TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI NA TIBA YAKE.
By Dokta Mathew
Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la tatizo la uvimbe kwenye kizazi kwa akina mama ama wanawake wengi.
Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la uzazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi (ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.
Kuna aina tatu za fibroids:
1.Submucosal fibroids (ndani ya kizazi)
2.intramural fibroid (ndani ya nyama za kizazi)
3. Subserosal (nje ya kizazi)
Ni watu gani wenye hatari ya kupata fibroids
1. Mwanamkehajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa
2. Miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma
3. Kurithi
4. Uzito wa juu au Unene
5. Kuingia hedhi mapema
Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani
vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda
makazi ya mtoto.
Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma.
Dalili za fibroids
1.Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi.
2. Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya au ambao hauna harufu lakini mwingi na mweupe.
3. Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe, wengi hupata maumivu makali sana.
4.Tumbo kuuma sana chini ya kitovu.
5. Hedhi zisizokuwa na mpango
6. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
7. Kukosa hamu ya tendo la ndoa
8. Maumivu makali wakati wa hedhi
Uvimbe unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo.
1.Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo
2.Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo (U.T.I isiyokoma)
3.Haja kuwa ngumu
4. Miguu kuvimba
5. Kupungukiwa damu
Jinsi fibroids zinavyoweza kuzuia kupata mtoto:
1.Fibriods zikikua sana zinakandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye kiwanda yaani ovaries
2.Uvimbe pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi, hasa submucosal fibroids
3. Pia huzuia mfuko wa kizazi kukaza kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.
______
Tunakuhakikishia kuwa na afya njema zaidi ukiitunza na kuihudumia afya yako kwa vyakula na bidhaa za tibalishe daima.