Habari hii iwafikie wote wanaokodolea macho nafasi za uongozi.
Ifahamike kuwa bila tume huru hakuna uchaguzi.
Hatutaangalia mgombea ni mwanamke au mwanaume. Haki zetu za binadamu hazitakuwa na mbadala.
Kama ni mtarajiwa atuambie atafanya nini kuondoa kadhia kama hizi:
Kama alikuwamo madarakani atwambie alifanya nini kuondoa kadhia kama hizo.
Kutesa watu, kuteka watu, kuuwa watu au kuwashikilia watu bila kujulikana walipo kinyume cha utashi wao ni kinyume cha sheria na kinyume cha haki za binadamu.
Tutahitaji kujua wako wapi wote waliopotezwa na dola.
Tutahitaji kujua yuko wapi Moses Lijenje. Tutahitaji kujua alipo Luteni Dennis Urio na kwa nini kama yupo anashikiliwa na kuteswa huko aliko.
Aghalabu hao ni kwa kuanzia kwani orodha yote ya waliotoweka itakuwapo.
Uongozi siyo udhwalimu.
Tunayo haki ya kuishi nchini mwetu kwa furaha itokanavyo na uwepo wa uhuru, haki, usawa na demokrasia.