Utetezi wa uumbaji kimahesabu na kifizikia: Mathematician's and theoretical physicist appeal to creation

Utetezi wa uumbaji kimahesabu na kifizikia: Mathematician's and theoretical physicist appeal to creation

Siyo kisichoshikika hakiitwi kitu. Wazo nalo ni kitu chenye sifa anuai zake. Lakini hata tukijaalia wazo likawa si kitu. Wapi linatoka wazo ? Wazo halimiliki wazo halina utambuzi, vipi ulipe sifa ambayo si yake. Mfano wazo la kujenga, vipi ulipe sifa ya kujenga hali ya kuwa lenyewe halijafanyiwa kazi ?

Maana yake wazo haliwezi kuwa Mola. Ni sawa na sisi tumetoka kwa Mola kwahiyo sisi hatuwezi kuwa Mola sababu hatuna sifa alizo nazo Mola kwa dhati yake.

Uhai siyo wazo, wazo haliwi wazo mpaka liwe limewaziwa na kuwasilishwa.
Sawa sio kitu, ni zaidi ya kitu. Ni kama energy fulani lakini sio energy, bali ni hali tu. Sijui kuhusu nyie/wewe kuhusu tulivyolivyo na Mola alivyolivyo. Kumbuka tumesema wazo linalojitambua. Intelligent idea ama consciousness. Mawazo ambayo hayamiliki utambuzi yapo na yanakuwa yametengenezwa na yale yanayomiliki utambuzi ambayo nayo yapo[sisi]. Na yote yanaishi katika Babalao - Super Intelligence linalouwezeha hata huo utambuzi wenyewe kuwepo

Kwetu sisi, japo tunakubali kwamba Mungu mwenyewe hafananishwi.....tunafahamu kwamba sisi[wanaadamu] kiuhalisia/essence ni mfano wa Mungu. Au tuambie wewe ni nani/nini haswa kabla hatujaendelea.

Sawa sifa alizo nazo mola hatuzifikii kwa dhati yake, perfection lakini hilo halituzuii kujenga dhana kama - Mungu ni Baba yetu etc
 
Hoja kila mtu anazo utofauti ni kipimo cha kuangalia authenticity ya hizo hoja kama zime qualify

Ukitumia Quran kama ndio kipimo wa madai yako ambayo unasema ni sahihi kumbuka unaweza kukosolewa na mkristo kupitia biblia yake
Hapa umerudia nilichokiandika. Weka nukta.

Kuhusu Qur'aan kuwa kipimo hili liko wazi sababu kuna sifa anuai kwazo zinafanya hilo liwe.

Ukija katika Biblia uongo wake unakuja katika historia na namna ya uandishi wake na iko hivyo katika vitabu vingine. Biblia haina chain na hii si kwa bahati mbaya, Biblia haikuachwa na Yesu. Sasa kuna sababu nyingi kwazo zinafanya Biblia isiwe marejeo na kuonyesha si kitabu kutoka kwa muumba. Sasa watakao pinga watapinga kiushabik na mapenzi na si kwa ukweli na ubainifu.
Sasa mjadala unaohusisha hoja za vitabu ni infinite kwakua hakuna aliyetayari kukubali kitabu chake ni uwongo na kitabu cha mwingine ndio cha kweli.
Hauwezi kuwa na ukomo, sababu wapo wanao kuja kukubali ukweli na wapo wanao kaidi kwa maslahi yao, hii ipo tangu zama za mitume na manabii. Ndiyo maana huwa hatulazimishani wewe uukubali ukweli.
Hata saizi ukiwa na hoja ya ku challenge bible ambayo hoja biyo wewe unaona iko sahihi kuonesha kasora ya bible ni lazima kwa namna moja uwe umeipitisha katika misingi ya Quran
Sahihi kabisa lazima iwe hivyo kwa sababu maalumu. Qur'aan ni kamilifu na haina kosa hata la herufi, na historia yake iko wazi na inajulikana.
Yani utasema jambo fulani wakristo mmepotosha kwa kuzingatia sababu ambazo hilo jambo lilivyoelezwa kwenye Quran

Yani by default umejitengenezea msimamo kuwa Quran ndio msingi sahihi muda wote
Huo ndiyo ukweli na siyo tu msimamo bali ni msimamo wa kielimu na uhalisia.

Ndiyo maana watu wako huru kukosoa jambo analo ona haliko sawa.
Lakini ukumbuke hayo yote unayoweza kuyafanya, pia hata wakristo ndio hivyo hivyo.
Hii siyo hoja kabisa, lazima tuhakiki kila kinachowasilishwa na upande pinzani.
Na ndio maana nasema hoja ya kusema Mungu hivi Mungu vile kwasababu kitabu kimesema haipaswi kutumiwa kwa watu rational ilihali miongoni mwenu tu mnaomini Mungu hamkubaliani na viatabu vya nyinyi kwa nyinyi
Hakuna mtu mwenye akili anaye pinga uwepo wa Mola. Hili kwanza unatakiwa uliweke akilini, kipimo cha mtu asiye na akili timamu ni kumkana Mola.

Hapa tunarudi katika ile nukta ya msingi, kuna kujiona upo fulani wakati kiuhalisia huna kitu hicho. Mfano wewe unajiona una akili, lakini tukiijadili akili kwa mawanda yake siyo wewe tu bali hata hao wakubwa wenu hawana akili timamu.

Leo hii nikikuuliza swali rahisi kwanini umekuwepo hapa duniani ? Huna jibu la swali hili, halafu muda huo huo unajiona una akili. Huku ni kuikosea adabu akili na watu wake.
 
Nakuuliza swali rahisi hapa, wazo linaweza vipi kuamua jambo au kupanga mambo ?
Mbona rahisi tu; ni kama ambavyo wewe ni wazo linalojielewa na ndio maana umepanga na umeamua kuuliza hili swali. Wazo linalojielewa lina nguvu hizo......au kama draga anavvyopendaga kusema nguvu iliyopo ndani yako imetokeza akili na kuleta mpango huo.

Na falsafa usiibeze maana inatusaidia kuujua ukweli na uhalisia, ni kifaa kimojawapo tulichonacho. Tukitumie
 
Mbona umekimbia darsa nilikuwa nakupa , muhammad anasema mbwa wote weusi ni mashetani
Mpo na mada gani huko, kuwasoma nyie wawili midiscuss inatupaga somo sie wengine haswa tusio na ujuzi mzuri wa Qura'an. Link tafadhali
 
Nacho shangaa ni oale wanapotaka kutushawishi sisi tusio amini Mungu kwa nja ya vitabu

Ya i vitabu ambavyo wao kwa wao hwakubaliani kama ni vya kweli, vitabu hivyo hivyo wanataka kuvitumia kama uthibitisho kwetu

Hiyo hatukubali, kama wataona vitabu ni hoja za msingi kwenye uthibitisho basi wafanye makubaliano wampitishe

Mungu mmoja: Mwenye sifa moja, eidha yehova ambaye kasema kwenda peponi ni lazima umkubali Yesu na kuoa mke zaidi ya mmoja ni uzinzi

Au Allah ambaye yuko mbingu ya 7 kasema watu wasali swala tano, kufunga kula, uoe wake wa 4 na kutakuwa na adhabu ya kaburi kwa waovu nk.

Hapo inatakiwa achaguliwe Mungu mkoja na mmoja atemwe.

Kitabu kimoja: Maana yake kuna kitabu hapo kinatakiwa kipitishwe kua ni batili ili hicho kimoja kiwe cha kweli),

Pepo moja: Maana yake hapa wakubaliane ni either wakubaliane pepo yenye kuimba na kusifu au yenye bikra 72. Hapa pia linahitajika jibu moja tu

Kama wao watashindwa kuafikiana jibu moja basi itakuwa ni ujinga kutumia vitabu hivyo kama hoja ya uthibitisho kumthibitishia mtu asiyeamini katika Mungu.
Unatumia kitabu kilichoa anza kabla
 
Mbona rahisi tu; ni kama ambavyo wewe ni wazo linalojielewa na ndio maana umepanga na umeamua kuuliza hili swali. Wazo linalojielewa lina nguvu hizo......au kama draga anavvyopendaga kusema nguvu iliyopo ndani yako imetokeza akili na kuleta mpango huo.

Na falsafa usiibeze maana inatusaidia kuujua ukweli na uhalisia, ni kifaa kimojawapo tulichonacho. Tukitumie
Wazo au neno ni kitu hai, mchawi anaroga kwa neno, Muislamu, Mkristo kupitia neno anaponya
 
Wazo au neno ni kitu hai, mchawi anaroga kwa neno, Muislamu, Mkristo kupitia neno anaponya
Asante kwa msaada umenisaidia pakubwa kupeleka mbele hii concept.

Tukitumia fact ulotoa kuhusu ulozi wa kutumia maneno/spells inawezekana huwa wanajenga wazo kwa kusema maneno halafu ili kuyapa uhai 'wanauiba' kutoka kwa kiumbe hai maana wao hawawezi kuumba uhai!!

Ndio hapo makafara, na kuchinja kuku inapokuja nadhani - I am just speculating
 
Maneno ni Roho kamili tena inayoishi neno ni uhai,thus ukimlaani mtu mfano kumtamkia maneno au kumsomea albadili asipoyablock Yale maneno anadhurika.
 
Maneno ni Roho kamili tena inayoishi neno ni uhai,thus ukimlaani mtu mfano kumtamkia maneno au kumsomea albadili asipoyablock Yale maneno anadhurika.
Basi mororo,

Ila mi nitataka kitu kimoja tukiweke sawa kuwa maneno yaweza kuwa neutral, au yenye nguvu hasi, au yenye nguvu chanya. Ni roho ila zinahitaji kuwa powered na nguvu fulani na tayari zinayo hiyo nguvu ndio maana zipo.

Neno/wazo linaweza kuwa powered na Nguvu za Nuru
Neno/wazo linaweza kuwa powered na nguvuzagiza
Au likawa neutral likasubiri kuwa powered na wewe unayelipokea au unayelitoa

Nitakuwa sawa?
 
Hapa umerudia nilichokiandika. Weka nukta.

Kuhusu Qur'aan kuwa kipimo hili liko wazi sababu kuna sifa anuai kwazo zinafanya hilo liwe.

Ukija katika Biblia uongo wake unakuja katika historia na namna ya uandishi wake na iko hivyo katika vitabu vingine. Biblia haina chain na hii si kwa bahati mbaya, Biblia haikuachwa na Yesu. Sasa kuna sababu nyingi kwazo zinafanya Biblia isiwe marejeo na kuonyesha si kitabu kutoka kwa muumba. Sasa watakao pinga watapinga kiushabik na mapenzi na si kwa ukweli na ubainifu.

Hauwezi kuwa na ukomo, sababu wapo wanao kuja kukubali ukweli na wapo wanao kaidi kwa maslahi yao, hii ipo tangu zama za mitume na manabii. Ndiyo maana huwa hatulazimishani wewe uukubali ukweli.

Sahihi kabisa lazima iwe hivyo kwa sababu maalumu. Qur'aan ni kamilifu na haina kosa hata la herufi, na historia yake iko wazi na inajulikana.

Huo ndiyo ukweli na siyo tu msimamo bali ni msimamo wa kielimu na uhalisia.

Ndiyo maana watu wako huru kukosoa jambo analo ona haliko sawa.

Hii siyo hoja kabisa, lazima tuhakiki kila kinachowasilishwa na upande pinzani.

Hakuna mtu mwenye akili anaye pinga uwepo wa Mola. Hili kwanza unatakiwa uliweke akilini, kipimo cha mtu asiye na akili timamu ni kumkana Mola.

Hapa tunarudi katika ile nukta ya msingi, kuna kujiona upo fulani wakati kiuhalisia huna kitu hicho. Mfano wewe unajiona una akili, lakini tukiijadili akili kwa mawanda yake siyo wewe tu bali hata hao wakubwa wenu hawana akili timamu.

Leo hii nikikuuliza swali rahisi kwanini umekuwepo hapa duniani ? Huna jibu la swali hili, halafu muda huo huo unajiona una akili. Huku ni kuikosea adabu akili na watu wake.
Nieleze dini gani iliwahi kudai kitabu chake sio cha kweli nakukitaja chako kua ndio kitabu cha kweli?

Muislam kuendelea kunieleza ambavyo Quran ni kitabu sahihi na vingine sio, sio jambo la kushangaza

Kuisema biblia kuwa ni kitabu chenye makosa na wakati wewe ni muislamu na hicho kitabu kimewekewa utaratibu wa namna gani ya kukisoma

Mfano wakristo wanasema biblia haisomwi kama gazeti. Ili uweze kuielewe biblia lazima upate muongozo wa roho mtakatifu (jambo ambalo wewe katika uislamu halipo na linapingwa)

Na wanakuambia ukishukiwa na roho mtakatifu huwezi kuiona biblia ina makosa.

Kwa hiyo wakristo huo ndio utaratibu wao, sasa unaposema kwenye biblia kuna makosa fulani na fulani maana yake uliisoma kama gazeti bila kuvuviwa roho mtakatifu.

Mtu yeyote ambaye anapinga biblia kuwa ina makosa basi mtu huyo hakushukiwa na roho mtakatifu na alisoma biblia kama gazeti.

Sasa mpaka hapo unaweza kumuambia nini mkristo kuwa biblia ina makosa akakuelewa?

Mimi nimeliona hilo na ndio maana napendekeza m reason kwa facts na sio kutumia maandiko ya vitabu vyenu.
 
Tatizo lipo kwenye watu kutaka kutumia mila na desturi zao kama sheria ya kufuatwa na wote duniani, ego,nationalism etc

Sasa ili wafanikishe hilo jambo wanaamua kusema ni maagizo ya Mungu

Lakini sijui kwa waamini wengine lakini binafsi naona Mungu ni mkuuuuubwa mno kuanza kufuatilia eti tuoaneje, au tutumie siasa zipi. Cha msingi tu je hivyo vitu vinaijenga jamii au vinaibomoa amueni kama jamii ilostaarabika.

Maamuzi ya haki yanayofanywa duniani Mungu huwa anayapitisha wala haina ubaaaabe. No.

So katika jamii ya wakulima ni sahihi kusali mara moja kwa wiki na usiku labda. Ila kwa wanaovuna mafuta ni sahihi kwao kusali kila baada ya masaa matano.

Jamii yenye almost idafi sawa ya jinsia ni sahihi mke mmoja mme mmoja na jamii ambayo wanaume wamepotezwa vitani ni sahihi mme mmoja wake wawili-wanne.

Hakuna cha dhambi wala nini kama hilo jambo ni jema kwa 'afya' ya jamii husika bro
Ukikataa sera ya kusema jambo fulani ni maagizo ya Mungu automatically umepinga authenticity ya vitabu vya dini.

Hapo unakuwa umepinga habari nyingi ikiwemo na habari za uwepo wa Mungu mwenyewe

Ukisema hakuna cha dhambi, hapo unakuwa unaongelea Mungu wa dzaini nyingine ambaye unamjua wewe peke yako
 
Mbona rahisi tu; ni kama ambavyo wewe ni wazo linalojielewa na ndio maana umepanga na umeamua kuuliza hili swali. Wazo linalojielewa lina nguvu hizo......au kama @draga anavvyopendaga kusema nguvu iliyopo ndani yako imetokeza akili na kuleta mpango huo.
Hiki ulichokiandika kimemili katika falsafa zaidi kuliko uhalisia. Yaani umejibu swali bila kujua wazo ni nini, hii imekupekea kukosea katika kujibu swali.

Hujaonyesha mimi nawezaje kuwa wazo ? Mimi ni nafsi ambaye nimeundwa au ni mjumuiko wa roho na mwili.

Labda tujadili kwanza maana ya tamko wazo. Sababu hiki mnachokiandika kwanza ni matumizi mabaya ya tamoo wazo, kwa maana lugha inakataa matumizi haya ya tamko hili wazo kulipa sifa za uhai yaani kiumbe chenye akili.

Naomba utusaidie au unisaidie kitu kimoja, naomba unipe maana ya tanko "Wazo".
Na falsafa usiibeze maana inatusaidia kuujua ukweli na uhalisia, ni kifaa kimojawapo tulichonacho. Tukitumie
Hapa itabidi unipe ushahid au kuonyesha wapi falsafa imekusaidia kuujia ukweli na uhalisia. Maana yake ingekuwa hivyo basi kina Plato, Socrates, Aristotle, Pythagoras wote wangepatia katika kuelezea chanzo cha ulimwengu na maisha, au wana Atomu kadhalika.

Nachokijua mimi kuhusu falsafa na Wanafalsafa ni kuwa walikuwa na maswali sahihi ila walikosa njia za kuwapa majibu sahihi.
 
Unatumia kitabu kilichoa anza kabla
kama kipi?

Maana hivyo vya kale zaidi vimeongelea Mungu wengi (Gods)

Kuna dini ya summerian ambayo kuna kaka wa Mungu, dada, baba, nk

Hao ndio walioongelea habari za heaven na earth, habari hizo ambazo baada ya miaka 1000 Quran ikaja kuziandika halafu modern muslim wamekuwa wakizitumia kusema Quran imezungumzia bing bang na kuwa sayansi inatumia kitabu chao kufanya utafiti.

Zipo ancient texts za kihindi (vedana) zilizoandika habari za embryology miaka elfu kabla ya ujio wa Quran, lakini Quran imekuja kuyaandika hapo juzi tena kwa kifupi hata yayajaenda in deep kama ilivyoelezewa kwa dini ya kihindu lakini ndio yamekuwa yakitumika kuoneshea ukuu wa Allah.

Maandiko ya kale ni mengi sana na waumini wa hizi dini mbili (wakristo&waislam) wengi hawaelewi kwasababu wamejifungia katija pazia la kusoma yale yanayowahusu dini yao tu.
 
Nieleze dini yake iliwahi kudai kitabu chaje dio cha kweli nakukitaja chako kua ndio kitabu cha kweli?
Sijaelewa swali lako.
Muislam kuendelea kunieleza ambavyo Quran ni kitabu sahihi na vingine sio, sio jambo la kushangaza
Na lengo siyo kukushangaza na hupaswi kushangaa, bali unatakiwa uujue ukweli au onyeshe uongo wa hili. Hakuna cha ziada.
Kuisema biblia kuwa ni kitabu chenye makosa na wakati wewe ni muislamu na hicho kitabu kimewekewa utaratibu wa namna gani ya kukisoma
Hapa sijakuelewa kadhalika. Fafanua.
Mfano wakristo wanasema biia haisomwi kama gazeti. Ili uweze kuielewe biblia lazima upate muongozo wa roho mtakatifu (jambo ambalo wewe katika uislamu halipo na linapingwa)
Safi kabisa, hoja siyo nani kasema hoja je kinachosemwa ni sahihi. Hili ndiyo la msingi. Sisi tunaambiwa hivi kama si kuja mitume leo hii wangesema watu kila wanachokitaka na wasikemewe au kukosolewa.

Kwa akili tu ya kawaida, kauli hii inakashiwa kwa hoja za wazi.
Na wanakuambia ukishukiwa na roho mtakatifu huwezi kuiona biia ina makosa
Swali la msingi kwa mtu mwenye akili atauliza na kitaka kujua hilo jambo je ni kweli ? Sasa usiishie tu kusema. Kama huwezi kuona bia ni haramu, mafundisho ya Yesu yanasemaje kuhusu Bia.
Kwa hiyo wakristo huo ndio utaratibu wao, sasa unaposema kwenye biblia kuna makosa fulani na fulani maana yake uliisoma kama gazeti bila kuvuviwa roho mtakatifu.
Hii siyo kweli sababu hayo wanayo yasema hayatoki kwa mtume wala nabii yoyote na wala hayana asili. Sisi tutawauliza mafundisho haya wameyapata wapi ?

Kingine kuna uhalisia, jambo hilo linapingana na uhalisia ulivyo.
Sasa mpaka hapo unaweza kumuambia nini mkristo kuwa biblia ina makosa akakuelewa?
Yapo mengi sana ya kuwaambia na wapo wanao elewa na kukiri ya kuwa maandiko yako hayatoki kwa Allah.
Mimi nimeliona hilo na ndio maana napendekeza m reason kwa facts na sio kutumia maandiko ya vitabu vyenu.
Hili umeliona lakini limeonyesha ni namna gani hujui kukosoa hoja au kuhoji mambo kwa undani, hili si kosa lako sababu hata hao ulio chukua fikra hizo uwezo huo hawakuwa nao. Hili rahisi sana.
 
Ukikataa sera ya kusema jambo fulani ni maagizo ya Mungu automatically umepinga authenticity ya vitabu vya dini.

Hapo unakuwa umepinga habari nyingi ikiwemo na habari za uwepo wa Mungu mwenyewe

Ukisema hakuna cha dhambi, hapo unakuwa unaongelea Mungu wa dzaini nyingine ambaye unamjua wewe peke yako
In simple terms;

Sio kila kilichoko kwenye maandiko ni maagizo mojakwamoja ya Mungu nyingine ni mila desturi na taratibu za jamii husika.

Mr Scars, unaweza kumuamini Mungu bila ya kufungwa na maandishi/maandiko fulani fulani au elimu fulani. Ndiyo maana mtu yeyote anaweza kusoma fizikia, hesabu na baiolojia na akamuona Mungu

Nilisema hakuna dhambi kwa kitu chenye 'AFYA' kilichoamuliwa na wanajamii husika kwa akili njema kabisa NA KUSUDI JEMA kuwa utamaduni wao
 
Sijaelewa swali lako.

Na lengo siyo kukushangaza na hupaswi kushangaa, bali unatakiwa uujue ukweli au onyeshe uongo wa hili. Hakuna cha ziada.

Hapa sijakuelewa kadhalika. Fafanua.

Safi kabisa, hoja siyo nani kasema hoja je kinachosemwa ni sahihi. Hili ndiyo la msingi. Sisi tunaambiwa hivi kama si kuja mitume leo hii wangesema watu kila wanachokitaka na wasikemewe au kukosolewa.

Kwa akili tu ya kawaida, kauli hii inakashiwa kwa hoja za wazi.

Swali la msingi kwa mtu mwenye akili atauliza na kitaka kujua hilo jambo je ni kweli ? Sasa usiishie tu kusema. Kama huwezi kuona bia ni haramu, mafundisho ya Yesu yanasemaje kuhusu Bia.

Hii siyo kweli sababu hayo wanayo yasema hayatoki kwa mtume wala nabii yoyote na wala hayana asili. Sisi tutawauliza mafundisho haya wameyapata wapi ?

Kingine kuna uhalisia, jambo hilo linapingana na uhalisia ulivyo.

Yapo mengi sana ya kuwaambia na wapo wanao elewa na kukiri ya kuwa maandiko yako hayatoki kwa Allah.

Hili umeliona lakini limeonyesha ni namna gani hujui kukosoa hoja au kuhoji mambo kwa undani, hili si kosa lako sababu hata hao ulio chukua fikra hizo uwezo huo hawakuwa nao. Hili rahisi sana.
Nimerudia kuhariri hizo sehemu ambazo nimeandika kimakosa unaweza kurejea kuisoma tena kama hutojari

Najua lengo halikuwa kunishangaza ila nakutifautishaje na mkristo au mtu mwingine tofauti na imani yako ambaye anadai yuko sahihi na wengine walio kinyume na yeye (ikiwemo na wewe) kuwa mmepotoka?

Lakini hapo chini umejibu mfano wangu ambao ulikuwa unaonesha protocols za wakristo kuisoma biblia.

Wewe umedai kuwa hoja ni kuangalia kinachosemwa ni sahihi?

Sasa hapa ndio tunarudi pale pale je hicho ulichokisoma kwenye biblia kabla ya kukifikiria ni sahihi au lah je ulishushiwa roho mtakatifu wa kukuongoza kusoma hiyo biblia?

Kama jibu hapo litakuwa ndio basi biblia ni kweli kwasababu since ukiongozwa na roho mtakatifu huwezi kuona makosa kwenye biblia.

Lakini endapo utasema hukuhitaji roho mtakatifu basi hapo unakuwa umesha feli kufikia vigezo ambavyo vinapaswa kufuatwa ili kuielewa biblia.

Hoja yako ya kusema unapima jambo kwa uhalisia napo hii inaleta majadala mwingine

Kwa mfano jambo lolote ambalo limehusianishwa na muujiza huwa ni ngumu sana kuliweka kwenye uhalisia.

Hata wewe kuna habari za Quran zinazosema mtume alipaa angani mpaka mbinguni na farasi aitwaye Buraq (kama nitakuwa sahihi) jambo hilo kwako unaweza ukalirahisha kuwa ni uhalisia kwa dhana ndogo tu ya kusema ni miujiza

Lakini leo hii katika ulimwengu swala hilo halielezeki kwa namna yeyote bila kuacha utata na ndio maana muujiza unatumika ku cover gape la kuziba mianya ya maswali magumu kama hayo.
 
In simple terms;

Sio kila kilichoko kwenye maandiko ni maagizo mojakwamoja ya Mungu nyingine ni mila desturi na taratibu za jamii husika.

Mr Scars, unaweza kumuamini Mungu bila ya kufungwa na maandishi/maandiko fulani fulani au elimu fulani. Ndiyo maana mtu yeyote anaweza kusoma fizikia, hesabu na baiolojia na akamuona Mungu

Nilisema hakuna dhambi kwa kitu chenye 'AFYA' kilichoamuliwa na wanajamii husika kwa akili njema kabisa NA KUSUDI JEMA kuwa utamaduni wao
Narudi pale pale

Ikiwa kama sio kila kilichoandikwa kwenye maandiko ya vitabu vya dini ni cha kweli utajuaje kama katika visivyoio vya kweli sio pamoja na habari za uwepo wa Mungu?
 
Narudi pale pale

Ikiwa kama sio kila kilichoandikwa kwenye maandiko ya vitabu vya dini ni cha kweli utajuaje kama katika visivyoio vya kweli sio pamoja na habari za uwepo wa Mungu?
Kwa sababu nnayo 'fitrah' hata kama kungekuwa hakunaga maandiko ningejua tu kuwa Mungu yupo.

Unakumbuka nilikuambiaga watu binafsi walianza na dini ya ki evolution inayoelekeana na ukweli lakini sio ile KWELI halisi? Baadaye ndiyo tukasaidiwa na revelation ili kukamilisha?

So hata bila maandiko Mungu Yupo, utashi unaongoza katika hilo kiotomati. Wengine hapa bro tumeanzia kwenye Sayansi kumsoma Mungu halafu ndio tukakamilisha na maandiko!!! shangaa....... shangaa sana
 
Kwa hiyo kwako wewe wazo la Mungu unalipata kupitia assumption baada ya kujiuliza maswali kadhaa ambayo ukakosa majibu?
 
Back
Top Bottom