Hiki ulichokiandika kimemili katika falsafa zaidi kuliko uhalisia. Yaani umejibu swali bila kujua wazo ni nini, hii imekupekea kukosea katika kujibu swali.
Hujaonyesha mimi nawezaje kuwa wazo ? Mimi ni nafsi ambaye nimeundwa au ni mjumuiko wa roho na mwili.
Labda tujadili kwanza maana ya tamko wazo. Sababu hiki mnachokiandika kwanza ni matumizi mabaya ya tamoo wazo, kwa maana lugha inakataa matumizi haya ya tamko hili wazo kulipa sifa za uhai yaani kiumbe chenye akili.
Naomba utusaidie au unisaidie kitu kimoja, naomba unipe maana ya tanko "Wazo".
Wazungu wana msemo unasema: Let us not get caught up in semantics.
Na hata kama kungekuwa na tafsiri rasmi za hivi 'vitu' vilivyo katika hali za ki-wazowazo bado lazima tutapwaya kwa sababu sio vitu. Vitu kama akili, utambuzi, wazo, idea, concept havikamiliki bila kupelekea circular reasoning kadha wa kadha.
Moja kati ya vitu hatujavitafsiri vizuri ni akili/intelligence na utambuzi/consciousness hivi ndivyo ninavyovizungumzia kila ninaposema wazo hai. Katika kuichambua na wenzangu tukakuta kuna nishati fulani inayopower mawazo yaliyo katika hali hiyo. Ni kama entity moja tu hivi.............. ndicho kinachozungumziwa humu.
Kwani nikikuuliza unaposema wewe ni nafsi- hicho 'kinafsi' kipo katika hali gani? Hata roho nayo ipo katika hali gani? Nikisema vipo kiwazowazo roho ikiwa in essence wazo pure toka kwa Mola na nafsi ikiwa ni wazo hai unaloendelea kulijenga kwa mchakato unaoitwa kuishi na kuwa 'being'. Hapo vipi?
Hapa itabidi unipe ushahid au kuonyesha wapi falsafa imekusaidia kuujia ukweli na uhalisia. Maana yake ingekuwa hivyo basi kina Plato, Socrates, Aristotle, Pythagoras wote wangepatia katika kuelezea chanzo cha ulimwengu na maisha, au wana Atomu kadhalika.
Nachokijua mimi kuhusu falsafa na Wanafalsafa ni kuwa walikuwa na maswali sahihi ila walikosa njia za kuwapa majibu sahihi.
Philosophy faster definitions: Tafsiri za harakaharaka😂😂
1. the study of the fundamental nature of
knowledge, reality, and existence, especially when considered as an academic discipline.
2.a theory or attitude that acts as a guiding principle for behaviour.
Waliotutangulia wakubwa ikiwamo mitume na manabii wamekuwa wakituelekeza elimu ya uhalisia upojepoje - moja kati ya tafsiri ya wanafalsafa.
Popote ninapoona mtu anajaribu kuuelewa ukweli wa uwepo wetu ulivyo naona anatumia falsafa, kuna muda tunakosa vipande fulani vya ukweli basi Mola anatupatia mafunuo kuzikamilisha falsafa zetu tunazoendelea kujifunza. Inaweza kupitia kwa Roho mtakatifu aliye ndani yako, kupitia mtu mwingine ambaye tutamuita nabiy/mtume.
Falsafa ikimtambua Mungu hiyo huitwa dini [my take hii sentensi ya mwisho]