Yeye na boss wake walitakiwa kua jela. Hasara walizoingizia taasisi za umma walizokua wakiongoza hazielezeki.
Ni mabingwa wa kuanzisha miradi isiyo na kichwa wala miguu ili wapige 10% waondoke.
Chande na Makamba wakiwa Tanesco walianzisha miradi hewa inayoitwa Grid Imara, wakatangaza tenda 30 ndani ya mwaka mmoja za zaidi ya trilioni 4. Wakasaini mikataba wameacha wakandarasi hawajalipwa hata 10 kwa sababu serikali imeshindwa kuendana na mahitaji makubwa ya kuwalipa wakandarasi 30 kwa wakati mmoja wa umeme ambao wanadai zaidi ya Trilioni 4.
Makamba hakuishia hapo, akahamia mambo ya nje, akaanzisha mradi wa ujenzi wa vitega uchumi kwenye balozi zetu Duniani kote eti ili tuwe tunapangisha huko tunapata fedha, nia yake ni apate 10% ya watu watakapoewa tenda ya ujenzi wa hayo majengo ale aondoke.
Mama asiishie kuwatumbua tu, wafikishwe mahakamani pia.