The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Kwa ufupi:
Kauli na hoja za Paul Makonda na majibu yake:
HOJA #1: Tundu Lissu ni mchanga kwake (Makonda) kisiasa. Kauli hii ina ukweli wowote?
JIBU: ➡Ni mwongo, mzushi. Tundu Lissu yumo ndani ya siasa (active politics) tangu mwaka 1995 na mwaka huo aligombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki, kwao. Wakati huo Paul Makonda akiwa kijijini Kolomije wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza akiwa bado anasoma Shule ya Msingi akiwa na jina lake halisi la Albert Bashite Malyangili
➡Paul Makonda ameanza kujulikana mwaka 2014 kwa kutenda tukio baya la kumpiga mzee Joseph Warioba ndani ya ukumbi wa Ubungo Plazza, DSM wakati kongamano la mjadala wa katiba mpya lililoandaliwa na iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba wakati huo Tundu Lissu tayari ni mbunge.....
HOJA #2: Paul Makonda, "sihusiki na tukio la kuvamiwa kwa Clouds TV". Kuna ukweli kwenye hili?
JIBU: ➡Ni mwongo na mzushi. Picha za CCTV zinamuonesha wazi yeye kwa sura yake akiingia na kufanya vurugu ndani ya studio. Aidha askari alioambatana nao wakiwa na bunduki za kivita, baadaye ilikuja kujulikana kuwa ni miongoni mwa walinzi wa kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais John P. Magufuli wakati huo...
➡Askofu & Mch. Josephat Gwajima aliyekuwa mlengwa wa sakata hilo la udhalilishaji pamoja na waandaji wa kipindi ambacho alikuwa anataka kwenda kukitumia kurusha video clips zake wanathibitisha kuwa ni yeye katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari kwa nyakati tofautofauti.....
➡Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari wakati huo Ndugu Nnape Moses Nuye kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha bila shaka ushiriki wake na ikamtia hatiani. Kwa sababu boss wake wakati huo (Hayati Rais Magufuli) alikuwa ni mshiriki mwenzake kwenye uovu na uhalifu huu, Nnape Nauye - Waziri wa Habari by then, alipoteza uwaziri wake ktk namna ya kudhalilishwa vibaya sana ikiwemo kutishiwa na kunusurika kupigwa risasi. Sababu ni kwanini aliweka wazi taarifa hiyo iliyokuwa inam - incriminate Paul Makonda kwenye uhalifu huo...
NOTE: Ili ufaidi na kupata taarifa zaidi, fungua hiyo video na tazama na sikiliza uchambuzi huo kwa makini hadi mwisho kisha toa maoni yako