Mkuu ninauzoefu wa kutengeneza sabuni za mi
che. soko lipo kubwa mmno.kwani viwanda havikidhi mahitaji ndio sababu bado tuna import sabuni.
Machine ya kutengeneza sabuni -Ploder ni milioni7,ya kukata chips milioni1 ,na clutcher ya kupikia sabuni ni around 3millioni,ila unaweza kuanzia kupika ktk mapipa ya lita200(siyo kazi rahisi kutumia mapipa)
hivyo unahitaji around milioni11 kwa ajili ya equipment.
tatizo ni Mali Ghafi. mafuta ya kutengeneza sabuni yanatoka nje ya nchi ,hivyo yanaagizwa na viwanda vikubwa ,viwanda vidogo wananunua kwa dili kutoka kwa madalali.
kuna mafuta ya mise yanatoka mbeya,na kigoma haya ni rahisi ila kama upo dar gharama ya usafiri ni kubwa.\
competitors
Sabuni ya kiwanda kidogo huwa na ubora zaidi ktk maji ya chumvi/kisima ambayo ndio maji yanayotumika na watanzania wengi,sabuni za viwanda vikubwa huwa zimechujwa sana(highly refined and processed oils)hivyo hazifai ktk maji ya visima.
watengeneza sabuni za mikono kutoka kigoma huwa wanamwaga sabuni nyingi ktk soko la DAr ,wanarudi a month later kuchukua pesa,hivyo jiandae kushindania nao.
Viwanda vikubwa sabuni zao zinapendwa mjini e.g Dar,Arusha na Mwanza ambako kuna maji ya bomba,hivyo tarajia soko la mikoani na vijijini,
ili uwafikie hawa wateja inabidi uunde distribution network ya whole sellers,pale manzese kuna maduka ya wapemba ya whole sale ukiwapelekea mzigo wanakulipa hapo hapo,wao huwa wanawauzia watu wanaopeleka bidhaa za maduka mikoani.e.g pruduct yangu nilikuwa siioni madukani in Daresalaam.nilipodadisi nikagundua ipo very popula in Kibaigwa dodoma.so nikisupply mzigo jamaa wanaotoka dodoma hawanunui kitu kingene zaidi hiyo sabuni.
------------------------
kama utafungua kiwanda mitaani na siyo ktk industrial zone e.g pugu road,epza 🙂
jinpange kupambana na TFDA,bora ya TBS
Afisa biashara
TRA
mwen
yekiti wa serikali za mtaa.
Packaging ya product yako ni muhimu sana,ndiyo maana wachina wanauza vitu vyao kwa wingi wao wanajua packaging and presentation nzuri za quality.
kwa sabuni ya mche ni kutengeneza mabox.nenda pugu road kiwanda kinaitwa Commercial printers wao wanabei nzuri na ni wazoefu kwa ajili ya SME s wenye viwanda vidogo.watakufanyia design ya box,inabidi uende na miche yako ili wawe na uhakika wa vipimo vya carton.
kwa ushauri zaidi wa michanganuo ya biashara na faida muone BABALAO atakushauri vizuri zaidi mpaka jinsi ya kupata mkopo. 🙂