Utendaji Mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma; Rais Samia tupia jicho lako hapo

Ukishamalizana na Tume na Raisi unaenda CMA sio HC usipotoshe watu Hujui sheria wewe hapo Tume unafanyaje kazi kwa ufahamu huo?
Hii case unayoirejea ina uhusiano gani na TUME?? Nikusahihishe kidogo mi sio mtendaji wa Tuame nlishahama kitambo

nimekuambia ukitoka TUME unaenda kwa Rais ukishindwa huko unaenda MAHAKAMA KUU.

Naadhani umenielewa
 
Jamani enhe someni case ya John Mongella HC Labour Division meruhusu kwenda CMA tena ukitaka nenda CMA moja kwa moja achana na hao Tume. Ni ndani ya siku 30 baada ya kufukuzwa
Huyo hamna kitu anaisemea TUME asichokijua. Hajui hata kinachoendelea CMA na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Nafikiri huo uelewa mdogo ndio ulifanya akahamishwa TUME kama si alifukuzwa.
 
Mwajiri akuonee
Tume ikuonee
Rais akuonee

we umekuwa nani???
TUME ni kiunganishi kati Rais na Mwajiri. Hivyo Rais aliweka uaminifu wake kwa TUME ingawa TUME si waaminifu inanuka rushwa. Ndio maana hata Mh Rais akatamka kuwa hatarajii kupingana na maamuzi ya TUME kwa kuwa anaiamini na ndio maana sasa Mh Rais anaambiwa kuwa uaminifu wake kwa TUME si sawa kama alivyofikiri kwani TUME inashirikiana na Waaajiri kuhujumu mashauri ya rufaa ya watumishi wa umma.
 
Halafu hao Tume hata majibu ya rufaa yanachelewa kupelekwa kwa wafufani majibu wanatoa mwezi na nusu baada ya kikao yaani hata kuandika barua ya majibu tuu ni shida
TUME ni kiunganishi kati Rais na Mwajiri. Hivyo Rais aliweka uaminifu wake kwa TUME ingawa TUME si waaminifu inanuka rushwa. Ndio maana hata Mh Rais akatamka kuwa hatarajii kupingana na maamuzi ya TUME kwa kuwa anaiamini na ndio maana sasa Mh Rais anaambiwa kuwa uaminifu wake kwa TUME si sawa kama alivyofikiri kwani TUME inashirikiana na Waaajiri kuhujumu mashauri ya rufaa ya watumishi wa umma.
 
Halafu hao Tume hata majibu ya rufaa yanachelewa kupelekwa kwa warufani majibu wanatoa mwezi na nusu baada ya kikao yaani hata kuandika barua ya majibu tuu ni shida
 
Wewe EISTEIN 112 hapo ndio mwisho wa uelewa wako? ebu tupatie mfano wa kesi iliyoamuliwa kuwa CMA haiwezi tena kushughulikia malalamiko ya watumishi wa umma. Hapo unatupa wasiwasi maana wewe ni mtendaji wa TUME na inaonekana hujui sheria. Sasa maamuzi yenu (TUME) yatakuwa ya haki kweli kwa watumishi wa umma?
Sio kesi iliyoamua bali kuna mabadiliko ya sheria Cap 298 na marejeo ya mwaka 2019 kuna kipengele kilichowekwa kwamba issues zote za rufaa za watumishi wa umma zitaongozwa na Sheria hiyo then baada ya kuexhaust ndipo wanaweza kuseek other remedies. Hata CMA wanalitambua hili.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] hivi John Mbiso ndie alietoa tangazo kwenye uzi huu hapo mwanzo kuwa Tume ina staff 35 workload ni kubwa ndio maana rufaa za watumishi zinachelewa[emoji38][emoji38][emoji38]

Kazi kwelikweli!!
Ni jambo la kushangaza sana! Ni afadhali wangekaa kimya tu!
 
Hasira zako zinaufumba ufahamu wako, kuna mdau huko juuamesema rufaa yake ilichukua mda mfupi we yako ina mwaka?? kama mwajiri wako amepeleka vielelezo mapema basi vuta subira ishu yako inafanyiwa kazi na majibu utayapata usiporidhika utaenda ngazi za juu
Amepeleka mapema, kwani ni utashi wa mwajiri kupeleka vielelezo mapema au kwa kuchelewa, au ni sheria inamtaka kuwasilisha vielelezo ndani ya muda fulani? (Siku 14 baada ya kupokea nakala ya Rufaa)
 
Mkuu kwa mfano hajaleta unamfanyaje? Utaandika reminder tena na tena.

Kumbuka unaendelea na majukumu mengine, unless mrufani akumbushie ishu yake.
 
Yaani mbona Tume ina watu wa ajabu kama wewe? mnangoja kukumbushwa na mrufani wakati hammwambii kinachoendelea huko?

Raisi tunaomba ondoa hawa watu hawana sifa ya kufanya hii kazi.

Mpigie simu kabisa maana naona unateseka sana.

Unahisi.kwa mfano bado ningekuwa Tume ningekaa natafakari rufaa yako tu kati ya rufaa za watu maelfu ambao tayari wana vielelezo.

Sikia nshakuambia sio.msemaji wa Tume so usinikoti pambana na hali yako. ungekuwa na sifa ya kufanya kazi saivi usingekuwa umefukuzwa. Wenye sifa bado tupo mzigoni
 
Yaani mbona Tume ina watu wa ajabu kama wewe? mnangoja kukumbushwa na mrufani wakati hammwambii kinachoendelea huko?

Raisi tunaomba ondoa hawa watu hawana sifa ya kufanya hii kazi.
Ooh yes,hawafanyi kazi kwa kufuata Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Wanafanyakazi kwa jinsi wanavyoona wao na sio Sheria na Kanuni zinavyotaka, eti mrufani akumbushie wakati sheria inasema ni ndani ya siku 14 mwajiri awe ameleta vielelezo assuming other things remain constant!

Bure kabisa!!😆😆😆😆😆 up to infinite!!
 
Mkuu kwa mfano hajaleta unamfanyaje? Utaandika reminder tena na tena.

Kumbuka unaendelea na majukumu mengine, unless mrufani akumbushie ishu yake.
Unaandika reminder kwa nini wakati sheria ipo clear kuwa atume ndani ya siku 14??? Unambembeleza? Hiyo huruma ya kuandika reminder mnaitoa wapi na inakuwaje mnashindwa kuitumia huruma hiyo kwa watumishi wanaowasilisha rufaa zao nje ya muda?
 
Ni hivi baada ya Two reminders kama hajatekeleza anaitwa Mamlaka ya Nidham mbele ya tume kuja kutoa maelezo kwanini hajatekeleza maelekezo ya Tume.

Anyway maswali zaidi nendeni ofisini kwao Luthuli street kiwanja namba 10
 
Tunaomba tutaje baadhi ya taasisi zinazotoa rushwa kwa wajumbe wa tume ilikuondoa hisia.
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji mbovu wa Tume ya Utumishi wa Umma ikiongozwa na ndugu Muhoji aliyezungukwa na wasaidizi vilaza wavivu kutumia akili katika kushughulikia rufaa za watumishi wa umma walioonewa na waajiri enzi zile!

Kumekuwa na biasness kubwa sana katika kushughulikia rufaa za watumishi wa umma pale Tume.

1. Tume imekuwa ikishirikiana na waajiri katika kuhujumu haki za watumishi.

2. Rufaa zimekuwa zinakaa kwa muda mrefu bila kuzitolea maamuzi. Ningefurahi sana kujua kama kuna kipengele chochote kinachoibana Tume kuhusu muda.

3. Maafisa wa Tume hawako makini katika uchambuzi wa rufaa za watumishi.

4. Maafisa wa Tume wamekosa customer service or care kwenye kazi zao na hivyo kupelekea wwtumishi wanaokwenda kuulizia rufaa kuwafanya kama maadui, they are so defensive and protective.

5. Wamekuwa wakipewa rushwa na waajiri ili watumishi wakandamizwe ktk kudai haki zao kwasababu waajiri wengi wamekuwa wakiwabambikkiza makosa watumishi wao.

Hivyo basi, tunaomba Mh. Rais Samia tupia jicho lako kwenye hiyo Tume, wanafanya kazi kwa mazoea na kuminya haki za watumishi.
 
Nadhani umeamua kubishana

nimeeleza kuwa Mtumishi wa umma ukiwa na na shida dhidi ya Mamlaka yako ya Nidhamu/ Mwajiri sehemu pekee unapotakiwa kukata rufaa au kulalamika ni TUME YA UTUMISHI WA UMAA na sio CMA? na usiporiadhika na maamuzi ya TUME unakata Rufaa kwa Mh. Rais

Mabadiliko ya Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2019 yamewaondoa watumishi wote wa Umma CMA

ukiamua kuendelea kubishana endelea mi nshamaliza
EINSTEIN112 ngoja nikufundishe kidogo namna ya kusoma sheria (Act), itakusaidia kuelewa mambo na sio kubisha bisha bali kama utabisha basi itakuwa ni kwa hoja. Kama bado unafanya TUME ya Utumishi utaitumia fursa hii kuwaambia makamishna na watumishi wenzako kuwa Tafsiri sahihi ya sheria ni hii na sio hivyo mnavyoelewa. Darasa linaweza kuwa refu lakini SOMA uelewe maana ni muhimu kwako na kwa wenzako mnaoamua hatima za maisha ya watu kwa nguvu za kisheria mlizopewa (ingawa mnazitumia vibaya).

IPO HIVI
CMA ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kusuluhisha migogoro itokanayo au ihusianayo na ajira mwajiri na mfanyakazi). Mamlaka hayo CMA imeyapata kupitia kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mahakama/Taasisi za Kazi (The Labour Institutions Act Cap 366 RE 2019)

Screen Shot 2021-08-23 at 9.09.40 PM.png

Hapo unaona kabisa kuwa CMA ina mamlaka ya kusuluhisha mgogoro wowote wa kikazi unaowasilishwa mbele yake kwa Sheria yoyote ya mambo ya ajira (Sheria ya utumishi wa Umma ikiwa ni mojawapo ya sheria za kazi).

Sheria ya Ajira na mahusiano kazini (the Employment and Labour Relations Act CAP 366 R.E 2019) kupitia kifungu cha 2 (1) inaeleza vyema kuwa ITATUMIKA kwa wafanyakazi wote wa sekta binafsi na wa Serikali isipokuwa wachache wa serikali ambao wameainishwa. Wakati kifungu cha 34A cha Sheria ya Utumishi wa Umma kimeeleza kuwa unpotokea mkanganyiko kati ya Sheria ya Utumishi wa Umma na Sheria nyingine inayohusu utumishi wa Umma ( Sio ELRA), basi Sheria ya utumishi wa Umma (CAP 298 R.E 2019) itakuwa na nguvu dhidi ya nyingine (ya serikali). Kwa lugha rahisi ni kwamba, Sheria ya Utumishi wa Umma haina nguvu kuzidi Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (hata kwa watumishi wa Umma).
Screen Shot 2021-08-23 at 8.25.35 PM.png

RUFAA ZA WATUMISHI WA UMMA
Pale ambapo mamlaka ya nidhamu inakuwa imetoa adhabu (maamuzi) dhidi ya mtumishi wa umma kutokana na nguvu iliyopewa na sheria basi mtumishi huyo anaelekezwa kupitia Kifungu cha 25 (1) (b) cha Sheria ya utumishi wa umma kukata Rufaa kwenye TUME ya UTUMISHI WA UMMA.

Msisitizo,
Ni pale tu mamlaka ya nidhamu inapokuwa imetekeleza mamlaka yake kisheria kwa kutoa adhabu kwa mtumishi kama kumshusha cheo, kumshusha mshahara au kumfukuza kazi ndio mtumishi anaweza kukata Rufaa, kama hakuna adhabu iliyotolewa mtumishi hawezi kukata Rufaa.

Screen Shot 2021-08-23 at 9.32.49 PM.png

TUME KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA
Tume ya Utumishi wa Umma haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya Malalamiko ya Watumishi wa Umma. TUME haina uhalali wa kusikiliza migogoro mibichi (original jurisdiction) isipokuwa inaweza kusikiliza migogoro katika hatua ya Rufaa tu (Appellate Jurisdiction) kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 10 (1) (d) cha Sheria ya utumishi wa Umma. Kwa hiyo kinachofanyika sasa TUME kusikiliza Malalamiko ya watu pale ambapo mwajiri anakuwa amemkosea au anamuonea mtumishi. Mamlaka haya yapo CMA tu kama nilivyoeleza awali na TUME imeyapora kutoka CMA kwa kisingizo cha mabadiliko ya Sheria ya utumishi wa Umma, kitu ambacho sio kweli, tutakisoma kifungu hicho wanachotumia TUME na ambacho hakiwapi mamlaka hayo. Kazi za TUME ni hizi hapa;

Screen Shot 2021-08-23 at 7.44.38 PM.png

JE NI LAZIMA KISHERIA KWA MTUMISHI WA UMMA KUEXHAUST LOCAL REMEDIES KABLA YA KWENDA CMA?
Jibu ni inategemea na aina ya mgogoro.
Kama kinacholalamikiwa ni maamuzi ya mamlaka ya nidhamu basi mtumishi wa Umma anapaswa kukata Rufaa TUME na baadae kama hajaridhika kukata rufaa kwa Rais na kisha kama hajaridhika na maamuzi ya rais kurudi Mahakama Kuu kwa Judicial Review, hii ndio inaitwa exhaustion of local remedy. Lakini kama mgogoro ni malalamiko juu ya uonevu wa mwajiri basi mtumishi anaruhusiwa kwenda moja kwa moja CMA bila kupita popote sababu CMA ndicho chombo pekee chenye mamala ya kusikiliza migogoro ya kazi/ ajira. Hana local remedy anayotakiwa kuexhaust.

JE, MABADILIKO YA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA MWAKA 2016 YALIHUSU WATUMISHI WOTE?
Jibu ni HAPANA, mabadiliko hayo ya kuwataka watumishi waexhaust local remedies yaliwahusu watumishi wa umma walio katika ngazi ya OPERATIONAL SERVICE, yaani watumishi wasio na digrii. Ili uelewe vyema jambo hili, unatakiwa kusoma Sub Heading ya Kifungu cha 32 na 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma, kimeandikwa (c) Operational Service. Kwa hiyo Mabadiliko ya Sheria mwaka 2016 yaliongeza Kifungu 32A kuwahusu Watumishi wa Umma ambao wapo katka kundi la Operational Service tu na sio wengineo. BAHATI mbaya, Mawakili wa Serikali wamekuwa wakiipotosha Mahakama kwa kuwaambia kifungu hicho kinahusu waumishi wote wa Umma jambo ambalo sio kweli. Wamekuwa wakiweka Mapingamizi ya Kisheria kila mara mtumishi wa umma anapofungua CMA mgogoro usiohusu adhabu za mamlaka ya nidhamu wakimtaa aexhaust local remedies. Majaji na Waamuzi wa CMA nao wamekuwa wakiingia mtego huu wa mawakili wa serikali, labda kwa kutokusoma kifungu husika au kwa kukisoma vibaya. Maofisa ambao sheria ya utumishi wa Umma imewatambulishakuwa ni wale walioajiriwa kwa digrii (shahada) kama ngazi ya mwanzo kabisa ya ajira zao mfano maafisa kilimo, maafisa watendaji wa Kata, maafisa ugavi nk wanaitwa AFISA. Msingi wa kuongeza Kifungu hiki cha 32A ilikuwa ni kuwazuia watumishi wa Operational Service kwenda CMA moja kwa moja kwa kuwa Sheria ya Utumishi wa Umma hiyohiyo kupitia Kifungu cha 32 iliwaelekeza kuwa watumishi hao wanatawaliwa ama wanaongozwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini.
Screen Shot 2021-08-23 at 7.46.43 PM.png

Kwa hiyo, TUME ya Utumishi wa Umma imekwa ikitekeleza jambo amabalo haina mamalaka nalo la kusikiliza malalamiko na kuyatolea uamuzi.
Natumai EINSTEIN112 na wenzako mtakuwa mmenielwa vyema na mmejifunza.

Screen Shot 2021-08-23 at 7.47.57 PM.png
 
EINSTEIN112 ngoja nikufundishe kidogo namna ya kusoma sheria (Act), itakusaidia kuelewa mambo na sio kubisha bisha bali kama utabisha basi itakuwa ni kwa hoja. Kama bado unafanya TUME ya Utumishi utaitumia fursa hii kuwaambia makamishna na watumishi wenzako kuwa Tafsiri sahihi ya sheria ni hii na sio hivyo mnavyoelewa. Darasa linaweza kuwa refu lakini SOMA uelewe maana ni muhimu kwako na kwa wenzako mnaoamua hatima za maisha ya watu kwa nguvu za kisheria mlizopewa (ingawa mnazitumia vibaya).

IPO HIVI
CMA ndio chombo pekee chenye mamlaka ya kusuluhisha migogoro itokanayo au ihusianayo na ajira mwajiri na mfanyakazi). Mamlaka hayo CMA imeyapata kupitia kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Mahakama/Taasisi za Kazi (The Labour Institutions Act Cap 366 RE 2019)

View attachment 1905293
Hapo unaona kabisa kuwa CMA ina mamlaka ya kusuluhisha mgogoro wowote wa kikazi unaowasilishwa mbele yake kwa Sheria yoyote ya mambo ya ajira (Sheria ya utumishi wa Umma ikiwa ni mojawapo ya sheria za kazi).

Sheria ya Ajira na mahusiano kazini (the Employment and Labour Relations Act CAP 366 R.E 2019) kupitia kifungu cha 2 (1) inaeleza vyema kuwa ITATUMIKA kwa wafanyakazi wote wa sekta binafsi na wa Serikali isipokuwa wachache wa serikali ambao wameainishwa. Wakati kifungu cha 34A cha Sheria ya Utumishi wa Umma kimeeleza kuwa unpotokea mkanganyiko kati ya Sheria ya Utumishi wa Umma na Sheria nyingine inayohusu utumishi wa Umma ( Sio ELRA), basi Sheria ya utumishi wa Umma (CAP 298 R.E 2019) itakuwa na nguvu dhidi ya nyingine (ya serikali). Kwa lugha rahisi ni kwamba, Sheria ya Utumishi wa Umma haina nguvu kuzidi Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (hata kwa watumishi wa Umma).
View attachment 1905296

RUFAA ZA WATUMISHI WA UMMA
Pale ambapo mamlaka ya nidhamu inakuwa imetoa adhabu (maamuzi) dhidi ya mtumishi wa umma kutokana na nguvu iliyopewa na sheria basi mtumishi huyo anaelekezwa kupitia Kifungu cha 25 (1) (b) cha Sheria ya utumishi wa umma kukata Rufaa kwenye TUME ya UTUMISHI WA UMMA.

Msisitizo,
Ni pale tu mamlaka ya nidhamu inapokuwa imetekeleza mamlaka yake kisheria kwa kutoa adhabu kwa mtumishi kama kumshusha cheo, kumshusha mshahara au kumfukuza kazi ndio mtumishi anaweza kukata Rufaa, kama hakuna adhabu iliyotolewa mtumishi hawezi kukata Rufaa.

View attachment 1905301

TUME KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WATUMISHI WA UMMA
Tume ya Utumishi wa Umma haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya Malalamiko ya Watumishi wa Umma. TUME haina uhalali wa kusikiliza migogoro mibichi (original jurisdiction) isipokuwa inaweza kusikiliza migogoro katika hatua ya Rufaa tu (Appellate Jurisdiction) kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 10 (1) (d) cha Sheria ya utumishi wa Umma. Kwa hiyo kinachofanyika sasa TUME kusikiliza Malalamiko ya watu pale ambapo mwajiri anakuwa amemkosea au anamuonea mtumishi. Mamlaka haya yapo CMA tu kama nilivyoeleza awali na TUME imeyapora kutoka CMA kwa kisingizo cha mabadiliko ya Sheria ya utumishi wa Umma, kitu ambacho sio kweli, tutakisoma kifungu hicho wanachotumia TUME na ambacho hakiwapi mamlaka hayo. Kazi za TUME ni hizi hapa;

View attachment 1905302

JE NI LAZIMA KISHERIA KWA MTUMISHI WA UMMA KUEXHAUST LOCAL REMEDIES KABLA YA KWENDA CMA?
Jibu ni inategemea na aina ya mgogoro.
Kama kinacholalamikiwa ni maamuzi ya mamlaka ya nidhamu basi mtumishi wa Umma anapaswa kukata Rufaa TUME na baadae kama hajaridhika kukata rufaa kwa Rais na kisha kama hajaridhika na maamuzi ya rais kurudi Mahakama Kuu kwa Judicial Review, hii ndio inaitwa exhaustion of local remedy. Lakini kama mgogoro ni malalamiko juu ya uonevu wa mwajiri basi mtumishi anaruhusiwa kwenda moja kwa moja CMA bila kupita popote sababu CMA ndicho chombo pekee chenye mamala ya kusikiliza migogoro ya kazi/ ajira. Hana local remedy anayotakiwa kuexhaust.

JE, MABADILIKO YA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA MWAKA 2016 YALIHUSU WATUMISHI WOTE?
Jibu ni HAPANA, mabadiliko hayo ya kuwataka watumishi waexhaust local remedies yaliwahusu watumishi wa umma walio katika ngazi ya OPERATIONAL SERVICE, yaani watumishi wasio na digrii. Ili uelewe vyema jambo hili, unatakiwa kusoma Sub Heading ya Kifungu cha 32 na 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma, kimeandikwa (c) Operational Service. Kwa hiyo Mabadiliko ya Sheria mwaka 2016 yaliongeza Kifungu 32A kuwahusu Watumishi wa Umma ambao wapo katka kundi la Operational Service tu na sio wengineo. BAHATI mbaya, Mawakili wa Serikali wamekuwa wakiipotosha Mahakama kwa kuwaambia kifungu hicho kinahusu waumishi wote wa Umma jambo ambalo sio kweli. Wamekuwa wakiweka Mapingamizi ya Kisheria kila mara mtumishi wa umma anapofungua CMA mgogoro usiohusu adhabu za mamlaka ya nidhamu wakimtaa aexhaust local remedies. Majaji na Waamuzi wa CMA nao wamekuwa wakiingia mtego huu wa mawakili wa serikali, labda kwa kutokusoma kifungu husika au kwa kukisoma vibaya. Maofisa ambao sheria ya utumishi wa Umma imewatambulishakuwa ni wale walioajiriwa kwa digrii (shahada) kama ngazi ya mwanzo kabisa ya ajira zao mfano maafisa kilimo, maafisa watendaji wa Kata, maafisa ugavi nk wanaitwa AFISA. Msingi wa kuongeza Kifungu hiki cha 32A ilikuwa ni kuwazuia watumishi wa Operational Service kwenda CMA moja kwa moja kwa kuwa Sheria ya Utumishi wa Umma hiyohiyo kupitia Kifungu cha 32 iliwaelekeza kuwa watumishi hao wanatawaliwa ama wanaongozwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini.
View attachment 1905307

Kwa hiyo, TUME ya Utumishi wa Umma imekwa ikitekeleza jambo amabalo haina mamalaka nalo la kusikiliza malalamiko na kuyatolea uamuzi.
Natumai EINSTEIN112 na wenzako mtakuwa mmenielwa vyema na mmejifunza.

View attachment 1905300
Somo zuri
 
Back
Top Bottom