Kijana rejea wewe uliye kosea kunukuu nilichokiandika.
Kijana hapa hatuongelei kudai hata wewe leo hii unadai ya kuwa Mola hayupo, lakini je ni kweli Mola hayupo ? Jibu ni kinyume chake. Sasa sisi tunautafuta ukweli na kutaka kumjua mkweli ni naniz ndiyo maana nikasema huko awali bila mitume kuwepo watu wangedai kila wanachokidai na kukaliwa kimya. Kwahiyo hata weseme wao ni wakweli swali je ni wakweli kweli au kinyume chake ?
Sasa kijana naona unaniletea stori na hujibu maswali yangu ya msingi. Chimbuko la Ukristo wenyewe wanadai ni Yesu, je kweli wanayo yadai na kuyaamini ya kweli yanatoka kwa Yesu ?
Sasa hizo hatua unazo sema ndiyo zimeelekezwa na Yesu au ni maoni yao binafsi ? Sasa usipoteze muda kwenye hakuna, sababu hata misingi nayo ina marejeo yake.
Hakuna mahali nimeelezea Biblia kwa kufata misingi ya Qur'aan, nimeelezea namna sahihi ya kuujua ukweli kwa mujibu wa uhalisia na kufata elimu za uhakiki wa habari, misingi ambayo pia ilitumika kujua ukweli juu ya yale ambayo watu walikuwa wanasema yametoka kwa Mtume. Kwahiyo usiandike ambacho sijakifanya.
Kwahiyo kukiri kwao kuwa ni cha kweli hakutoshi mpaka waonyeshe huo ukweli ambao wanaukiri.
Biblia wenyewe Wakristo wanasema ina vitabu 72 wengine wanasema 73 kwa kumbukumbu zangu, na humo zimo habari za Yesu na wenginez mpaka kuna kumbukumbu la Torati na vitabu vinginez usahihi wa hivi vitabu lazima uhakikiwe. Siyo kudai tu ya kuwa kitabu fulani ni cha kweli oasi na kuonyesha huo ukweli wenyewe.
Bado una ubishi wa kizamani hata ukirekebishwa mahali ulipokosea bado unajitia ujuaji
Usi flip hoja, hoja sio Mungu hayupo hapa nazungumzia imani labda kama unataka kusema imani ni madai (jambo ambalo hata uislamu utabidi uhusike)
N kwa kuweza kujua ni wa kweli kwanini usiangalie katika hizo nia walizozisema wao uone kama hazikuleti kwenye jibu la kweli?
Kwanini usijaribu kufata muongozo ambao wao wameupendekeza?
Ukisema wakristo wanadai chimbuko lao ni Yesu pia ukumbuke Yesu huyo alikuwa mbinguni. Kwa hiyo usaijiwekee dhana kwamba kwasababu yesu alizaliwa hapa duniani basi ndio mwanzo wa ukristo, wakristo walikuwa wanamjua Yesu akiwa mbinguni a ni biblia hiyo hiyo imeeleza namna alivyo teuliwa kuja duniani.
Namna gani sahihi ya kujua ukweli ambayo haizingatii misingi ya imani husika iliyojiwekea?
Leo hii mtu akisema uislamu ni uongo kwasababu unaabudu jiwe linaloitwa kaaba, mtu huyo ni lazima atakuwa yuko katika imani pingamizi na yako na amefanya comparison ya kile mnacho kiabudu kwa kulinganisha na yale ambayo ni sahihi kwa dini yake na makatazo ya dini yake ambayo yanakataza vitu vingi ikiwemo ibada za kuabudu mawe
Hata wewe hapa kusema kwako jambo fulani linafanywa na wakristo kwa kupotosha , on other hand kuna misingi ya kiimani unayo shkilia kupima usahihi wa vitu vingine vilivyo nje na imani yako.
Biblia kuwa a vitabu 72 au 73 sio jambo la kufanya imani yao iwe ya uongo, maana hata nyinyi mnamatabaka mengi na mnapishana kwenye mambo mengi kwenye vtabu vyenu vya dini na hata humu tunawaona mkizozana wenyewe kwa wenyewe.
Mimi hoja yangu nashauri muache kutumia hivi vitabu vya dini kama hoja za uthibitisho dhidi ya atheists kwasababu hata nyinyi kwa nyinyi hamkubaliani na wewe umekiri kuwa haiwezekani mkawa kitu kimoja
Ugumu unaoupata wewe kushawishika kwa hoja za biblia na kuziona jinsi ambavyo hazifai kuwa uthibitisho wa kukushawishi kukubali ukristo basi fikiria hali hiyo hiyo inanipata mimi pale ambapo unajaribu kunielezea habari za Allah.