Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Sikubaliani nawe kwenye NAFASI KUTANGAZWA. Hakuna kitu fisadi anakipenda kama kutangaza nafasi, na wahusika wagombee au waombe. Kwa sababu Fisadi silaha yake kubwa ni pesa, na wanazo. Kwa hiyo mfumo huo wanauwezo mkubwa wa kupenyeza watu wao na wakawahudumia wao sio wananchi. Kwani hao mawaziri si walichaguliwa na wananchi, huku nafasi za majimbo yakitangazwa. Wakapita kwa kutumia pesa.Imeharibiwa na mifumo ya wizi na kujuana, kwanini huwezi sikia Vodacom, Airtel, Tigo n.K wamefilisika lakini ni mashirika ya umma pekee ambayo yanafilisika pamoja na kupewa ruzuku? kama nafasi zingetangazwa tungepata watu wazuri sn, huu mfumo wa kuteua ndugu na chawa ndiyo ujinga wetu.
China ilitupilia mbali huo mfumo, kwa sababu ukiwa na masikini wengi kama nchi zetu ni balaa tupu. Urusi alicheleweshwa na hayo, sasa wanarudi kule kule.
Leo tunajua bei za ubunge na nafasi nyingine tofauti zinazotangazwa na wenye nia wakaomba.
Narudia msemo wa Nyerere "Watanzania wana majibu RAHISI kwa maswali MAGUMA sana."