINA YENU.

UJUMBE UTAFIKA MAPEMA ZAIDI
 
Hao Tume wajirekebishe kwa nini rufaa nyingi zipo pending wakati muajiri amejibu na vielelezo vipo. Wangedesign template ambayo wangeitumua mfano template hiyo pamoja na mambo mengine ktk kila rufaa ingeangalia vitu viwili vya msingi 1. je mfanyakazi alifukuzwa kazi kwa sababu za msingi na za kweli (fair reasons) 2. Je utaratibu ulifuatwa. Kimojawapo kikikosekana au vyote vikikosekana basi ushindi ni wa mrufani. kama vyote vipo basi mamlaka ya nidhamu ipo sasa. Ni simple hivyo sasa wao kila kikao wanaleta rufaa chache mno. Hawana extra ordinary meetings!!! Hawafanyi maamuzi by circular resolution kwa rufaa ambazo ni simple mfano mrufani kuchelewa sana kupeleka rufaa tume nk.
NAOMBA NIWAACHE NIENDELEE NA KUFURAHIA MAJUKWAA MENGINE.

KILA LA HERI WAKUU.

BEST SOLUTION ANDIKENI BARUA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI NAKALA IKULU KWA KUSPEED UP ISHU ZENU AU ANDIKE MAKALA GAZETINI BILA KUWEKA MAJINA YENU.

UJUMBE UTAFIKA MAPEMA ZAIDI
 
Wamekaa tu kama robot kazi kusumbua watu. Hawana ubunifu.
Kwa mfano wanaajiri kwa utaratibu wa usaili ila wameruhusu utaratibu wa ajira za kujitolea kwa mkataba. Vijana wahitimu wanajitolea hadi wamekua nguvu kazi ya kutegemewa. Unakuta mtu yuko miaka miwili hapati ajira ya kudumu. Ingefaa kuwe na utaratibu tofauti kwa wale mumewapa ajira kujitolea ili waweze kupewa ajira za kudumu.
 
Ni simple hivyo sasa wao kila kikao wanaleta rufaa chache mno.
Ushawahi kuhudhuria kikao ikaona items ngapi zinaingia per kikao, Tume inakaa 14 ipitie taarifa mbalimbali na rufaa 150+ unasema chache.

Kuna rufaa inahoja 30+ Taarifa ya kamati kubwa kama Biblia hapo hujapitia majobu ya hoja, Standing Oder09, P.S Regulation2003, hujapitia Regs za Taasisi husika.

NI RAHISI SANA KUSEMA RUFAA NI SIMPLE
hii ilishafanywa na KAMATI YA UCHUNGUZI
Hawafanyi maamuzi by circular resolution kwa rufaa ambazo ni simple mfano mrufani kuchelewa sana kupeleka rufaa tume nk.
Mrufani anachelewaje kupeleka rufaa Tume wakati ana siku 45?
 
Ingefaa kuwe na utaratibu tofauti kwa wale mumewapa ajira kujitolea ili waweze kupewa ajira za kudumu.
USICHANGANYE OFISI WE MTU. TUME HAIHUSIKI NA HIKI ULICHOANDIKA NAONA UNATAFUTA HURUMA

VIBALI VYA AJIRA VINATOKA UTUMISHI NA AJIRA NI KWA "USHINDANI" TENA ZOEZI LINAENDESHWA NA SEKRETARIETI YA AJIRA

KAMA UMEHITIMU CHUO NA UNAUZOEFU WA MIAKA MIWILI YA KUJITOLEA UNAZIDIWAJE INTERVIEW NA FRESH GRADUATES???
 
Acha hizo wewe mahakama zinaangalia vielelezo kibao na kusikiliza mashahidi wengi tuuu lakini speed kubwa. Mbona CMA speed ya kesi ni nzuri? Shida tume haingalii hizo sababu mbili kwa mujibu wa sheria. 1. Fair reasons 2. Fair Procedure. Kwa nini wanahangaika na mambo mengine? Public Service Act na Standing orders ndio zimeweka mambo haya bayana hivyo vingine wanavitoa wapi. Matokeo yake ni kutoa maamuzi ya ndivyo sivyo.

Hii Tume imepewa dhamana ya kusimamia utumishi wa umma mizaha ya nini hapo. Walipaswa kujipanga na kurekebisha mambo. Wakirekebisha kasoro nani atalalamika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…