Jamani naomba tutende haki mleta thread ameleta changamoto, sheria jamani zinachanganya sana na zina double standard kwa mujibu wa CPA mtoto ni yule ambaye hajafikisha miaka kumi na sita, lakini wakati wa kupinga kura sheria inasema mtu mzima ni above 18yrs, this is contraversal laws, lakini miaka haiondoi kosa la kubaka hata siku moja hata mkeo unaweza kumbaka, lakini wasanii wasimhukumu Lulu kwani hiyo si kazi yao kama wanataka kutenda haki basi inabidi washiriki kumnasua Lulu hata kwa kumuwekea wakili mahiri lulu, kwani naye mchango wake ni mkubwa katika jamii na bado tunauhitaji kama alivyo mwendazake, kitu alichofanya Lulu ni self defence, kumbuka mdogo wa kanumba aliitwa na Lulu kutoa msaada kwa kaka yake hii ni dhahiri hakuwa na nia ya kuua hata polisi Lulu alienda mwenyewe wala hakukamatwa. Hivi hebu tujiulize kama Lulu angezidiwa nguvu ingebidi afe yeye sijui wasanii wa filamu ndio wangefurahi.