Utetezi wa RC Paul Makonda RC juu ya ushiriki wake kumpiga risasi Lissu, kuvamia Clouds TV

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267
Your browser is not able to display this video.

Kwa ufupi:

Kauli na hoja za Paul Makonda na majibu yake:

HOJA #1: Tundu Lissu ni mchanga kwake (Makonda) kisiasa. Kauli hii ina ukweli wowote?

JIBU
: ➡Ni mwongo, mzushi. Tundu Lissu yumo ndani ya siasa (active politics) tangu mwaka 1995 na mwaka huo aligombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki, kwao. Wakati huo Paul Makonda akiwa kijijini Kolomije wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza akiwa bado anasoma Shule ya Msingi akiwa na jina lake halisi la Albert Bashite Malyangili

➡Paul Makonda ameanza kujulikana mwaka 2014 kwa kutenda tukio baya la kumpiga mzee Joseph Warioba ndani ya ukumbi wa Ubungo Plazza, DSM wakati kongamano la mjadala wa katiba mpya lililoandaliwa na iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba wakati huo Tundu Lissu tayari ni mbunge.....


HOJA #2: Paul Makonda, "sihusiki na tukio la kuvamiwa kwa Clouds TV". Kuna ukweli kwenye hili?

JIBU
: ➡Ni mwongo na mzushi. Picha za CCTV zinamuonesha wazi yeye kwa sura yake akiingia na kufanya vurugu ndani ya studio. Aidha askari alioambatana nao wakiwa na bunduki za kivita, baadaye ilikuja kujulikana kuwa ni miongoni mwa walinzi wa kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais John P. Magufuli wakati huo...

Askofu & Mch. Josephat Gwajima aliyekuwa mlengwa wa sakata hilo la udhalilishaji pamoja na waandaji wa kipindi ambacho alikuwa anataka kwenda kukitumia kurusha video clips zake wanathibitisha kuwa ni yeye katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari kwa nyakati tofautofauti.....

➡Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari wakati huo Ndugu Nnape Moses Nuye kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha bila shaka ushiriki wake na ikamtia hatiani. Kwa sababu boss wake wakati huo (Hayati Rais Magufuli) alikuwa ni mshiriki mwenzake kwenye uovu na uhalifu huu, Nnape Nauye - Waziri wa Habari by then, alipoteza uwaziri wake ktk namna ya kudhalilishwa vibaya sana ikiwemo kutishiwa na kunusurika kupigwa risasi. Sababu ni kwanini aliweka wazi taarifa hiyo iliyokuwa inam - incriminate Paul Makonda kwenye uhalifu huo...


NOTE: Ili ufaidi na kupata taarifa zaidi, fungua hiyo video na tazama na sikiliza uchambuzi huo kwa makini hadi mwisho kisha toa maoni yako
 
UCHAFU MTUPU SIJUI UNAANDAIKA NA KUFIKIRIA KWAKUTUMIA NINI?MATOPE KICHWANI
 
Hata kumuita mkuu wa mkoa naona kama tunakosea. Huyu anapaswa kuitwa "mkuu wa mauaji"
Hii ndiyo sura, picha ya uhalisia wa viongozi karibu wote wa serikali...

Karibu wote wana mapungufu makubwa ya kimaadilI. Lakini ni bahati kuwa hawa ndio wamepewa dhamana ya kuiongoza nchi na taifa hili...

Tunapokuwa na viongozi wanaoweza kutumia rasrimali za nchi kuitisha kongamano la gharama kubwa kama hili ili kwenda kusema uongo na uzushi, tutegemee nini kama taifa..??
 
Asante kwa maoni yako..

Hata hivyo, jiangalie na kujichunguza wewe kwanza...

Kwani kwa kauli yako hii, haina shaka kuwa wewe huyo ndiye uchafu wenyewe halisi...!!
ACHA UJINGA YAANI WATU NA AKILI ZETU TUKUSIKILIZE WEWE UNAYEONGEA UCHAFU HUMU?
 
Waaandishi wa habari najua mpo humu swali langu kwenu n hili, hivi huyo Makonda ana uspecial gani mpaka mna mpa political mileage iliyopitiliza kuwazidi maRc wa mikoa mingine?
Kuanzia background yake ya kielimu imejaa utata utata mtupu ilitosha umma umtilie mashaka makubwa hyu mtu.

Waandish wetu mngekuwa na akili timamu ilitakiwa muichimbe Kwa undani Historia yake Kwa kinna ametokea wapi na amefikaje fikaje hapo.

Hii nchi kuna maRc wachapa kazi wazuri mf. Mtaka,Homero e.tc lkn nyie waaandishi wetu vilaza wenye njaa kila siku mpo bize na huyo Kilaza mwenzenu a confused fellow,opportunist,sadist,big headed,mwenye dharau na kiburi.
 
ACHA UJINGA YAANI WATU NA AKILI ZETU TUKUSIKILIZE WEWE UNAYEONGEA UCHAFU HUMU?
Mtoa mada amesema ukweli. Tundu Lissu ni mtu mzito, na mzoefu, amejulikana tangu wakati wa Mzee Mwinyi, na Mzee Mkapa. Wakati Lissu akitetea wananchi wa Rufiji delta, Makonda huenda alikuwa shule ya msingi. Kwa kifupi Makonda amesema uongo na mtoa mada yuko sahihi kutoa angalizo.
 
Makonda anatakiwa atulie afanye vitu vingine aache kujitetea kiuongo uongo vitu ambavyo alivifanya hapo nyuma ili tuendelee na mambo mengine.
 
Makonda anatakiwa atulie afanye vitu vingine aache kujitetea kiuongo uongo vitu ambavyo alivifanya hapo nyuma ili tuendelee na mambo mengine.
 
Makonda anatakiwa atulie afanye vitu vingine aache kujitetea kiuongo uongo vitu ambavyo alivifanya hapo nyuma ili tuendelee na mambo mengine.
 
Ndugu promethus, huyu jamaa ndiyo hirizi na nyundo ya uovu wa serikali na CCM hii..!

Hao ma - RCs wengine hutawaona waki trend kwa kuwa hawana access na mafungu ya pesa ya kufanyia uovu na uhalifu ili kuilinda CCM na serikali iliyoko madarakani..

Huyu jamaa alikaa bench (nje ya mifumo ya kichama & kiserikali) kwa takribani miaka mi2 au 3 tangu "Lord-Master" wake John Pombe Magufuli alipokufa...

Baada ya misukosuko na kashkash za critics wa CCM na serikali kuwa nzito, "mwana wa uovu mkuu" ilibidi aitwe kazini ili mbinu za siasa za kimafia zilizotumiwa na Magufuli kati ya 2016 - 2021 huku miongoni mwa waratibu wake wakuu akiwa Paul Makonda ilionekana ndizo zinazohitajika zitumike tena kuikoa serikali na CCM kwa ujumla...

Mwana wa uovu ndiyo huyo. Yuko kazini. Mtazame tu kwenye video yake ya kwenye mkuano wake huo alioutisha huko Arusha....

Jamaa ana macho makavu, amejaa ujasiri wa kiovu na ukatili mtupu, mwongo na mzushi wa waziwazi asiye hata na kumbukumbu nzuri kujua alikotoka na aliyofanya huko nyuma...

Huyu amebeba sura na tabia za shetani mwenyewe halisi: Hana hata chembe ya haya wala aibu, amejaa ujasiri wa kiovu, uongo, uzushi, unafiki na menginr yafananayo na hayo
 
Hakika mkuu umenena.
Binafsi nimewadharau mno waaandishi waliohudhuria huo mkutano kama sio nguvu ya pesa na wamefanya Kwa utashi wao bhasi nchi hii ina matatizo makubwa mno.
 
UCHAFU MTUPU SIJUI UNAANDAIKA NA KUFIKIRIA KWAKUTUMIA NINI?MATOPE KICHWANI
Ni jambo moja tu lililo niingia akilini baada ya kusoma uliyo andika wewe. Maslahi yako na Makonda ni yapi hasa!
'Mihapase'..., inabidi nianze kuwatambuwa kundi hili linalo shirikiana na mtu mwovu huyu.
 
Makonda amekosea sana kusema uongo, na kuzusha, katika mambo ambayo jamii inauelewa nayo. Hakutakiwa kudanganya kuwa eti hakuvamia studio za Clouds. Hakutakiwa kudanganya kwamba Lissu alisababisha Chadema ikose kura 2020 wakati kila mtu anajua uporaji uliofanywa na serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…