Wazo ni kama dhana fulani au nadharia fulani hivi. Wazo sio kitu cha kushikika, kwa hiyo unapolichambua usilifix kama kitu fulani hautalielewa ukifanya hivyo. Wazo latoka kwa Mola na ndiyo Mola havitenganishiki sawa tu na ilivyo wazo-hai la mtu na mtu mwenyewe visivyoachanishika.
Siyo kisichoshikika hakiitwi kitu. Wazo nalo ni kitu chenye sifa anuai zake. Lakini hata tukijaalia wazo likawa si kitu. Wapi linatoka wazo ? Wazo halimiliki wazo halina utambuzi, vipi ulipe sifa ambayo si yake. Mfano wazo la kujenga, vipi ulipe sifa ya kujenga hali ya kuwa lenyewe halijafanyiwa kazi ?
Maana yake wazo haliwezi kuwa Mola. Ni sawa na sisi tumetoka kwa Mola kwahiyo sisi hatuwezi kuwa Mola sababu hatuna sifa alizo nazo Mola kwa dhati yake.
Uhai siyo wazo, wazo haliwi wazo mpaka liwe limewaziwa na kuwasilishwa.
Haya mambo unapokosea wewe unayaongelea kifalsafa zaidi ndiyo maana ynakuwa mbali na jambo husika, yaani huligusi jambo husika.
Jaribu kuyaelezea haya mambo kiuhalisia, shida ya falsafa ni kama kuuzunguka mbuyu. Yaani unakuwa unazunguka tu pasi na kuugusa mbuyu husika, ndicho unachokifanya wewe.
Kama tumeshaona wenye vitabu vinavyodaiwa kuwa ni vya Mungu bado vitabu vyao vinapingana na kuonesha hali ya kutofautiana mafundisho na maagizo wanayosema yametoka kwa Mungu?
Ndiyo maana kila siku huwa nawakosoa kwa kutokuwa kwenu watafiti na kufatilia mambo. Usome Ukristo katika misingi yake, kadhalika Uislamu na sini nyingine. Mtu mwenye akili timamu huuliza kama Mola ni mmoja kwanini kuna dini nyingi ? Jibu sahihi ni kuwa Mola ni mmoja na dini lazima iwe moja. Jalia Mola wangekuwa zaidi ya mmona hii dunia ingeendeshwaje ? Lazima kungekuwa na vuta ni kuvute huu ndiyo uhakika wa mambo.
Kwahiyo wenye akili timamu lazima watataka kujua nani yuko sahihi na nani ni kinyume chake. Vipi utajua nani mkweli na nani si mkweli, haoa lazima uweke nia ya kutaka kujua mambo na si kama mnavyo fanya nyinyi, kutaka kujitutumua na hamna mnachokijua.
Sisi huwa tunasema hivi "Kila mmona ana dai Laila ni mpenzi wake, lakini tukimuuliza Laila juu ya hilo ana kana ya kuwa hakua mpenzi wake hata mmoja katika hao ." Hii na maanisha ya kwamba lazima mambo uyajue ndiyo uhitimishe.
Point hapa ni kuwa, kumbe kitabu au aina fulani ya maandiko yanayodaiwa kuwa yameandikwa na Mungu au kwa muongozo wa Mungu sio uthibitisho wa kuonesha kweli kilichoandikwa humo kimeandikwa
Sahihi kabisa hali iko hivyo.
Kwa hiyo una suggest nini hapo?
Kila mtu mwenye hoja zake aruhusu kuhojiwa na kuthibitisha hoja zake na kujibu kila anachoulizwa. Sababu hali ilivyo ni kiwa mchana wake ni sawa na usiku wake hapitei humo ila mwenye kutaka apotee. Mambo yako wazi mno.
Utumie maelezo ya kitabu kama hoja ya uthibitishi kwa atheist kueleza habari za Mungu wakati kuna theists wenzako hawakubaliani na kitabu chako kuwa ni uthibitisho wa Mungu?
Hili nalo siyo hoja, ndiyo maana sisi huwa tunasema hivi leteni hoja zenu kama nyinyi mnasema kweli. Kwahiyo kila mtu ataleta hoja zake. Sababu ukweli uko wazi lazima atajulikana nani mkweli na nani muongo, sababu sote tumejaaliwa neema ya akili na kutafakari.
Kuna vitu huwa havipingani na akili kabisa, hili wengi hawalijui na kama wanalijua basi wana kaidi. Mfano tu suala la kwamba Mola yupo, hili jambo halipingani kabisa na akili, yeyote apingaye jambo hilo, aidha :
1. Ni mjinga hajui anachokipinga
2. Au ni mpumbavu
3. Au anavyo vyote viwili.
If I were you I would prefer reasonable facts and ignoring text scriptures as evidence.
Maandiko ndiyo uhalisia wenyewe. Mola wetu baada ya kufunga mlango wa utume na akatupa ishara, aliyaacha mambo wazi mno. Watu siyo kwamba wanaukataa ukweli kwamba unakasoro la hasha wapo wanao kataa ukweli kwa ajili ya malsahi yao. Hili kwanza liweke akilini.
Kingine ufunuo haupingani na ufunuo, ukiona akili yako inapingana na ufunuo kuna moja kati ya mawili au una yote, aidha umjinga au mpumbavu au una vyote.
Sababu uhalisia ndiyo facts yenyewe, mfano wa fact hii je kwamba hii dunia imejiumba au imetikana pasi na chochote ? Hii ni facts yaani uhalisia, huwezi kupinga jambo hili, majibu yake huonyesha ya kuwa hii dunia haiwezi kutokea pasi na chochote au kujiumba sababu singi wa wa ujenzi unajulikana, ni ufinyu wenu tu wa kutofikiria mambo katika uhalisia wake, ndiyo maana hili wakana mungu wote hamjawi kutuambia ya kuwa sis imekuwaje mpaka tukawepo hapa duniani ?
Mola wetu ametuumba sote na kitu kiitwacho "Fitrah (Inert disposition)" hichi kitu kinamfanya mtu asipinge uwepo wa Mola endapo atafikiria kwa undani zaidi na lazima atakiri ya kuwa hii dunia imeumbwa. Hii hali anayo kila mtu.
Leo hii wakana mungu ukiwauliza kwanini tunaishi ? Hawana jibu sahihi, je tunaishi na kufa tu, halafu basi ? Maana yake haya maisha hayana maana. Sasa akili iliyo salama inakataa hili, inakwambia lazima kuna lengo maalumu la kutufanya sisi tuishi na kuwepo hapa, sasa kuanzia hapa akili yako itaonekana inafanya kazi vizuri. Sasa wakana Mungu akili hii hawana, wao ni kukaririshana mawazo ya wajinga fulani na wao wanayabeba kama yalivyo.