Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Utetetezi wa Sabaya, haupo kisheria, na pia unavunja kanuni za Kijasusi

Angejiteteaje kwa mfano? Umetumwa na wakuu wa nchi lkn wakati wa matatizo wamekaa kimya wanendelea kupiga kampari tu. Lazima nao wajulikane kuwa ndio waliokuwa wakituuwa.

Da ila inasikitisha sana, kuwa awamu ya tano ya serikali ya Tz badala ya kulinda usalama wa wananchi wake serikali ndo ikawa inatengeneza vikundi vya uarifu! Da hìi hatari sana. Lkn Mungu fundi.
Kaona waliomtuma wameuchuna. Akaamua kujilipua kama Mbwai na iwe Mbwai
 
Wanasheria wake ni wapumbavu sana, Ila kesi kama hiyo anaweza kujiteteaje jaman? Ni jambo lisilowezekana kabisa! Ashafungwa huyo!

Sema anamrahishia Hakimu kumhukumu, wakati mwingine hakuna haja ya kujitetea, unakuwa kimya tu kabisa bila kusema lolote!

Akipewa Backup anachomoa
 
Eti kanuni za kijasusi..,unafanya ujasusi nchi kwako mwenyewe wkti ww ni mtawala tena wa juu kbsa😂😂
 
Eti kanuni za kijasusi..,unafanya ujasusi nchi kwako mwenyewe wkti ww ni mtawala tena wa juu kbsa😂😂

😃😃😃

Ndivyo anajaribu Kuieleza Mahakama.

Sasa anapaswa aiambie Mahakama mbali na kazi yake ya UDC alikuwa na kazi gani nyingine hata Kama ni yasiri, maana keshaanza kuongea ambayo huenda yangekuwa yasirini.

Yaani ukishasema kazi maalumu moja Kwa moja ukawaambia watu wewe ni mtu wa kitengo
 
Amejieleza vizuri na kwakuwagusa wakubwa watashtuka na kutafuta namna ya kuimaliza kesi juu kwa juu! Wanajua wanaweza hitajika mahakamani kwa ushahidi na kwao hiyo in fedheha kubwa!! Ndotudai katiba mpya maana MTU mwenyekinga anatuma watu operesheni za kigaidi alafu eti hatakiwi kushtakiwa.
Waendelee kumweka ndani ili tuujue ukweli wrote kumbe hata yule wa Dar alitumwa pia na wanamirembe
 
Ataambiwa atoe ushahidi na sio maneno matupu/porojo zake.

Akitoa ushahidi hiyo inaweza muweka pazuri.
 
Amejieleza vizuri na kwakuwagusa wakubwa watashtuka na kutafuta namna ya kuimaliza kesi juu kwa juu! Wanajua wanaweza hitajika mahakamani kwa ushahidi na kwao hiyo in fedheha kubwa!! Ndotudai katiba mpya maana MTU mwenyekinga anatuma watu operesheni za kigaidi alafu eti hatakiwi kushtakiwa.
Waendelee kumweka ndani ili tuujue ukweli wrote kumbe hata yule wa Dar alitumwa pia na wanamirembe

Katumia mbinu ya Prof Mahalu.
 
Kwa hiyo mpaka sasa inaonekana yupo pekeake, anatumia utashi wake kujibu maswali, si ndivyo?

Unajua Magufuli aliamua kuiba uchaguzi bila aibu, kama Hii itakuwa mbinu ya kumtoa ni sawa, maana Hakuna sana!

ILA ili Sanaa iwezekana lazima kuwe na maandalizi, Mfano angemtaja Magufuli akawaacha waliopo etc!

Huu utopokaji ni ngumu sana kumtoa kwa Sana’a, labda umtoe kwa mabavu bila kujali mijadala, and it so, kwa nini umpeleke mahakaman ili waje mtoa Kizembe
 
Ni Sawa.

Kama Hakuwa na urafiki mzuri na wakubwa sidhani Sana.
Atapambana kivyake, sheria imuokoe
 
Sabaya ni mjinga pamoja na nguvu zake na ukatili wake lakini akili yake finyu.

Hii kesi yake ilikuwa ni spinning tu na publicity stunt kuonesha kwamba Utawala uliopo unaondoa makandokando yaliyolalamikiwa nyuma. Lakini yeye nadhani hakuwa briefed na huyu ilikuwa anachomokea mahakamani lakini kwa sababu akili yake ndogo kaanza kubwabwaja. Lakini sababu ni jamhuri huyu atatoka na ataachiwa.

Hili limedhirisha kwamba yale ya kukusanya kodi kwa taskforce za kibabe, mamalaka kutumia nguvu kubana wananchi hii sio misingi ya demokrasia na wananchi tutaendelea kuhoji nafasi za ma dc uhalali wake haswa kuendelea kuwepo ili hali tunahitaji kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kuinua uchumi wetu. # Katibampyahaikwepeki # Katibailiyopoikufutwaingesaidia
 
Unajua Magufuli aliamua kuiba uchaguzi bila aibu, kama Hii itakuwa mbinu ya kumtoa ni sawa, maana Hakuna sana!

ILA ili Sanaa iwezekana lazima kuwe na maandalizi, Mfano angemtaja Magufuli akawaacha waliopo etc!

Huu utopokaji ni ngumu sana kumtoa kwa Sana’a, labda umtoe kwa mabavu bila kujali mijadala, and it so, kwa nini umpeleke mahakaman ili waje mtoa Kizembe

Generali Ulimwengu juzi kati alizungumzia sifa ya kuijua nchi kwa anayepewa madaraka. Achutame tu hajachelewa. Heri ya nusu shari.
 
Mambo ni Moto

Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.

Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.

Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate

Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.

Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.

Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.

Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.

Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.

Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.

Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.

Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.

Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.

Robert Heriel
Labda huwezi jua msema kweli ni__
 
Sabaya ni mjinga pamoja na nguvu zake na ukatili wake lakini akili yake finyu.

Hii kesi yake ilikuwa ni spinning tu na publicity stunt kuonesha kwamba Utawala uliopo unaondoa makandokando yaliyolalamikiwa nyuma. Lakini yeye nadhani hakuwa briefed na huyu ilikuwa anachomokea mahakamani lakini kwa sababu akili yake ndogo kaanza kubwabwaja. Lakini sababu ni jamhuri huyu atatoka na ataachiwa.

Hili limedhirisha kwamba yale ya kukusanya kodi kwa taskforce za kibabe, mamalaka kutumia nguvu kubana wananchi hii sio misingi ya demokrasia na wananchi tutaendelea kuhoji nafasi za ma dc uhalali wake haswa kuendelea kuwepo ili hali tunahitaji kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kuinua uchumi wetu. # Katibampyahaikwepeki # Katibailiyopoikufutwaingesaidia

Umeongea ukweli kabisa.
 
Ole sabaya hakuna aliyemtuma kufanya upuuzi wake. Ajitetee bila kuhusisha wengine japo tunajuwa marehemu alikuwa mpuuzi kwa mambo mengine.
 
Back
Top Bottom