Utenguzi: Maharage Chande wa Posta, Ulanga wa TTCL na Justina Mashiba wa UCSAF watumbuliwa

Utenguzi: Maharage Chande wa Posta, Ulanga wa TTCL na Justina Mashiba wa UCSAF watumbuliwa

Asiyemkubali mama akapimwe akili, tulimuona mpole au haelewi kinachoendelea kumbe yupo zaidi ya makini mama ana kura yangu na ukoo wangu
Mimi, nikiwa kama mwenyekiti wa ukoo natamka yafuatayo-kwanza kabisa huruhusiwi kutoa tamko,maagizo,wala kutoa amri yoyote kwa niaba ya ukoo, pili, bado utabakiwa na haki ya kutoa maoni nje ya vikao rasmi vya ukoo,,hata hivyo maoni yako hayatazingatiwa isipokuwa kwa ridhaa yangu tu,tatu, maagizo,maamuzi,amri, na chochote ulichoamua kwa niaba ya ukoo, kuanzia tarehe hii ya leo kitachukuliwa kama null and void,hayatatambulika wala kuzingatiwa na wana ukoo, vilevile, kamati tendaji ya ukoo itakutana haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi dhidi yako.

Mwenyekiti wa ukoo.
 
Tengua teua Wala haisaidii sana nchi kukua kwa kuwa haitoi mwanya watu kuonyesha vipawa walivyopewa na Mungu
Kwamba mtu akiharibu aendelee kuvumiliwa kwa imani kwamba ipo siku ataonesha kipawa?

Mtu akitenguliwa hata chini ya mwezi tangu ateuliwe ni sawa tu as long as kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.
 
Hapa kuna mchezo tunachezewa wa kisaikolojia. Hawa matapeli wana ajenda yao ya Siri.

Nape na makamba jr hawajatolewa kwasababu za kiutendaji wametolewa ili waanze kuingia mtaani kufanyia utekelezaji zoezi la kutengeneza kura kwaajiri ya uchaguzi ujao.
Kwamba wangebaki na mamlaka yao wangeshindwa kufanya hiyo kazi huko mtaani!!???
 
View attachment 3050179
View attachment 3050203
View attachment 3050205
View attachment 3050206
Mie namtengua wewe unamwambia asante na shukurani, unajifanya kiziwi kama chura eeh!
Kule Kenya Ruto alipovunja baraza la mawaziri, mawaziri karibu wote walimshukuru mheshimiwa raisi kwa kuwapa heshima ya kutumikia nchi yao, na hakuna taasisi au shirika liilowapongeza mawaziri waliotenguliwa, kwetu imekuwa kinyume anapongezwa waziri aliyefutwa kazi, hapa ndipo tulipofikia waziri anapofanya taasisi au mashirika yaliyo chini yake,kama SACCOS zake binafsi,hizi teuzi za wakurugenzi wanakuwa na mikono yao,kiasi kwamba wanafanya wanavyotaka kwenye hizi taasisi au haya mashirika, mawaziri wamekuwa miungu watu kwenye taasisi zetu, Nape ni mfano tu wa mauzauzza tuliyonayo kwa wateule wetu, wameweka mizizi kwenye taasisi zilizo chini yao, si ajabu wamekuwa na ukwasi mkubwa ono kupienia nafasi zao. Sote tunakumbuka miada ile mawaziri fulani walipokuwa na bendi zao za muziki walizianzisha wakiwa mawaziri,walipokosa tu uwaziri bendi zikafa na sasa tuna wamiliki wa timi za mpira,wakikosa kuteuliwa hizo timu zitakufa baada ya wiki moja tu,huku ndiko tulikofikia,hatimaye viburi na dharau kutamalaki, na lugha za dharau kuibuka, utawasikia asiyetaka ahamie Burundi, wazuri hawafi, Mungu kaamua...hizi ni kejeli kutuka kwa waliovimbiwa na kulawa madaraka na tunaendelea kuwaangalia tu mwishoni dharau zinahamia hata kwa yule aliyewapa madaraka.
 
Ubaya wake, jitu likiingia madarakani likijua litatenguliwa muda wowote, litaiba kwa pupa sana. Ni ngumu kutenda kwa uzalendo akijua muda wowote nyasi zinaota. hasa jamii ya mtu mweusi.


JESUS IS LORD&SAVIOR

Tuwachunguze na ikibainikq mkondo wa sheria uchukue nafasi..Hakuna alie juu ya sheria..
 
Upumbavu wake uko wapi? Kusema ukweli ndo umwite mpumbavu? Kama unanufaika na hii tabia ya kutengua wa bara tu, kaa kimya. Wengine inatuumiza, tumeamua kusema.
Nasema aache upumbavu kwasabu hiyo roho ya KIBAGUZI Ni sawa na kula nyama ya mtu, wenzetu south Africa haya mambo yaliwagarimu sana halafu anatokea mpumbavu mmoja anaanza kuleta roho ya KIBAGUZI na hapa kwetu, tunaomba bwana benjamin netanyau UTUKOME!
 
Maza ana hasira balaa, huwezi kuona amegusa wateule wa Zanzibar na Pwani
Hapo hakuna uzanzibari.
Mh.Samia anaondoa mchwa wote wanaokula mbao za samani za nyumba nzuri iitwayo Tanzania.
Anaweka utiifu kwa mamlaka siyo kwa watu binafsi.
JF Ina nguvu Sana. Ikikusagia kunguni tu huchomoi ni mwendo wa kusubiria siku na saa hata ipite miaka miwili utafikiwa tu.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu MkuuKiongozi Balozi Dk.t Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:-

1. Bi Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

2. Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Bw. Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.

3. Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Bi. Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

View attachment 3050160
Pia soma; UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL
Hii ndio kazi pekee anayoiweza vizuri 😂😂.
 
Sijui kama kuna uhusiano na hizi screenshots zinazozunguka mtandaoni🤷🏾‍♂️ but anyway, kama kuna wakati Mheshimiwa Rais amekonga nyoyo na matarajio ya watu kwa furaha, basi ni sasa. She’s literally won a full mass support.
af39538a-7429-492c-af54-18a56f94704d.jpeg
ae318cac-2142-4e54-9dc3-bc877881f843.jpeg
 
Hakuna cha mchezo. Atulie afanye kazi na aachane na personalities.

Kumtumbua mtu kwa kumshukuru aliyetoka sio sahihi! Hizo ni roho za kishetani na zinakuonesha kuwa you are not competent.

Kuna shida mahali. It's either anazungukwa na watu ambao sio sahihi au she is incompetent.

Hili la kubadili wakuu wa TISS 4 in 3 years tu ni a very serious red flag.

Samia atulie. Anajipa pressure unnecessary!
Wewe ni Mh January au Nape? 😂😂
 
Safi sana fagio linaendelea kupita👇👇
---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:-

i. B.i Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

ii. Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Bw. Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.

iii. Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Bi. Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Hivi hawa watu wakitenguliwa, na mishahara yao huwa inatenguliwa au ndo ile kanuni kwamba mshahara huwa haushuki hata ukitenguliwa?!
 
Hii tabia ya kurudiarudia alichoweka mwenzako na tayari kishawekwa na kimeshasomwa na watu wanajua na wameelewa ni dalili ya Uzwazwa A.K.A utaahira
 
Hivi hawa watu wakitenguliwa, na mishahara yao huwa inatenguliwa au ndo ile kanuni kwamba mshahara huwa haushuki hata ukitenguliwa?!
Kama alikuwa mtumishi wa Umma ,salary itabakia pale pale.

Wazo la kutengua na kupunguziwa salary liliwahi letwa na Mwigulu ila likaishia hewani
 
Back
Top Bottom