Utenguzi: Rais Samia ametengua Uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba

Utenguzi: Rais Samia ametengua Uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba

Alionesha udhaifu wa kiuongozi jukwaani. Waziri ikabidi amuombe radhi yeye badala ya kumuombea radhi.

Wakati anahutubia aliletewa kimemo na mtu mmoja pale jukwaani. Akakereheka akafedheheka akakitupa kile kimemo na kuzira kuendelea na hotuba akisema wasimletee utani utani. Inaonekana kimemo kimetoka kwa Waziri labda

Nadhani kushindwa kwake kujidhibiti ama kudhibiti hasira kumepelekea rais kuondoa imani kwake
Ndicho kilichotokea, na yale maneno ya aweso alipopanda jukwaani ndio yakamaliza kabisa.
 
Ndicho kilichotokea, na yale maneno ya aweso alipopanda jukwaani ndio yakamaliza kabisa.
Kimemo kimeenda kubonyeza panic button kwa Katibu Mkuu kisha Mwanasiasa akaja kugongelea jeneza for exit
 
Aweso effect.
Hata huyo nae, hadi leo kashindwa kuleta maji hata hapo karibu Mwanza, palipo na ziwa Victoria tu, bali wamebakia na ' mbambamba' za ahadi tupu za kisiasa huku wananchi wanaendelea kutaabika Kwa karaha ya shida ya maji.....kazi kwelikweli.
 
Hiyo imekuja kuhitimisha ya nyuma. Huyo mama ana dharau, hasira na kiburi sana. Hashauriki wala kumsikiliza mtu hata kwenye jambo lenye tija. Hapaswi kupewa mamlaka makubwa ya kuongoza watu.
 
Inaonekana hapo kazini kwake kuna hali ya kutokuelewana na wenzake,hii inaweza kuwa linatokana na tabia zake mwenyewe au kuna figisu zinafanyika na wengine kwahiyo yuko defensive kila wakati....
 
Hiyo imekuja kuhitimisha ya nyuma. Huyo mama ana dharau, hasira na kiburi sana. Hashauriki wala kumsikiliza mtu hata kwenye jambo lenye tija. Hapaswi kupewa mamlaka makubwa ya kuongoza watu.
Kaolewa?
 
Dharau mbaya sana ukidharau hata walio chini yako na walio juu yako zaidi hata wewe kama uko juu kidogo wanakushusha kiulaini.
Nitoe mfano ukiwa manager wa shamba ukawa unawadharau vibarua wanaopanda mahindi wanachokifanya zile mbegu wanazichemsha kisha huku umeshika kiuno unawaambia nyie wapumbafu fanyeni kazi.Kwa watu wa kanda ya ziwa wanakuambia nahene mayo.
Baada ya mwezi hakuna mbegu inaota anakuja boss wako mkuu anakutumbua umechukua mbegu mbaya labda ulikula mlungula.
Tuchunge sana midomo yetu kwa waliojuu yetu kivyeo na walio chini.
Aliyetoa methali ukubwa ni jalala hakukosea.Ukiwa kiongozi unatakiwa kuwa na kifua kipana sana cha kumeza lawama ujue kusamehe ukiombwa radhi kubali.
Kuna yule alikuwa waziri flani hivi wa mambo ya ughaibuni naye akawa sikio linataka kukua kuzidi kichwa akatumbuliwa asubuhi kabla ya saa nne.
Nadhani watu wa kanda ile flani ya misifa wajitafakari.
 
Hata huyo nae, hadi leo kashindwa kuleta maji hata hapo karibu Mwanza, palipo na ziwa Victoria tu, bali wamebakia na ' mbambamba' za ahadi tupu za kisiasa huku wananchi wanaendelea kutaabika Kwa karaha ya shida ya maji.....kazi kwelikweli.
Tatizo la Mwanza ni miundombinu mibovu ya usafirishaji Maji! Maji mengi yanamwagika Mtaani!
 
Back
Top Bottom